Mbinu za kivita zinavyompaisha Membe

Mbinu za kivita zinavyompaisha Membe

View attachment 1101087
Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Tanzania Bernard Membe ambaye amekuwa akitajwa kuwa na mpango wa kugombea tiketi ya urais 2020, amekuwa na mbinu za kipekee ambazo zinazidi kung’arisha Kisiasa. Jambo ambalo limenifanya nijadili mbinu za waziri huyu wa Zamani, ambae amendelea kubamba kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Baada ya kubaini mbinu na mikakati yake imekuwa ikishabiana sana na mbinu za kivita kwenye oparesheni mbalili mbali za kijeshi. Nimeona nijadili mbinu hizi kama zinavyo ainishwa na mwandishi wa maswala ya kivita bwana Sun Tzu kwenye kitabu chake maarufu cha ‘the Art of War’.

Sun Tzu anabainisha “ufundi wa vita umejikita kwenye hadaa (deception), Unapo kuwa teyari kuvamia jifanye hauko teyari, Unapo mkaribia adui jifanye uko mbali na Unapo kuwa mbali mwaminishe upo karibu”. Katika hili Mzee Membe amafanikiwa sana, kwani swala la kuibua fununu kumhusu na nia yake ya kuutaka urais 2020. Kulimuibua Katibu Mkuu wa CCM Dr. Bashiru alie amua kumkabili vikali mwishoni mwa mwaka jana, jambo lilito muongezea umaarufu maradufu kuliko kumdhofisha. Hata hivyo haijulikani kama Membe ndie alie anzisha vuguvugu lililo pelekea kujadiliwa mitandaoni au la! . Pamoja na hayo kwa mtazamo wangumwaka jana kulikuwa bado kuna umbali kuelekea uchaguzi wa 2020 na huenda Membe alikuwa hajajipanga vya kutosha. Hapa tuna muona Membe akifanikiwa kuwahadaa adui zake wa kisiasa waamini yuko karibu wakati angali yupo mbali. Pia hata tunavyo zidi kuukaribia uchaguzi hazungumzi lolote kuhusu nia yake juu ya urasi tusijisahau kua ni mwendelezo wa kuwahadaa maadui wake waamini yuko mbali na wakati yupo karibu. Ili Mwisho awache mdomo wazi maadui zake wa kisiasa pale watakapo jisahau.

Mwandishi huyu wa maswala ya kivita anaendelea kwa kusema “ Mpige adui sehemu asiyoweza kuilinda (Kupangua) na jifiche asipo weza kukupiga”. Kwenye hili Mzee Membe amendelea kuwa very smart, anawakabili maadui vilivyo. Nani anaamini kuwa Musiba angetulia dhidi ya Membe. Kitendo cha Mzee kudhibiti Musiba Kisheria kimemziba mdomo na kumkata maini dhidi ya porojo zake. Japo kesi inaendelea lakini Musiba mkeka wake upo kwenye hatihati ya kuchanika. Pili anapo mwambia Rostam ajikite kwenye main issues (masuala makuu) ya nchi, siyo personal (watu binafsi), hizi tunaachia watu wa chini, kwa level (hadhi) yetu ni tunazungumzia masuala ya kitaifa ya uchumi. Kwanini uchumi wetu upo hapa ulipo, kwanini wafanyabiashara wadogo na wakubwa wanafunga biashara zao au zile alizozieleza kama economic distortions (upotoshaji wa kiuchumi) tunazijibu vipi." Hapa sio tu kampiga Rostam, Bali kawagusa wengi ambao watapata tabu kumjibu kwa kuwa hoja haikuelekezwa kwao moja kwa moja bali kwa Rostam. Pia kwa upande wa Rostam akimjibu Membe itaonekana kajikita kwenye personal Issues ambayo ni mambo ya watu wa chini kwa mujibu wa Membe. Sidhani kama Rostam ataingia kwenye mtego wa kutaka kuwadhibitishia watanzania kuwa yeye ni mtu wa chini alie amua kujikita kwenye personal issues badala ya main issues.Kiufupi hapa Membe amepiga pasipo panguliwa na kujificha pasipo pigika.

Samabamba na hayo Mwandishi anasisitiza katika vita ushindi upo ndani ya mambo makuu matano “Atashinda anejua wapi apigane na wapi asipigane. Atashinda ane weza kuyaongoza vyema majeshi yake yenye nguvu na dhaifu.Atashinda mwenye jeshi lenye morali kwa kada zote. Atashinda alie jianda kumkabili adui asie na maandalizi. Atashinda mwenye jeshi lenye nguvu,ambalo uhuru wake haujaingiliwa”. Katika hatua hii ni ngumu kuweza kutabili ushindi katika vita ya kisiasa inayo endelea kwa kuwa bado hatujui vema jeshi la wafwasi wa Membe na wagombea wengine wanao tarajia kutia nia hapo mwakani.

Hata hivyo kwa mtia nia alie jiandaa na ana wafahamu adui zake vema hana mashaka juu ya ushindi wake. Kwani Nguli huyu wa mikatati ya kivita bwana Sun Tzu anabainisha kwamba. “Unapo jifahamu vyema na kumfahamu adui yako hauna hofu dhidi ya mamia ya mapambano.Lakini kama unajifahamu vyeme na humfahamu adui,kila ushindi utakao pata kuna namna utaugulia maumivu ya kushindwa. Pia anaendelea kwa kusema na kama Hujijui vema wala adui yako kila pambano utakuwa kama kipofu. Hata hivyo ni Mtazamo wangu . Kila mtia nia wa tiketi ya urais 2020 awe makini kuchunguza na kuelewa uwezo wake, lakini pia atafute namna ya kuwafahamu wema adui zake. Hii itamsaidia namna bora ya kupanga mikakati yake na kujitengenezea mazingira ya ushindi katika uchaaguzi ujao. Mungu ibariki Tanzania
Hongera mkuu, kwangu huu ni uzi bora wa kichambuzi kuupitia humu JF tangu mwaka uanze
 
sijaona mahusiano ya hizo mbinu za kivita na ulichokizungumzia juu ya Membe.

Membe nitamkumbuka kama aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje kipindi tulichokuwa na migogoro na nchi za Rwanda na Malawi, zaidi ya hapo sina ninachokumbuka kumhusu huyu mtu.

Ninachoona kwake ni mtu anaye endekeza siasa za makundi na anayeamini katika matabaka.

Vile vile asiyemvumilivu kisiasa kwani kipindi kile anataka kugombea alituambia wazi kuwa akifanikiwa kuwa Rais maadui Zake 11 watahama nchi.

Vile vile kesi yake na Musiba ni kiashirio kingine cha ukosefu wa uvumilivu kisiasa unless anataka kuitumia hiyo kesi kama Jukwaa la kumrejesha katika lingo za kisiasa.

ili kujua kuwa Membe sio mvumilivu kisiasa kauli ndogo tu ya Rostam imetosha kabisa kumfanya aweke hadharani mipango yake ya kugombea Urais 2020.
Kwani akigombea kuna tatizo gani!?
 
Msikilize vizuri Rostam utaelewa tatizo linakujaje ??
Ili kumdhibiti asigombee wekeni kanuni inayompa rais aliyeko madarakani mandate ya kutopingwa nje na hapo kulia lia kuwa muendelee kuenzi utamaduni mtakua mnaendekeza ujala wakati ambapo aliye madarakani pumzi imekata
 
Nakuonya tena kumtegemea mtu duni asiyefahamika na aliyepuuzwa na wananchi kama Musiba mmekwisha umia
Na Membe asitegemee kuona kiongozi mwandamizi anajibishana nae ,apambane na huyo size yake,sisi kazi yetu ni kumpatia nondo na scandal za jamaa yako,kisha anamwaga hadharani
 
Kituko,jana msiba kanya tena,ngoma inogile ,tafuta clip uje kiupya
Jana Musiba katitukana Chama cha Mapinduzi chini ya Uenyekiti wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Taifa (Mstaafu), Mzee Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
Hii ni kwa sababu hakuna anayeamini kuwa 'Wavunaji' kutoka nje wanaletwa na Waziri yeyote wa Serikali.
'Wavunaji' hao wanaokuja kwa mwamvuli wa jina la 'Wawejezaji' huletwa na Sera za Chama kilicho madarakani, CCM!
Vinginevyo itabidi tujiulize kuwa "Kampuni toka Kenya iliyokuja kwa mbwembwe kununua korosho, na ikakusanya Mawaziri kadhaa wakati wa kutiliana sahihi kwenye makubaliano", ililetwa na Waziri yupi wa Serikali ya awamu ya tano?
 
Ili kumdhibiti asigombee wekeni kanuni inayompa rais aliyeko madarakani mandate ya kutopingwa nje na hapo kulia lia kuwa muendelee kuenzi utamaduni mtakua mnaendekeza ukale wakati ambapo aliye madarakani pumzi imekata
 
Ili kumdhibiti asigombee wekeni kanuni inayompa rais aliyeko madarakani mandate ya kutopingwa nje na hapo kulia lia kuwa muendelee kuenzi utamaduni mtakua mnaendekeza ujala wakati ambapo aliye madarakani pumzi imekata
Tamaduni ni nadra sana kuandikwa ila huheshimiwa na watu wa jamii husika ndio Maana hata huko UK hawana katiba iliyoandikwa lakini mambo yanakwenda.

Ndio Maana hata yeye Membe kwa kufahamu tamaduni hiyo alikua anapambana kikwete asipingwe 2010.

Ni jambo gani hasa limepelekea yeye kukenguka na kutaka kuvunja tamaduni ambazo hapo awali alikua muumini kindaki ndaki.

Hapo ndipo linapokuja swala la umimi. Kwamba yeye ndiye anayestahili zaidi ya mwingine. Nadhani umemsikia keshasema yeye ni Raia wa daraja la juu.
 
Ahsante kwa ufafanuzi mujarabu, ni nadra sana kwako na wenzako wa Lumumba na praising team ya Magufuli kufunguka kwa hoja kama ulivyofanya leo, ahsante sana mkuu na nime appreciate your argumentation
Tamaduni ni nadra sana kuandikwa ila huheshimiwa na watu wa jamii husika ndio Maana hata huko UK hawana katiba iliyoandikwa lakini mambo yanakwenda.

Ndio Maana hata yeye Membe kwa kufahamu tamaduni hiyo alikua anapambana kikwete asipingwe 2010.

Ni jambo gani hasa limepelekea yeye kukenguka na kutaka kuvunja tamaduni ambazo hapo awali alikua muumini kindaki ndaki.

Hapo ndipo linapokuja swala la umimi. Kwamba yeye ndiye anayestahili zaidi ya mwingine. Nadhani umemsikia keshasema yeye ni Raia wa daraja la juu.
 
View attachment 1101087
Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Tanzania Bernard Membe ambaye amekuwa akitajwa kuwa na mpango wa kugombea tiketi ya urais 2020, amekuwa na mbinu za kipekee ambazo zinazidi kung’arisha Kisiasa. Jambo ambalo limenifanya nijadili mbinu za waziri huyu wa Zamani, ambae amendelea kubamba kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Baada ya kubaini mbinu na mikakati yake imekuwa ikishabiana sana na mbinu za kivita kwenye oparesheni mbalili mbali za kijeshi. Nimeona nijadili mbinu hizi kama zinavyo ainishwa na mwandishi wa maswala ya kivita bwana Sun Tzu kwenye kitabu chake maarufu cha ‘the Art of War’.

Sun Tzu anabainisha “ufundi wa vita umejikita kwenye hadaa (deception), Unapo kuwa teyari kuvamia jifanye hauko teyari, Unapo mkaribia adui jifanye uko mbali na Unapo kuwa mbali mwaminishe upo karibu”. Katika hili Mzee Membe amafanikiwa sana, kwani swala la kuibua fununu kumhusu na nia yake ya kuutaka urais 2020. Kulimuibua Katibu Mkuu wa CCM Dr. Bashiru alie amua kumkabili vikali mwishoni mwa mwaka jana, jambo lilito muongezea umaarufu maradufu kuliko kumdhofisha. Hata hivyo haijulikani kama Membe ndie alie anzisha vuguvugu lililo pelekea kujadiliwa mitandaoni au la! . Pamoja na hayo kwa mtazamo wangumwaka jana kulikuwa bado kuna umbali kuelekea uchaguzi wa 2020 na huenda Membe alikuwa hajajipanga vya kutosha. Hapa tuna muona Membe akifanikiwa kuwahadaa adui zake wa kisiasa waamini yuko karibu wakati angali yupo mbali. Pia hata tunavyo zidi kuukaribia uchaguzi hazungumzi lolote kuhusu nia yake juu ya urasi tusijisahau kua ni mwendelezo wa kuwahadaa maadui wake waamini yuko mbali na wakati yupo karibu. Ili Mwisho awache mdomo wazi maadui zake wa kisiasa pale watakapo jisahau.

Mwandishi huyu wa maswala ya kivita anaendelea kwa kusema “ Mpige adui sehemu asiyoweza kuilinda (Kupangua) na jifiche asipo weza kukupiga”. Kwenye hili Mzee Membe amendelea kuwa very smart, anawakabili maadui vilivyo. Nani anaamini kuwa Musiba angetulia dhidi ya Membe. Kitendo cha Mzee kudhibiti Musiba Kisheria kimemziba mdomo na kumkata maini dhidi ya porojo zake. Japo kesi inaendelea lakini Musiba mkeka wake upo kwenye hatihati ya kuchanika. Pili anapo mwambia Rostam ajikite kwenye main issues (masuala makuu) ya nchi, siyo personal (watu binafsi), hizi tunaachia watu wa chini, kwa level (hadhi) yetu ni tunazungumzia masuala ya kitaifa ya uchumi. Kwanini uchumi wetu upo hapa ulipo, kwanini wafanyabiashara wadogo na wakubwa wanafunga biashara zao au zile alizozieleza kama economic distortions (upotoshaji wa kiuchumi) tunazijibu vipi." Hapa sio tu kampiga Rostam, Bali kawagusa wengi ambao watapata tabu kumjibu kwa kuwa hoja haikuelekezwa kwao moja kwa moja bali kwa Rostam. Pia kwa upande wa Rostam akimjibu Membe itaonekana kajikita kwenye personal Issues ambayo ni mambo ya watu wa chini kwa mujibu wa Membe. Sidhani kama Rostam ataingia kwenye mtego wa kutaka kuwadhibitishia watanzania kuwa yeye ni mtu wa chini alie amua kujikita kwenye personal issues badala ya main issues.Kiufupi hapa Membe amepiga pasipo panguliwa na kujificha pasipo pigika.

Samabamba na hayo Mwandishi anasisitiza katika vita ushindi upo ndani ya mambo makuu matano “Atashinda anejua wapi apigane na wapi asipigane. Atashinda ane weza kuyaongoza vyema majeshi yake yenye nguvu na dhaifu.Atashinda mwenye jeshi lenye morali kwa kada zote. Atashinda alie jianda kumkabili adui asie na maandalizi. Atashinda mwenye jeshi lenye nguvu,ambalo uhuru wake haujaingiliwa”. Katika hatua hii ni ngumu kuweza kutabili ushindi katika vita ya kisiasa inayo endelea kwa kuwa bado hatujui vema jeshi la wafwasi wa Membe na wagombea wengine wanao tarajia kutia nia hapo mwakani.

Hata hivyo kwa mtia nia alie jiandaa na ana wafahamu adui zake vema hana mashaka juu ya ushindi wake. Kwani Nguli huyu wa mikatati ya kivita bwana Sun Tzu anabainisha kwamba. “Unapo jifahamu vyema na kumfahamu adui yako hauna hofu dhidi ya mamia ya mapambano.Lakini kama unajifahamu vyeme na humfahamu adui,kila ushindi utakao pata kuna namna utaugulia maumivu ya kushindwa. Pia anaendelea kwa kusema na kama Hujijui vema wala adui yako kila pambano utakuwa kama kipofu. Hata hivyo ni Mtazamo wangu . Kila mtia nia wa tiketi ya urais 2020 awe makini kuchunguza na kuelewa uwezo wake, lakini pia atafute namna ya kuwafahamu wema adui zake. Hii itamsaidia namna bora ya kupanga mikakati yake na kujitengenezea mazingira ya ushindi katika uchaaguzi ujao. Mungu ibariki Tanzania
Katiba ya nchi na ile ya ccm zimebadilishwa? Kama bado hii ni second half game hili huwa halina sub
 
sijaona mahusiano ya hizo mbinu za kivita na ulichokizungumzia juu ya Membe.

Membe nitamkumbuka kama aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje kipindi tulichokuwa na migogoro na nchi za Rwanda na Malawi, zaidi ya hapo sina ninachokumbuka kumhusu huyu mtu.

Ninachoona kwake ni mtu anaye endekeza siasa za makundi na anayeamini katika matabaka.

Vile vile asiyemvumilivu kisiasa kwani kipindi kile anataka kugombea alituambia wazi kuwa akifanikiwa kuwa Rais maadui Zake 11 watahama nchi.

Vile vile kesi yake na Musiba ni kiashirio kingine cha ukosefu wa uvumilivu kisiasa unless anataka kuitumia hiyo kesi kama Jukwaa la kumrejesha katika lingo za kisiasa.

ili kujua kuwa Membe sio mvumilivu kisiasa kauli ndogo tu ya Rostam imetosha kabisa kumfanya aweke hadharani mipango yake ya kugombea Urais 2020.

Mkuu hizo negativity ulizozungumza kuhusu Membe ni kweli kabisa, ila ni nusu tu ya tabia za jiwe, ila tu humzungumzi kuhusu hizo tabia kisa huwa unajipendekeza kwa kiongozi aliye madarakani.
 
Huyu Mzee Membe kajituliza kwake vizuuri tena yupo kimya,wala hajawahi kushiriki wala kujihusisha na maswala yoyote ya Siasa tangu awamu hii ya 5 iwe madarakani
Tatizo hawa viongozi ndio wanamchokonoa chokonoa Mzee Membe wanaona kama wamzimishe kabisa kumbe hawajifahamu kuwa ndio kwanza wanamuamsha,hata kama mtu alikuwa hana nia ya kugombea hapo ndio anaweka nia sasa kutokana na mwono wake watu wanavyomkubali,pia wanazidi kumpa umaarufu nchini,na ndio maana kila kukicha Social Medias zote Mzee Membe anazidi ku Trend[emoji1321]‍♂️
 
sijaona mahusiano ya hizo mbinu za kivita na ulichokizungumzia juu ya Membe.

Membe nitamkumbuka kama aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje kipindi tulichokuwa na migogoro na nchi za Rwanda na Malawi, zaidi ya hapo sina ninachokumbuka kumhusu huyu mtu.

Ninachoona kwake ni mtu anaye endekeza siasa za makundi na anayeamini katika matabaka.

Vile vile asiyemvumilivu kisiasa kwani kipindi kile anataka kugombea alituambia wazi kuwa akifanikiwa kuwa Rais maadui Zake 11 watahama nchi.

Vile vile kesi yake na Musiba ni kiashirio kingine cha ukosefu wa uvumilivu kisiasa unless anataka kuitumia hiyo kesi kama Jukwaa la kumrejesha katika lingo za kisiasa.

ili kujua kuwa Membe sio mvumilivu kisiasa kauli ndogo tu ya Rostam imetosha kabisa kumfanya aweke hadharani mipango yake ya kugombea Urais 2020.
Kama mahali wakati anamjibu Rostam, ametamka kuwa atagombea?
 
Nimeuoenda mtiririko wa uandishi wako. Ila kama ungetusaidia kujua kuwa Bernard Membe mgombea mtarajiwa 2020 atagombea kwa tiketi ya chama gani?
CCM wao washajitainisha wanadumisha tamaduni za 2rounds na vetting ya kwanza inafanywa na CC ambayo ukiliwa kichwa huko imetoka.

CDM labda watachukua makombo tena.
ACT nao huenda wakajaribu bahati ya kutumia rejects.
Unaposema tujadili issues, personality matters.
Yesu alikuja kuwaokoa wanadamu na dhambi zao.
Musa alikuwa na jukumu kuwatoa Israel Misri.
JKN alikuwa na jukumu kuwaondoa wakoloni Tanganyika na baadae kusini wa subsaharan Africa.

Bernard Membe ana mission gani vivid kwa ajili ya Watanzania ili wasimame nyuma yake?
Membe hajasema chochote kuhusu kuutaka urais. Kuhusu CDM au ACT kumchukuwa sidhani kwani bado wana maumivu ya Mzee Edo, wanonesha support kwa Membe ili CCM wavulugane "If your enemy is united divide him...Sun Tzu"
 
Hizi mbinu za kivita kwanini hakutumia 2015? Heading zenu zinawafanya hata wanaompenda kuanza kumpuuza!
 
Kwani dhambi akionyesha nia ya kugombea? Katiba ya CCM inakataza? Jiwe apewe changamoto hakuna namna
Sio dhambi na katiba haijakataza. Sema ni Mapokeo flani yanayo dumishwa na chama kuwa mhula wa pili Raisi alie hudumu mhula wa kwanza apite bila kupingwa ndani ya chama
 
Back
Top Bottom