Mbinu za kivita zinavyompaisha Membe

Mbinu za kivita zinavyompaisha Membe

Sisi sote ni watoto wa kambo
sijaona mahusiano ya hizo mbinu za kivita na ulichokizungumzia juu ya Membe.

Membe nitamkumbuka kama aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje kipindi tulichokuwa na migogoro na nchi za Rwanda na Malawi, zaidi ya hapo sina ninachokumbuka kumhusu huyu mtu.

Ninachoona kwake ni mtu anaye endekeza siasa za makundi na anayeamini katika matabaka.

Vile vile asiyemvumilivu kisiasa kwani kipindi kile anataka kugombea alituambia wazi kuwa akifanikiwa kuwa Rais maadui Zake 11 watahama nchi.

Vile vile kesi yake na Musiba ni kiashirio kingine cha ukosefu wa uvumilivu kisiasa unless anataka kuitumia hiyo kesi kama Jukwaa la kumrejesha katika lingo za kisiasa.

ili kujua kuwa Membe sio mvumilivu kisiasa kauli ndogo tu ya Rostam imetosha kabisa kumfanya aweke hadharani mipango yake ya kugombea Urais 2020.
 
Kiongozi hoja siyo Membe kufaa au kuto faa, Nimejadili baadhi ya mbinu anazotumia. Hata hivyo haya nimawazo yangu nikilinganisha na nadharia za mwandishi wa kivita bwana Sun Tzu wa "the Art of War"
Katika andiko lako la awali/yaani mada hii iliyopo mbele yetu,nikupongeze kwa udadavuzi ulioufanya,hawa watu wengine upeo wao wa kufikiri ndio umefikia hapo na watu kama hawa mimi huwaita mashabiki wasiokua nahoja.

Pia nikupongeze kwa majibu yaliyojaa hekima kumjibu shabiki huyu asiyekua na hoja.Tafadhali usikatishwe tamaa na watu kama hawa.
 
Nimesoma mara mbili mbili kama sio mara tatu tatu, niseme tu nashukuru saana kwa kunitia moyo. Nahidi kuendelea kuandika chambuzi nyingi zenye tija kwa jamii yangu .Kwani ulimwengu wa vita vya silaha umepitwa na wakati tupo kwenye ulimwengu wa vita vya hoja.
 
Uko vizuri umechambua pasipo kuweka hisia binafsi hongera sana umenijenga.
Asante, umenijenga pia kwa kunitia moyo. Sasa nagundua kuwa kuna watu muhimu kama,wanaothamini uchambuzi wangu.
 
sijaona mahusiano ya hizo mbinu za kivita na ulichokizungumzia juu ya Membe.

Membe nitamkumbuka kama aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje kipindi tulichokuwa na migogoro na nchi za Rwanda na Malawi, zaidi ya hapo sina ninachokumbuka kumhusu huyu mtu.

Ninachoona kwake ni mtu anaye endekeza siasa za makundi na anayeamini katika matabaka.

Vile vile asiyemvumilivu kisiasa kwani kipindi kile anataka kugombea alituambia wazi kuwa akifanikiwa kuwa Rais maadui Zake 11 watahama nchi.

Vile vile kesi yake na Musiba ni kiashirio kingine cha ukosefu wa uvumilivu kisiasa unless anataka kuitumia hiyo kesi kama Jukwaa la kumrejesha katika lingo za kisiasa.

ili kujua kuwa Membe sio mvumilivu kisiasa kauli ndogo tu ya Rostam imetosha kabisa kumfanya aweke hadharani mipango yake ya kugombea Urais 2020.
Deception
 
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Yupo Ofisini Anaendelea Na Majukumu
Hawa Wengine Wafuate Utaratibu Muda Ukifika
Kutwa anapita mikoani akifanya kampeni anagawa pesa kwa wananchi nani asubiri?
 
View attachment 1101087
Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Tanzania Bernard Membe ambaye amekuwa akitajwa kuwa na mpango wa kugombea tiketi ya urais 2020, amekuwa na mbinu za kipekee ambazo zinazidi kung’arisha Kisiasa. Jambo ambalo limenifanya nijadili mbinu za waziri huyu wa Zamani, ambae amendelea kubamba kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Baada ya kubaini mbinu na mikakati yake imekuwa ikishabiana sana na mbinu za kivita kwenye oparesheni mbalili mbali za kijeshi. Nimeona nijadili mbinu hizi kama zinavyo ainishwa na mwandishi wa maswala ya kivita bwana Sun Tzu kwenye kitabu chake maarufu cha ‘the Art of War’.

Sun Tzu anabainisha “ufundi wa vita umejikita kwenye hadaa (deception), Unapo kuwa teyari kuvamia jifanye hauko teyari, Unapo mkaribia adui jifanye uko mbali na Unapo kuwa mbali mwaminishe upo karibu”. Katika hili Mzee Membe amafanikiwa sana, kwani swala la kuibua fununu kumhusu na nia yake ya kuutaka urais 2020. Kulimuibua Katibu Mkuu wa CCM Dr. Bashiru alie amua kumkabili vikali mwishoni mwa mwaka jana, jambo lilito muongezea umaarufu maradufu kuliko kumdhofisha. Hata hivyo haijulikani kama Membe ndie alie anzisha vuguvugu lililo pelekea kujadiliwa mitandaoni au la! . Pamoja na hayo kwa mtazamo wangumwaka jana kulikuwa bado kuna umbali kuelekea uchaguzi wa 2020 na huenda Membe alikuwa hajajipanga vya kutosha. Hapa tuna muona Membe akifanikiwa kuwahadaa adui zake wa kisiasa waamini yuko karibu wakati angali yupo mbali. Pia hata tunavyo zidi kuukaribia uchaguzi hazungumzi lolote kuhusu nia yake juu ya urasi tusijisahau kua ni mwendelezo wa kuwahadaa maadui wake waamini yuko mbali na wakati yupo karibu. Ili Mwisho awache mdomo wazi maadui zake wa kisiasa pale watakapo jisahau.

Mwandishi huyu wa maswala ya kivita anaendelea kwa kusema “ Mpige adui sehemu asiyoweza kuilinda (Kupangua) na jifiche asipo weza kukupiga”. Kwenye hili Mzee Membe amendelea kuwa very smart, anawakabili maadui vilivyo. Nani anaamini kuwa Musiba angetulia dhidi ya Membe. Kitendo cha Mzee kudhibiti Musiba Kisheria kimemziba mdomo na kumkata maini dhidi ya porojo zake. Japo kesi inaendelea lakini Musiba mkeka wake upo kwenye hatihati ya kuchanika. Pili anapo mwambia Rostam ajikite kwenye main issues (masuala makuu) ya nchi, siyo personal (watu binafsi), hizi tunaachia watu wa chini, kwa level (hadhi) yetu ni tunazungumzia masuala ya kitaifa ya uchumi. Kwanini uchumi wetu upo hapa ulipo, kwanini wafanyabiashara wadogo na wakubwa wanafunga biashara zao au zile alizozieleza kama economic distortions (upotoshaji wa kiuchumi) tunazijibu vipi." Hapa sio tu kampiga Rostam, Bali kawagusa wengi ambao watapata tabu kumjibu kwa kuwa hoja haikuelekezwa kwao moja kwa moja bali kwa Rostam. Pia kwa upande wa Rostam akimjibu Membe itaonekana kajikita kwenye personal Issues ambayo ni mambo ya watu wa chini kwa mujibu wa Membe. Sidhani kama Rostam ataingia kwenye mtego wa kutaka kuwadhibitishia watanzania kuwa yeye ni mtu wa chini alie amua kujikita kwenye personal issues badala ya main issues.Kiufupi hapa Membe amepiga pasipo panguliwa na kujificha pasipo pigika.

Samabamba na hayo Mwandishi anasisitiza katika vita ushindi upo ndani ya mambo makuu matano “Atashinda anejua wapi apigane na wapi asipigane. Atashinda ane weza kuyaongoza vyema majeshi yake yenye nguvu na dhaifu.Atashinda mwenye jeshi lenye morali kwa kada zote. Atashinda alie jianda kumkabili adui asie na maandalizi. Atashinda mwenye jeshi lenye nguvu,ambalo uhuru wake haujaingiliwa”. Katika hatua hii ni ngumu kuweza kutabili ushindi katika vita ya kisiasa inayo endelea kwa kuwa bado hatujui vema jeshi la wafwasi wa Membe na wagombea wengine wanao tarajia kutia nia hapo mwakani.

Hata hivyo kwa mtia nia alie jiandaa na ana wafahamu adui zake vema hana mashaka juu ya ushindi wake. Kwani Nguli huyu wa mikatati ya kivita bwana Sun Tzu anabainisha kwamba. “Unapo jifahamu vyema na kumfahamu adui yako hauna hofu dhidi ya mamia ya mapambano.Lakini kama unajifahamu vyeme na humfahamu adui,kila ushindi utakao pata kuna namna utaugulia maumivu ya kushindwa. Pia anaendelea kwa kusema na kama Hujijui vema wala adui yako kila pambano utakuwa kama kipofu. Hata hivyo ni Mtazamo wangu . Kila mtia nia wa tiketi ya urais 2020 awe makini kuchunguza na kuelewa uwezo wake, lakini pia atafute namna ya kuwafahamu wema adui zake. Hii itamsaidia namna bora ya kupanga mikakati yake na kujitengenezea mazingira ya ushindi katika uchaaguzi ujao. Mungu ibariki Tanzania
Huyu ndiye rais 2020
 
Sio dhambi na katiba haijakataza. Sema ni Mapokeo flani yanayo dumishwa na chama kuwa mhula wa pili Raisi alie hudumu mhula wa kwanza apite bila kupingwa ndani ya chama
Mbona alivyotoka Mwinyi hakuna Mzanzibar aliyekuwa raisi tena..
 
Mku hongera kwa uchambuzi mzuri

Back
Top Bottom