Jana Musiba katitukana Chama cha Mapinduzi chini ya Uenyekiti wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Taifa (Mstaafu), Mzee Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
Hii ni kwa sababu hakuna anayeamini kuwa 'Wavunaji' kutoka nje wanaletwa na Waziri yeyote wa Serikali.
'Wavunaji' hao wanaokuja kwa mwamvuli wa jina la 'Wawejezaji' huletwa na Sera za Chama kilicho madarakani, CCM!
Vinginevyo itabidi tujiulize kuwa "Kampuni toka Kenya iliyokuja kwa mbwembwe kununua korosho, na ikakusanya Mawaziri kadhaa wakati wa kutiliana sahihi kwenye makubaliano", ililetwa na Waziri yupi wa Serikali ya awamu ya tano?