Mbezi, Dar: Wamachinga wanarudi usiku kwa kasi

singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
5,308
6,884
Ukipita maeneo ya Mbezi Luis asubuhi unaweza kusifu sana jitihada za serikali kuboresha mazingira na makazi yetu.

Ikifika jioni hali inabadilika wamachinga wanavamia stendi yote na maeneo yote ya waenda kwa miguu na kupanga bidhaa zao.

Je,serikali inafanya kazi mchana tu, kwani kuanzia jioni hakuna watumiaji wa barabara mpaka machinga waachiwe kurudi?

Kwa kurudi huku muda si mrefu hali itarudi kama awali. Kama wamepewa maeneo wabaki huko usiku na mchana sio kurudi rudi tena barabarani.
 
Kama wamerudi lipo tatizo kwa utaratibu uliotumika kuwaondoa

Walipoondolewa walipelekwa wapi? Huko nako kulikua na wateja? Taratibu za kuwasimamia zikoje?

Kama hawajapata soko watarudi tuu, na wao wana mahitaji wana familia wanakula na wanalala
 
Sioni shida jamani waachwe,ishu sio wao tu kutafuta riziki bali pia hao ni msaada wa watu wengi wenye kipato kidogo
Manake unakuta mtu katoka kwenye husstle zake siku nzima kaishia kupata elf 2 au buku sasa akikutana na hao anaweza kupata hata dagaa mchele fungu 1 la jelo akaenda home familia ikapata ugali siku ikaisha!
Sasa mnapowaondoa hawa ni struggle kwa wengi,kama we wa kishua toka uzaliwe huwezi kuelewa hiki nilichoandika hapa ila kama nawe ushahusttle lazma utaelewa tu!
 
Kuna hawa walirudi na matoroli ya kuendesha, na hawa waliorudi bila aibu barabarani!! Hii double standards ndio inafanya waende Kuwaita wenzao, in Muhimu kuzuia kabla hawajawa wengi!! Huyu Comrade James anahusika na hili tatizo!! Either Hatoshi au anakwamsha taratibu za mama!! Fikiria Mimi binafsi Leo nimelipia leseni tzs 900,000 kiduka kidogo tuu!! Sasa iweje bado waruhusu wavamizi wa njia bila leseni!?
 
Sioni shida jamani waachwe,ishu sio wao tu kutafuta riziki bali pia hao ni msaada wa watu wengi wenye kipato kidogo
Manake unakuta mtu katoka kwenye husstle zake siku nzima kaishia kupata elf 2 au buku sasa akikutana na hao anaweza kupata hata dagaa mchele fungu 1 la jelo akaenda home familia ikapata ugali siku ikaisha!
Sasa mnapowaondoa hawa ni struggle kwa wengi,kama we wa kishua toka uzaliwe huwezi kuelewa hiki nilichoandika hapa ila kama nawe ushahusttle lazma utaelewa tu!
Utaratibu na sheria tunazojiwekea lazima zituongoze
 
Waacheni na wao wafaidi mema ya nchi tafdahali. Mara mtwambie nchi ni yetu sote, mara muwatimue. Wekeni tu utaratibu unaoeleweka. Eleweni mnadili na watu muhimu(machinga).
 
Ukipita maeneo ya Mbezi Luis asubuhi unaweza kusifu sana jitihada za serikali kuboresha mazingira na makazi yetu.
Ikifika jioni hali inabadilika wamachinga wanavamia stendi yote na maeneo yote ya waenda kwa miguu na kupanga bidhaa zao.
Je,serikali inafanya kazi mchana tu, kwani kuanzia jioni hakuna watumiaji wa barabara mpaka machinga waachiwe kurudi?
Kwa kurudi huku muda si mrefu hali itarudi kama awali. Kama wamepewa maeneo wabaki huko usiku na mchana sio kurudi rudi tena barabarani.
Maisha ni magumu sana, tubanane ivo ivo tu acha nao wapate ugali wao na familia zao,
 
Kwa mji kama Dar es salaam kuwe na utaratibu tuu wa kufunga taa usiku na camera maeneo muhimu ili Machinga wafanye kazi usiku kicha kumi na moja alfajiri wafunge ili wenye maduka nao wafungue
Kuwe na shift kati ya machinga na mfanyabiashara mkubwa na wa kati
Over
 
Ukipita maeneo ya Mbezi Luis asubuhi unaweza kusifu sana jitihada za serikali kuboresha mazingira na makazi yetu.
Ikifika jioni hali inabadilika wamachinga wanavamia stendi yote na maeneo yote ya waenda kwa miguu na kupanga bidhaa zao.
Je,serikali inafanya kazi mchana tu, kwani kuanzia jioni hakuna watumiaji wa barabara mpaka machinga waachiwe kurudi?
Kwa kurudi huku muda si mrefu hali itarudi kama awali. Kama wamepewa maeneo wabaki huko usiku na mchana sio kurudi rudi tena barabarani.
acha usnich
 
Nchi hii "wapumbavu" wengi kweli

Kwahiyo unataka serikali itumie mabomu ya machozi usiku? Unajua madhara yake?

Halafu unajua utaratibu uliotumika kuwaondoa machinga au unaandka tu? Kwa taarifa yako, Kariakoo yenyewe wamejaa, nenda wapi kwenye maeneo yao mama machinga wapo means maeneo waliyopelekwa hayafai na tafsiri yake ni utaratibu mbovu ulitumika kuwaondoa.

Halafu, sababu za kuwaondoa sidhani kama zilikuwa sahihi, au tangu waondolwe tumepata wageni wangapi ambao pengine wamekuza uchumi wetu ili tuondokane na tozo? Kama siyo, Kuna haja za kuwaondoa hawa watu?

Kuweni na huruma, maisha ni magumu, kama Serikali haiwezi kuweka mazjngira mazuri kwa Sasa kwenye biashara zao bora waachwe hadi pale watakapojipanga , watu wanafamilia , wanasomesha pia wanategemewa , mbona mna roho mbaya hivyo ,mnavyowaombea wenzetu wakose riziki? Wakati mnajua nao wanandoto za ku drive na kwenda kuvinjari Dubai au mnataka ninyi tu tuwatazame Facebook na Instagram mkipost?

Kuweni na huruma aise, MAISHA yenyewe mafupi tu bhana!!
 
Kama wamerudi lipo tatizo kwa utaratibu uliotumika kuwaondoa

Walipoondolewa walipelekwa wapi? Huko nako kulikua na wateja? Taratibu za kuwasimamia zikoje?

Kama hawajapata soko watarudi tuu, na wao wana mahitaji wana familia wanakula na wanalala

Wateja wamepata bidhaa wapi kama wauzaji wameondolewa? Si lazima wateja wangewafuata huko. Hawa wanaorudi ndio wanawaharibia wale waliopangiwa maeneo
 
Back
Top Bottom