Mbeya vs Dar es Salaam wapi kupo poa?

Mbeya vs Dar es Salaam wapi kupo poa?

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
9,001
Reaction score
11,881
Japokua naishi Dar es Salaam, binafsi nakupenda Mbeya kwasababu zifuatazo.

1. Mbeya kuna hali ya hewa nzuri ambayo hata mgeni kutoka Ulaya lazima aipende.
2. Mbeya kuna vyakula vingi vitamu na vya kila aina na vya bei ndogo.
3. Mbeya kuna mazingira mazuri ya kusomea
4. Mbeya unakunywa maji ya kisima😋😋😋😋😋😋😋😋Mbeya unafulia maji ya kisima.
5. Mbeya ukiagiza chakula hotelini maji ya kunywa unamiminiwa kutoka kwenye majagi maalumu. Na hayo maji yanachotwa kwenye ndoo tu. Kitu kimetulia cha baridiii
6. Mbeya kuna AC za asili, ukilala ukijifunika blanket unaweza sahau kwenda kazini. Usingizi mtamuuuu. Hii Christmas nataka nikale Mbeya, maeneo ya Soweto.

Japo naishi Dar ila huwa napenda sana ningeishi Mbeya. Dar kuna mbu sana mpaka kero nyieee, Dar unalala ndani ya chandarua. Dar maji ya kunywa ni shida, Dar maji ya kufulia ni shida, Dar maji ya kuoga ni shida.

Hii ndio imenipa akili ya kuanza mkakati wa kufungua kiwanda cha Kuchukua maji ya bahari ya Hindi na kuondoa chumvi, ili kupata maji safi na salama.

Lakini pia kuna vimashine nitawauzia wakazi wa Dar es salaam waliochimba visima vyenye maji ya chumvi, vitakua vinatumia solar kutoa chumvi kwenye maji ya kisima. Sasa wakazi wataweza kupata maji ya kunywa, kufulia na kuoga majumbani mwao.
 
😂😂😂 mkuu huu uzi wako ni comment yako mahali.

Hata mimi naipenda mbeya kuliko dar, ukiskia watu wanasema life begins at 40 basi jua hiyo inawahusu watu wa dar, hao ndo unaezakuta mwamba anapambana na life hadi 40's then anarudi mkoani kwao kuanza maisha 😂😂.
 
Dar mtu anatoka nyumbani kwake saa 9 alfajiri kisha anarudi saa sita usiku hana muda hata wa kukaa na watoto , ukimuuliza ni shida eti tunatafuta hela.
 
Huwezi kuacha kuipenda DAR kwa kuwa hiyo changamoto ndio fursa kwako,shusha nondo hizo na sisi iwe fursa kubadili maji chumvi kuwa fursa mahala tuishiko.
 
Wanaume/vijana wa mikoani mna shida sana. Mnafanana na nyoka ndumilakuwili..huku mnataka na kule mnataka!

Huwezi kufananisha Kijiji na Jiji
😀😀😀😀😀wewe hujawahi fika mbeya tuulize akina sisi tuliofika huko.
 
Hizo shida zoote ulizoorodhesha or kero za Dar ukiwa na hela huwezi kuziona.mana maji safi na salama kwa wenye pesa wanayapata vizuri tu.

Hayo maji ya kisima unayopenda ukiwa na pesa utakichimba na maji utayapata.hilo joto ni kwa vile pesa huna ila ukiwa nqzo Dar haina tofauti na njombe na Lushoto.

Vyakula ndio kabisaa utapata ambavyo mbeya huwezi kupata,so kifupi ni kwamba mazingira unayoishi ukiwa Dar ni duni sababu ya kipato kidogo kukuwezesha kumudu gharama za Jiji kubwa kama Dar ukilinganisha na Mbeya.

Mfano mzuri mchukue MTU anaeishi Dar ambae yuko vizuri kiuchumi mmpeleke New York City USA lazima atalia lia kama ambavyo ww unafanya hapa mana gharama za maisha zitakuwa juu ukilinganisha na Dar.

So Omba Radhi kwanza kuilinganisha Dar na Mbeya.
 
umesahau MBU😀😀😀😀😀😀
 
Mbeya my hood,Mbeya my soul Mbeya napapenda.Nipo Mbali ila napakumbuka sana green city.

Nitarudi Mbeya kuwasalimu wana pale Mabatini,Iyunga,Mama John mpaka pande za Mbalizi
 
Japo naishi Dar ila huwa napenda sana ningeishi Mbeya. Dar kuna mbu sana mpaka kero nyieee, Dar unalala ndani ya chandarua. Dar maji ya kunywa ni shida, Dar maji ya kufulia ni shida, Dar maji ya kuoga ni shida.
Sasa umetuulizia nini kama jibu unalo mwenyewe kwenu mbeya kuzuri! Nenda ukaishi huko mbeya tuache na jiji letu la daslam
 
Japokua naishi Dar es Salaam, binafsi nakupenda Mbeya kwasababu zifuatazo.

1. Mbeya kuna hali ya hewa nzuri ambayo hata mgeni kutoka Ulaya lazima aipende.
2. Mbeya kuna vyakula vingi vitamu na vya kila aina na vya bei ndogo.
3. Mbeya kuna mazingira mazuri ya kusomea
4. Mbeya unakunywa maji ya kisima😋😋😋😋😋😋😋😋Mbeya unafulia maji ya kisima.
5. Mbeya ukiagiza chakula hotelini maji ya kunywa unamiminiwa kutoka kwenye majagi maalumu. Na hayo maji yanachotwa kwenye ndoo tu. Kitu kimetulia cha baridiii
6. Mbeya kuna AC za asili, ukilala ukijifunika blanket unaweza sahau kwenda kazini. Usingizi mtamuuuu. Hii Christmas nataka nikale Mbeya, maeneo ya Soweto.

Japo naishi Dar ila huwa napenda sana ningeishi Mbeya. Dar kuna mbu sana mpaka kero nyieee, Dar unalala ndani ya chandarua. Dar maji ya kunywa ni shida, Dar maji ya kufulia ni shida, Dar maji ya kuoga ni shida.

Hii ndio imenipa akili ya kuanza mkakati wa kufungua kiwanda cha Kuchukua maji ya bahari ya Hindi na kuondoa chumvi, ili kupata maji safi na salama.

Lakini pia kuna vimashine nitawauzia wakazi wa Dar es salaam waliochimba visima vyenye maji ya chumvi, vitakua vinatumia solar kutoa chumvi kwenye maji ya kisima. Sasa wakazi wataweza kupata maji ya kunywa, kufulia na kuoga majumbani mwao.
Mkuu Dar unalinganisha na Mbeya Kwanza, huoni watu bado wanang'ang'ania kuangalia na kupigwa upepo wa maji chumvi,utawasikia nahamia mkoani mwaka huu ,akienda unamuona kesho karudi tena jijini.
 
Kwa mtumishi mwenye kipato fixed ni bora Mbeya mara nyingi kuliko Dar. Kuna wauza mitumba Dar walikuwa wanawaponda watu utasikia, "Na mshahara wako wa ualimu utaniambia nini!"
 
Back
Top Bottom