Mbinu watumiazo Mafundi Ujenzi kuibia mabosi zao

usije mwaga ubongo wa mtu tukusome magazetini mbinu ni kusimamia tu kikamilifu, ukubali kupigwa kidogo

Hivi hakuna kampuni zilizosajiliwa rasmi kusimamia shughuli za ujenzi? Hii ni fursa nzuri sana basi tukutoaminiana
Msimamizi mwaminifu wa kazi zako, nenda kasimame mbele ya kioo cha dressing table yako na utakayemuona mbele yako ndiye mtu sahihi.

Wengine wote, sijui kampuni, ndugu, rafiki na takataka zingine ni fekelo, utapigwa hadi uchakae.
 
Ujenzi nafanya nikiwa likizo tu,kila kitu nanunua mwenyewe fundi akiniagiza cement mifuko 30 mimi nanunua mifuko 20 tu,mbao 150 mimi nanunua mbao 100 halafu naangalia kama itatosha isipotoshea ndio naagiza mingine. Nafanya hivi kwa sababu mafundi wetu wengi hawajui makadilio walishawahi kuninunulisha mabati 200 zikatumika bati 140 tu 60 zikabaki

Kabisa mkuu , fundi hawezi kuniibia kwenye material kwasababu najua hesabu kwanza.....Kabla sijajenga namtafuta mtaalam namuuliza pembeni....Spacing ya nondo ,ratio ,size ya tofali(vipimo) ,namba ya kozi,area ya jengo!

Na pia ili usiibiwe ukitaka kujenga lazima uwe site one to one ,jino kwa jino ,ukijenga kwa simu lazima upigwe tu.

Mimi fundi ndiyo namwambia tutanunua nondo kiasi kadhaa na cement kadhaa na si yeye ndiyo aniambie.

Kuhusu kuelekezwa duka hiyo ni simple tu ,unaangalia price range ya maduka hata matano then unapata evarage price ya soko.
 
usije mwaga ubongo wa mtu tukusome magazetini mbinu ni kusimamia tu kikamilifu, ukubali kupigwa kidogo

Hivi hakuna kampuni zilizosajiliwa rasmi kusimamia shughuli za ujenzi? Hii ni fursa nzuri sana basi tukutoaminiana
Hahaha.........ikitokea hivyo ni kumbana fundi arejeshe vifaa vyako alivyoiba ama kutomlipa hela yake ya mwisho ya kazi

Zipo Kampuni zinafanya kazi ya Ukandarasi wa Ujenzi, kwahiyo unaweza kuzilipa kwaajili ya kukujengea
 
Nilimaliza kupauwa...fundi nlkuwa nae bega kwa bega....sasa namsindkza stend asepe zake ile nashka begi lake nakuta n zito sana...nkafungua zipu....oh...nakuta packet za misumali ya msauzi kaniibia nilichukua huku anaona....japo tuliendelea kuwa marafik..
Hakika ww ni mtu makini mno. Ndio wanataka ivyo
 
Kupigwa ni lazima. Hizi mbinu nyingi wanatumia haswa kwa wanaofanya ujenzi kwa mara ya kwanza. Usikubali kufanya manunuzi maduka anayoshauri fundi. Lakini umakini mkubwa unahitajika kwenye manunuzi ya vifaa vya umeme. Hapa ndiyo unapigwa vibaya. Mimi nililetewa Main Switch ya laki 3 wakati dukani nimelipia Main Switch ya laki 8. Hii nilikuja kugundua baadaye sana baada y kucheki bei ya Main Switc niliyoletewa.
Wa umeme sie alikuwa mstaarabu hakutupiga kabisa ila wa pvc, gutters, plaster ......nacheka kwa huruma

Kuna duka flani la vifaa vya ujenzi kasoro tiles na umeme lipo mbezi kibanda cha mkaa wanauza vitu nusu bei hapo tu ndipo tulipoponea na ukimpeleka fundi unamuona uso umebadilika ghafla km anataka kulia kujinyea au kutukana, fikiria bajeti ya m 4 ishuke mpaka 2.3
 
Msimamizi mwaminifu wa kazi zako, nenda kasimame mbele ya kioo cha dressing table yako na utakayemuona mbele yako ndiye mtu sahihi.

Wengine wote, sijui kampuni, ndugu, rafiki na takataka zingine ni fekelo, utapigwa hadi uchakae.
Kweli aisee ina maana ukiwa na ujenzi uache kazi zote ni wewe na site tu, kuna ile huna idea ila upo tu km picha napo utapigwa tu, kiufupi bongo pagumu sana
 
Cement ya elfu 14-15 umeipata wapi mkuu? Inaweza kuwa magendo hiyo. Bei aliyokutajia fundi wako ni sahihi kwa hali ya soko ya sasa.

Kuna umuhimu pia wa kujenga uhusiano mzuri na fundi ambao ndio utakuwa msingi wa uaminifu.
Nipo tanga mkuu, hizo Bei ninazokuambia Ni za madukani na wala si za magendo.
Tunajenga vp mahusiano mazuri na fundi wakati yeye yupo kukupiga kwa makusudi
 
Hahaha.........ikitokea hivyo ni kumbana fundi arejeshe vifaa vyako alivyoiba ama kutomlipa hela yake ya mwisho ya kazi

Zipo Kampuni zinafanya kazi ya Ukandarasi wa Ujenzi, kwahiyo unaweza kuzilipa kwaajili ya kukujengea
Heri kuingia mkataba na hizo kampuni kama unakuwa bize na majukumu mengine kuliko stress za mafundi wetu hawa wa kusimamia km watoto mwishowe unajikuta ushakuwa fundi maiko wa mchongo
 
kwa wale wanaoishi kwenye nyumba huku ujenzi unaendelea usilogwe
ukajitia mwema kuwapikia ili kazi waifanye kwa wakati kuwaepushia ile adha ya kutoka kutafuta chakula kama kazi ilikuwa ya wiki itaisha baada ya mwezi😅😅🤣🙌
 
Simenti unaweka store, wakitaka mifuko kadhaa unahakikisha imechanwa na kuchanganywa yote ndio unasepa. Fundi mkuu na vibarua wake huwa wanashirikiana kuiba.
 
Back
Top Bottom