meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,349
- 4,674
MIMI NI MUUMINI MTIIFU WA SIASA ZA DR SLAA!!
MIMI NI CHADEMA ASILIA!!
Mara baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 Chadema chini ya ukatibu mkuu wa Dr Slaa iliendelea kupiga kelele nyingi moja ikiwa ni ya Dr Slaa kuibiwa kura lakini nyingine ikiwa ni kupambana na kuhitimisha utawala wa mafisadi.
Chadema pia iligundua mapema sana kuwa elimu ya kuikubali Chadema katika vijiji na mitaa haikufika sawasawa hivyo kulihitajika kazi kubwa kuwafikia wanavijiji na wanamitaa na kusimika ofisi za Chadema na mabalozi wa chadema huko 'site'
Kazi hii ilifanyika kwa ustadi mkubwa na matokeo yake tulianza kuyaona mwaka 2014 kwenye mnyukano wa uchaguzi wa serikali za mitaa.ambapo maeneo kama Arumeru mashariki kwa Nassari aliweza kuchukua vijiji zaidi ya 90 kutoka sufuri,pia Arusha mjini ambapo chadema ilizoa nusu ya mitaa yote ya jiji hilo.
Hiyo ni mifano ya kazi iliyofanywa na chadema kujijenga na kutambulika kwa wanachi ndio maana ilipokuja kwenye ubunge haikuwa kazi ngumu kwa chadema kushinda maeneo hayo.
Hata pamoja na ujio wa lowassa Chadema haikutakiwa kuacha mbinu iliyojiwekea yaani kuendelea kujenga chama kwenye msingi au kuendelea kujenga chama kama taasisi.
Badala yake chadema ilikuja na mbinu mbovu kabisa yakuwekeza kwenye mtu....mbaya zaidi mtu ambaye walimuita fisadi.
Chadema wakaikumbatia mbinu ya kuuza sura kwenye media...tukashuhidia picha za mafuriko za kutaka kuionesha CNN,BBC,ALJAZEERA n.k
Yaani chadema ikawekeza kwenye usanii wa kisiasa just to attract international media.
Kwa hili la kuvuta media za kimataifa walifanikiwa lakini aliyeneemeka ni Magufuli kwani kajikuta amepambwa katika siku yake ya kuzaliwa.
Mgombea wa Chadema alijiweka kwenye upande wa washindwa kuanzia siku ya kupiga kura pale aliposema hatakubali matokeo.
Mgombea wa chadema akakurupuka wakati matokeo yanatangazwa na kuanza kuililia tume.
Hizi ni dalili za mtu anayetumia mbinu ya kutafuta media attention.
Ushauri wangu kwa chadema turudi vijijini tuanze mchakamchaka wa kusimika mabalozi wa chadema na wanachama watiifu kwa chadema ambao mwaka 2020 wataipigia kura chadema no matter what happens hawa ndio wafuasi walionao ccm.
2020 chadema iingie na mtaji wa wanachama kadhaa kama ilivyo ccm ili kampeni ziwalenge wachache wasio na itikadi.
Chadema asilia haiwezi kuishi kwa kutegemea hisani ya mataifa ya kizungu hii ni mbinu ya watu wasiojiamini kama wanaweza kuifluence changes.
GROW UP CDM ....
Hii ni kwa hisani ya Chadema asilia.