Mbeya: Profesa Mkenda apiga marufuku Chuo cha MUST kuanzisha fani ambazo sio za Sayansi na Teknolojia

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,109
49,811
Nakuunga mkono mh.Waziri wa Elimu Prof.Mkenda.

Hatuwezi kuwa na Vyuo ambavyo havielewi maana ya Specialisation badala yake vinakimbilia kwenye fani uchwara Kwa visingizio vya kuongeza mapato na blaa blaa kama hizo.

---
PROF MKENDA ATIMBA CHUO CHA MUST MBEYA, ACHUKUZWA NA ONGEZEKO LA FANI NJE YA SAYANSI " SIMAMIENI MISINGI YA CHUO HIKI"

Waziri wa elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameutaka uongozi wa chuo kikuu Cha Sayansi na Teknolojia Mbeya MUST, kusimamia msingi wa kuanzisha chuo hicho kwa kuzalisha wataalamu katika fani ya Sayansi na ubunifu wa teknolojia mbalimbali.

Akizungumza na watumishi wa chuo hicho baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa chuoni hapo, Prof. Mkenda amesema chuo hicho kilianzishwa mahususi kwaajili ya kuinua Teknolojia Nchini hivyo ni vyema kuacha kuongeza udahili nje ya fani za Sayansi na Teknolojia.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya elimu Sayansi na Teknolojia Prof Carolyne Nombo amewaomba viongozi hao kuongeza nguvu ya ushawishi kwa wasichana kujiunga katika chuo hicho Cha Sayansi na Teknolojia, huku Makamu Mkuu wa chuo hicho Prof Aloyce Mvuma akieleza bunifu mbalimbali zilizo fanywa na chuo hicho katika kuisaidia Jamii.

Chanzo: Wasafi
 
Hii safi sana
Screenshot_20230810-085453.jpg
 
Back
Top Bottom