Mbinu ya mvulana kukwepa ndoa

Mbinu ya mvulana kukwepa ndoa

Nazjaz

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
7,850
Reaction score
9,423
Mdada aliyekuwa anaishi na jamaa kinyemela alimng'ang'ania jamaa kama akidai
keshapotezewa sana muda lazima jamaa amuoe. Kila ujanja jamaa aliofanya mdada kakaza
kamba lazima aolewe. Jamaa akaskuti, akapata jibu. Kaingia facebook kachagua picha za
wadada wanne akaziprint, kisha kwenye kila picha akaandika RIP, akaficha kwenye
kitabu akakiweka juu ya TV. Mdada wakati wa kupukuta vumbi akazikuta zile picha
akaziangalia akabaki na maswali. Jioni jamaa aliporudi swali la kwanza likaanza; MDADA: Samahani nimezikuta picha za wanawake kwenye kitabu ni akina nani? JAMAA: Achana na zile picha MDADA: Zinanishangaza kuna nini? JAMAA: Niwe mkweli hebu leta hizo picha, huyu wa kwanza anaitwa Jeni, nilitaka kumuoa
wiki mbili kabla ya harusi akagongwa na daladala, huyu mwingine Sara tulikutana kwenye
pati ya kazini tukapenda siku ya kupeleka posa kwao majambazi wakaingia kwao na
kuuwa watu wawili yeye akiwa moja wapo. Huyu Davidina, alikuwa ndio kwanza katoka
kusoma Ulaya shangazi yangu akanitambulisha tukapendana sana, wajomba wakapeleka
posa kwao wakakuta msiba, aliangukiwa na ukuta wa nyumba iliyokuwa inajengwa akafa, huyu wa mwisho Esther ndie aliyekuwa mpenzi wangu wa mwisho kabla ya
wewe, tulikuwa karibu tufunge ndoa baba yake akampa pesa aende Dubai, ndege yao
ikaangukia baharini mwili wake haujaonekana, nilikaa kitambo nikitafakari hii mikosi
kabla ya kuoa lakini nimeona ilikuwa bahati mbaya tu, ndio tukaonana na wewe. Na
kiukweli nimeamua lazima nipeleke posa kwenu kesho MDADA: Posa sawa hata mimi nataka ulete, lakini ungengoja kwanza kesho asubuhi
ntaenda kuwaona wazazi, unajua sijawaona muda mrefu, nikae huko kidogo halafu
ntakubonyeza lini ulete posa JAMAA: Sawa lakini usichelewe sana
 
Imekaa powa sana hiyo hadithi Mkuu.
 
Mwanangu Nazjaz una kipaji unaweza kuandika vitabu vya hadithi. Ni bahati mbaya kuwa kuna wasomaji ambao hawakuliona hili wakaishia kukandia tu bila kujua wafanyacho. Hata kama si ukweli angalau piece hii inafikirisha.
 
Vijana siku hizi wanaogopa kuoa maana gharama imekuwa kubwa mno.
 
Viwanda vya kutengeneza uongo vimekuwa vingi TZ
 
Joseph, kuoa na kuzini kipi gharama kubwa?


[TABLE="width: 677, align: left"]
[TR]
[TD]GHARAMA ZA KUOA
[/TD]
[TD]GHARAMA ZA UZINZI
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]· Kujitambulisha…….. 20,0000/=
[/TD]
[TD]· Maandalizi ya mihadi ………………….20,000/=
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]· Kishika uchumba……….50,000/=
[/TD]
[TD]· Vocha ya simu ya mrembo……………10,000/=
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]· Mahari……………………… 300,000/=
[/TD]
[TD]· Vinywaji na viburudisho……………… 75,000/=
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]· Harusi…………………..7,000,000/=
[/TD]
[TD]· Hotel/ Guest House…………………… 50,000/=
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]· Condom……………………………………… 3,000/=
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]· Hela ya taxi ya mrembo………………… 30,000/=

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]· Posho ya mrembo………………………. 20,000/=
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]· Mizinga kwa mwezi……………………300,000/=
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]· Shopping …………………………………..500,000/=
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]· HUU NI MZUNGUKO WA MWAKA MZIMA
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
buji kwa porojo sikuwezi
[TABLE="width: 677, align: left"]
[TR]
[TD]GHARAMA ZA KUOA[/TD]
[TD]GHARAMA ZA UZINZI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]· Kujitambulisha…….. 20,0000/=[/TD]
[TD]· Maandalizi ya mihadi ………………….20,000/=[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]· Kishika uchumba……….50,000/=[/TD]
[TD]· Vocha ya simu ya mrembo……………10,000/=[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]· Mahari……………………… 300,000/=[/TD]
[TD]· Vinywaji na viburudisho……………… 75,000/=[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]· Harusi…………………..7,000,000/=[/TD]
[TD]· Hotel/ Guest House…………………… 50,000/=[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD]· Condom……………………………………… 3,000/=[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD]· Hela ya taxi ya mrembo………………… 30,000/=
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD]· Posho ya mrembo………………………. 20,000/=[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD]· Mizinga kwa mwezi……………………300,000/=[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD]· Shopping …………………………………..500,000/=[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD]· HUU NI MZUNGUKO WA MWAKA MZIMA[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom