Mbeya: Serikali za mtaa yaagiza kila Mwanafunzi Tsh 15,000/= uandikishwaji darasa la kwanza

Mwanah

JF-Expert Member
May 7, 2013
353
101
Katika hali inayoonyesha kupingana sera ya Magufuli ya elimu bure darasa la kwanza mpaka kidato cha nne serikali za mitaa ya Mwanyanje,Sokoni na Chemichem kata ya Igawilo jijini Mbeya wameagiza wananchi kuandikisha watoto wanatakaoanza darasa la kwanza mwakani 2016 na waende na malipo ya shilingi 15,000/=

Hii imetolewa leo katika mkutano wa wazazi wa shule ya msingi Mwanyanje uliofanyika leo viwanja vya shule hiyo leo ijumaa na kumalizika saa saba mchana huu eti yale yalikuwa maneno tu ya jukwaani kwenye suala la elimu tuache siasa MAGUFULI TUFAFANULIE (NILIKUWEPO KWENYE MKUTANO HUO)
 
Maguful hawezi fanya kitu chochote CCM ni ile ile ndio maana wana ukawa tulikua tunalia na mabadiliko ya kimfumo sio mtu pale magogoni!!!
 
Magufuli anasema hakuna kulipa ada hivyo kwa kauli yake inamaanisha michango yote inaendelea kama kawaida, hapo ndio mnatakiwa mjue CCM ni ile ile #Hapo Kazi tu# mnaisoma namba.
 
Utambue serikali za mitaa zina mamlaka ya kutunga sheria ndogondogo zenye kukidhi mahitaji ya jamii husika.Bure kwa nyakati hizi sahau, ni hewa tu utaipata bure
 
katika hali inayoonyesha kupingana sera ya magufuli ya elimu bure darasa la kwanza mpaka kidato cha nne serikali za mitaa ya mwanyanje,sokoni na chemichem kata ya igawilo jijini mbeya wameagiza wananchi kuandikisha watoto wanatakaoanza darasa la kwanza mwakani 2016 na waende na malipo ya shilingi 15000/=

Hii imetolewa leo katika mkutano wa wazazi wa shule ya msingi Mwanyanje uliofanyika leo viwanja vya shule hiyo leo ijumaa na kumalizika saa saba mchana huu eti yale yalikuwa maneno tu ya jukwaani kwenye suala la elimu tuache siasa MAGUFULI TUFAFANULIE (NILIKUWEPO KWENYE MKUTANO HUO)

Huwa sishangai sana nchi hii kusikia serekali imetangaza kitu fulani halafu unakuta mamlaka husika haitambui amri hiyo!! Kama huamini nenda toa mzigo bandarini ama pitisha bidhaa mpakani, utaona serekali inasema bidhaa fulani hailipiwi ushuru lakini mamlaka ya mapato yaani TRA wanataka ushuru na ukihoji wanakuwa kama wanakushangaa. Na iwapo hutalipa hutapitisha ama kutoa mzigo wako. Cha ajabu hutaweza kumuona anayejali hiyo amri wakati wewe unazidi kupoteza muda wako na uharibifu wa mali yako. kwa hiyo ya malipo ya ada subiri kusikia porojo za kisiasa ndio utajua nchi hii bado sana. Utashangaa wakati wa kulipa ada ilikuwa 50,000 lakini baada ya ada kufuta michango itapelekea kufika 70,000
 
Na itachangishwa sana hiyo michango hiyo ndio tuliambiwa tutaisoma namba,ahahahahahaaaaaaaaa uzuri hiyo namba tunaisoma wote waimbaji na waimbiwaji
 
Hiyo c ada ni mchango , mchango haujakatazwa

nasema ukweli nasema ukweli kabisa sababu msema kweli ni mpenz wa mungu nikichaguliwa tu kua rais sitaki kusikia habar za michangomichango elimu ni bure mpaka form four
 
Ni muda toka imefutwa ada ya shule za msingi.Hata hvyo mamlaka za mitaa zınasimamiwa na madiwanı pamoja na mbunge wa eneo kupitia halmashauri.Mbeya jıji linaongozwa na Chadema na Sugu ndiye mbuge.Na km hyo michango imewekwa na serikali za mıtaa ambazo kimsıngi Chadema ndiye kiongozi,maana Chadema wanapıshana na kauli ya rais lakn wana haki pengne.Tuilaumu CHADEMA.
 
Katika hali inayoonyesha kupingana sera ya Magufuli ya elimu bure darasa la kwanza mpaka kidato cha nne serikali za mitaa ya Mwanyanje,Sokoni na Chemichem kata ya Igawilo jijini Mbeya wameagiza wananchi kuandikisha watoto wanatakaoanza darasa la kwanza mwakani 2016 na waende na malipo ya shilingi 15,000/=

Hii imetolewa leo katika mkutano wa wazazi wa shule ya msingi Mwanyanje uliofanyika leo viwanja vya shule hiyo leo ijumaa na kumalizika saa saba mchana huu eti yale yalikuwa maneno tu ya jukwaani kwenye suala la elimu tuache siasa MAGUFULI TUFAFANULIE (NILIKUWEPO KWENYE MKUTANO HUO)

Serikali za mitaa Mbeya zipo chini ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya ambalo linaongozwa na Chadema, sasa Chadema Mbeya watuambie kama hii ndio sera ya Chadema?au ile elimu bure walikuwa wanafanya siasa?
 
Asante kwa kupost huu uzi mapema maana wengi tulijua kuwa JPM watamnukuu visivyo kwa kushindwa kutofautisha kati ya ADA na michango na ndio maana katika kila mkutana wake wa kampeni JPM alikuwa anarudia statement ileile ili wananchi wamwelewe, namnukuu " KWANZIA MWAKANI WANAFUNZI WATASOMA BURE BILA KULIPA ADA KUANZIA DARASA LA KWANZA MPAKA KIDATO CHA NNE" mwisho wa kunukuu. Kwahiyo utaona katika hiyo statement hiyo hakuna mahali ameongelea michango kama haitakuwepo au la.
 
Kuna tofauti kati ya ada na michango ya shule lakini vyote vinafanya kazi ileile. Matumizi ya shule. Ukfuta huku unaongeza kule. Shule lazime ziende hazilali
 
Back
Top Bottom