Amba Samedi
Senior Member
- Apr 5, 2024
- 193
- 326
Habari wanaJF,
Natumaini mko salama. Nina siku nyingi sijaja humu. Ila leo nimepata nafasi tena. Moto usizime. Mbele daima!
Leo tutazungumza kuhusu jinsi ya kutumia AI bila AI kukutumia wewe. AI itawasababisha wengi kuwa na uozo wa akili. Tafiti zinasema kuwa GenZ wa sasa watakuwa the most illiterate graduates ever. Sio mimi. Utafiti.
Kwa kuzingatia hili, nimeandika kanuni 6 ambazo zinaweza kubadilisha uhusiano wako na AI — hasa kama wewe ni mwanafunzi, mtaalamu, au mtu anayetaka kuendelea kuwa kiakili bila kudhurika.
Kabla ya kumwuliza AI chochote — chukua kalamu, karatasi, na akili yako. Jaribu kufikiria na kuwazua peke yako kwa dakika 15. Chora. Futa. Andika. Hapa ndipo unapojenga jitihada za kweli za akili.
Ukijua AI inavyofanya kazi, itabidi ujizuie kuitegemea kila wakati. Baada ya dakika hizo, utakuwa na maswali halisi — hayo ndiyo yaulize AI, sio maswali ya uvivu.
Wengi wetu tunatumia AI kama hivi:
Na hasa kama una vijana (sijasema watoto). Wafundishe kutafuta mbinu za kusukuma akili kufikiri, sio kuomba tu majibu ya haraka.
Tulipokuwa shuleni, wakati wa revision, tulikuwa na katabia: mwenzako alikupa kitabu, halafu akakuuliza maswali ili apime uelewa wako. Tabia hiyo ihuishwe leo, katika kizazi cha AI.
Prompt kama "Niulize maswali 10 kuhusu historia ya Tanzania halafu usahihishie majibu yangu" ni bora zaidi kuliko "Nipe mambo 10 kuhusu historia ya Tanzania."
Tofauti ni nini? Ya kwanza inakulazimu kujituma kiakili. Ya pili inakufanya usome tu na kusahau baadaye. Maswali yanaweza kuwa multiple choice au ya maelezo. Cha muhimu: jifunza, usipokee tu.
AI ni zana nzuri ya kukupelekea dhana moja kwa njia tofauti. Unaweza kuomba:
Haya, umekwama. Andika. Umejaribu kutatua. andika ulichofanya. AI imekupa jibu. Andika hilo pia. Halafu, mwisho, jaribu kudadavua mchakato mzima wa kutoka kwenye changamoto, hadi kwenye suluhisho.
Lakini usiishie hapo.
Andika jedwali dogo lenye nguzo nne:
Rejelea jedwali hili mara kwa mara kwa njia ya Spaced Repetition (yaani, lipitiepitie kwa vipindi fulani). Hutasahau, wala hutakuwa mlemavu wa AI.
Unataka kupiga hatua zaidi? tumia Feynman Method. jaribu kumfundisha mtu mwingine ulichojifunza wewe. Ukishindwa kueleza, rudi, jifunze tena. Ufundishaji ni namna ya kushika kitu kikakaa.
Hii ndiyo ngumu zaidi. Na muhimu zaidi.
AI itarahisisha mambo mengi zaidi kadri siku zinavyosonga mbele. Inakubidi uwe na mbinu za kulinda afya ya akili yako na kumbukumbu yako. Zingatia yafuatayo:
AI after effort is tutoring. AI before effort is replacement.
Mimi ni mwalimu wa AI. Ninafundisha watu jinsi ya kuboresha maisha yao kwa kutumia AI, na kujiandaa kwa mustakabali wa kazi na ajira (The Future of Work).
Endapo una maswali kuhusu jinsi ya kutumia AI katika kazi yako au masomo yako, jiunge na channel yangu ya WhatsApp. Kila wiki ninatoa maarifa mapya, mbinu za vitendo, na taarifa kuhusu AI.
👇 Bonyeza hapa kujiunga bila malipo:
🔗 Jiunge na Channel ya WhatsApp
Tukutane pale. 🚀
Natumaini mko salama. Nina siku nyingi sijaja humu. Ila leo nimepata nafasi tena. Moto usizime. Mbele daima!
Leo tutazungumza kuhusu jinsi ya kutumia AI bila AI kukutumia wewe. AI itawasababisha wengi kuwa na uozo wa akili. Tafiti zinasema kuwa GenZ wa sasa watakuwa the most illiterate graduates ever. Sio mimi. Utafiti.
Kwa kuzingatia hili, nimeandika kanuni 6 ambazo zinaweza kubadilisha uhusiano wako na AI — hasa kama wewe ni mwanafunzi, mtaalamu, au mtu anayetaka kuendelea kuwa kiakili bila kudhurika.
Kanuni #1: Tenga Walau Dakika 15 za Kufikiri Peke Yako
Kabla ya kumwuliza AI chochote — chukua kalamu, karatasi, na akili yako. Jaribu kufikiria na kuwazua peke yako kwa dakika 15. Chora. Futa. Andika. Hapa ndipo unapojenga jitihada za kweli za akili.
Ukijua AI inavyofanya kazi, itabidi ujizuie kuitegemea kila wakati. Baada ya dakika hizo, utakuwa na maswali halisi — hayo ndiyo yaulize AI, sio maswali ya uvivu.
Kanuni #2: Jifunze Kuuliza Maswali, Sio tu Kutafuta Majibu
Wengi wetu tunatumia AI kama hivi:
- "Niandikие barua pepe hii."
- "Nitatulie tatizo hili la hesabu."
- "Nidokezee jinsi ya kuanza tu — usiniambie jibu."
- "Niambie nilikosea wapi katika jaribio langu."
- "Nipe makosa 3 ya ninayoweza kutafiti na kujifunza kwayo"
Na hasa kama una vijana (sijasema watoto). Wafundishe kutafuta mbinu za kusukuma akili kufikiri, sio kuomba tu majibu ya haraka.
Kanuni #3: Mbinu ya "Niulize Maswali, Nikujibu"
Tulipokuwa shuleni, wakati wa revision, tulikuwa na katabia: mwenzako alikupa kitabu, halafu akakuuliza maswali ili apime uelewa wako. Tabia hiyo ihuishwe leo, katika kizazi cha AI.
Prompt kama "Niulize maswali 10 kuhusu historia ya Tanzania halafu usahihishie majibu yangu" ni bora zaidi kuliko "Nipe mambo 10 kuhusu historia ya Tanzania."
Tofauti ni nini? Ya kwanza inakulazimu kujituma kiakili. Ya pili inakufanya usome tu na kusahau baadaye. Maswali yanaweza kuwa multiple choice au ya maelezo. Cha muhimu: jifunza, usipokee tu.
Kanuni #4: Dhana Moja, Mitazamo Mingi
AI ni zana nzuri ya kukupelekea dhana moja kwa njia tofauti. Unaweza kuomba:
- Mchoro (Diagram)
- Mfano uliotatuliwa (Worked Example)
- Mfano rahisi kama wa mtoto (ELI5)
- Mifano inayopinga dhana (Edge Cases)
- Mfano wa kielelezo (Analogy)
Kanuni #5: Weka Kumbukumbu ya Mchakato Wako
Haya, umekwama. Andika. Umejaribu kutatua. andika ulichofanya. AI imekupa jibu. Andika hilo pia. Halafu, mwisho, jaribu kudadavua mchakato mzima wa kutoka kwenye changamoto, hadi kwenye suluhisho.
Lakini usiishie hapo.
Andika jedwali dogo lenye nguzo nne:
Rejelea jedwali hili mara kwa mara kwa njia ya Spaced Repetition (yaani, lipitiepitie kwa vipindi fulani). Hutasahau, wala hutakuwa mlemavu wa AI.
Unataka kupiga hatua zaidi? tumia Feynman Method. jaribu kumfundisha mtu mwingine ulichojifunza wewe. Ukishindwa kueleza, rudi, jifunze tena. Ufundishaji ni namna ya kushika kitu kikakaa.
Kanuni #6: Kuwa na Maisha Nje ya AI
Hii ndiyo ngumu zaidi. Na muhimu zaidi.
AI itarahisisha mambo mengi zaidi kadri siku zinavyosonga mbele. Inakubidi uwe na mbinu za kulinda afya ya akili yako na kumbukumbu yako. Zingatia yafuatayo:
- Soma kitabu cha kawaida (physical). Biblia. Biography. Quran. Chochote ambacho kinakuweza kukuweka chini kwa walau dakika 30 hadi 60. Utafiti unaonyesha kwamba watu wanaosoma vitabu vya kawaida wana uwezo bora wa kuzingatia na kukumbuka. Mitandao ya kijamii zimeharibu uwezo huu, na AI inazidi kukufanya uwe tegemezi. Kimbia mapema.
- Panga muda bila AI. Fanya hesabu kichwani bila calculator. Kariri namba 21 kwenye simu yako. Andika mawazo yako bila msaada wa AI. Utafiti kutoka Chuo Kikuu cha California unaonyesha kwamba watu wanaopunguza matumizi ya kiteknolojia wana uzalishaji wa juu zaidi na msongo mdogo wa mawazo.
- Kuboreka kuna faida yake. Kuwa na muda wa kuzima simu na kompyuta. Punga hewa safi. Weka simu janja mbali kwa siku nzima au kuwa muda fulani. Akili yako ina mfumo wa ndani (Default Mode Network) unaowaka tu unapokuwa kimya. Hii itakupa ubunifu na mawazo ya kina. AI (na teknolojia kwa ujumla) inazima mfumo huu endapo utaitumia bila kupumzika.
Hitimisho
Hizi kanuni 6 si za kupinga AI. Ni za kukutumia AI kwa akili, ili mwisho wa siku, bado uwe na ubongo wako wa uhuru, ubunifu, na nguvu za kujitegemea.AI after effort is tutoring. AI before effort is replacement.