Mbinu Chafu za Udini Dhidi ya Kanisa Katoliki, Kunazidisha Umoja wa Wakristo

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
6,512
Reaction score
15,098
Tuna utawala duni na wa ajabu nyakati hizi kuliko wakati wowote. Watawala wamenyimwa hekima, ufahamu na maono, kwani wanajitengenezea kaburi lao wenyewe.

Wajinga wanaamini kuwa kulishambulia Kanisa Katoliki la Roma, kutalidhoofisha, bila ya kufahamu kuwa Wakristo wote ni Wakatoliki. Katoliki ni Kanisa la Ulimwengu. Waanglikana ni wakatoliki, waKKKT ni wakatoliki, waOrthodox ni wakatoliki, na makanisa mengine yote ya baadaye ni wakatoliki kwa sababu ndiyo asili yao, ni wakatoliki wasio chini ya mamlaka ya Roma.

Ndiyo maana wale wakatoliki wa Roma wanaitwa Roman Catholic, kwa sababu wapo wakatoliki wengi ambao siyo Roman. Ukiwagusa wasabato, waTAG, waanglikana, waKKT, waOrthodox na madhehebu yote ya Kikristo yenye msingi wa mafundisho ya Kristo, basi umewashambulia wakristo wote.

Ushetani unaofanywa na utawala wa Samia, na watu wanafiki kama Mwigulu akisaidiwa na wapuuzi kama Ludovick na wale mashekhe ubwabwa kuwashambulia wakatoliki walio chini ya Roma, wajue wanawashambulia wakatoliki wote Duniani, yaani wakristo wote bila ya kujali wakristo hao wapo chini ya mamlaka ya Roma, Kanisa la Mashariki au chini ya mamlaka za utawala zinazojitegemea.

Unayeshambulia Kanisa lolote, anaushambulia ukristo Dunia nzima.

Ushetani unaofanywa dhidi ya TEC, ambao waandaaji wanategemea utawadhoofisha wakatoliki wa chini ya mamlaka ya Roma, ni wajinga wa ajabu, wasichokijua ni kuwa wanaimarisha umoja wa Wakristo nchini na Duniani kote.

Kanisa la Kristo siyo dhehebu bali ni mafundisho ya Kristo ambaye ni mwanga, chanzo cha uhai, njia na uzima wa milele. Kristo aliye chanzo cha upendo, umoja na pekee aliye njia ya kwenda mbinguni, ndiye mwanzilishi wa Kanisa lake la Ulimwengu, ndiye mlinzi mkuu, ndiyo maana shetani na mawakala wake wote kamwe hawajawahi kuliangamiza Kanisa.

Wakristo hatutenganishwi umoja wetu eti kwa sababu hawa wanabatizwa kwa maji mengi au kidogo, wala eti kwa sababu hawa wanasali Jumapili au Jumamosi, umoja wetu umehengwa katika Kristo yetu aliye chanzo cha upendo, umoja, na njia pekee ya kumfikia Baba wa mbinguni.

Samia na Mwigulu, wajue wataangamia wao, lakini siyo Kanisa Katoliki, Kanisa baba la ukristo. Nawaonea huruma sana Samia na Mwigulu maana wanajitengenezea mwisho wao mbaya hapa Duniani na katika umilele. Waombeeni hawa watu ili waweze kuwa huru kutoka kwenye utumwa wa shetani.

Angalieni walivyowachukua vijana wajinga waislam na makada wa chama chao cha mauaji, na kuwataka wajifanywe kuwa ni wakatoliki. Wote ambao majina yao yametambulika mlaka sasa, ni waislam, wapambe wa CCM. Badala ya kuwasaidia vijana hawa kutenda mema, wanawasajili kuwa watumishi waaminifu wa shetani.
 
Walokole wao wapo bize na illusion na hallucinations za so called mbinguni
 
Wakristo na Waislamu wema wanaojitambua, Haya so called maandano ya jana, ni ushenzi mkubwa. Ni udini wa kiliangamiza taifa!

Hawa ni wa dini ileeeee! Ni wachache wao na si wote.

Tuwe na umoja, tujilinde.

Hii vita haitaishia kwa wakatoliki. Wakimaliza wakatoliki wanakuja kwa Walutheri, Anglican na makanisa yote ya yanayomkiri Kristo!

Pia na waislamu tuungane kupinga ushenzi huu.
 
Umoja wa wakristo upo kwnye maandiko tuu.
 
Mmeyatimba wenyewe kunyweni wenyewe
Mtuache waanglican sisi ni wapatanishi
 
Tunaweza kuwa na ushabiki katika mambo yote lakini si hili la udini,linapokuja hili swala tuweke tofauti zetu pembeni na kupinga vikali huu ujinga.

Ni mtu tu asiyeelewa madhara ya vita za kidini ndio anaweza kushabikia haya mambo

TUWE BRAVE ENOUGH KUEPUKA CHOKO CHOKO ZOTE ZA KIDINI
 
Kuna watu wanaondekeza udini kama makafiri?

Japo serikali inakosea kwenye baadhi ya mambo lakn makafiri ya TEC hasa haya ya mtaani achana na kina kitima, ni majinga sana
 
Kumbe mnamchukia Samia sababu ya dini yake!!!
kusema kwamba sasa mmeungana kumshambulia
 
Uzuri wa RC wameshavuka kwenye hayo mashindano ya kitoto. Wao wameua kusimama na ukweli, kwani utawaweka huru.
 
Kwakweli walutheri wametulia,wapo na nchi
 

Attachments

  • Screenshot_2025-12-26-10-22-00-353.jpg
    181.8 KB · Views: 6
Bimsumi baada ya kuchemsha kuliandama Kanisa Katoliki kupitia mashehe ubwabwa wa Bakwata sasa ameamua kumtumia Mkristo Mluteri Mwigulu Nchemba kuendesha vita hiyo akiamini kuwa itamsaidia lakini ukweli ni kuwa ndiyo inazidi kumbomoa na kuharakisha anguko lake.
 
Roma/Warumi ilikua ni Dola lililo utawala ulimwengu.
Likaporomoka kisiasa,kiutamaduni mpaka kikabaki kieneo kidogo uko ITALY.
Kimebaki pale kwasababu za ki maandiko tu kwakua mpinga kristo atatokea apo.
Ni Dola lililokua na Mabavu ya ki ulimwengu na Sasa yamebaki masalia yanayo amini Bado Yana Nguvu kuliko serikali zilizopo Duniani.
Ki Msingi Kilichobakia Roman Catholic ni kumleta mpinga kristo tu ila Imani ya Ukristo haipo Tena ndani yake baada ya Dola lenyewe kusambaratika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…