Mbeya: Polisi wamkamata kijana akisafirisha vipodozi vyenye sumu

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Mnamo tarehe 06.03.2022 majira ya saa 02:00 usiku, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako huko Kata ya Chimala, Tarafa ya Ilongo Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya na katika msako huo alikamatwa mtuhumiwa EMANUEL MSIGALA [42] Mkazi wa Uyole – Mbeya akiwa amepakia na kusafirisha vipodozi vyenye viambata sumu vilivyopigwa marufuku nchini aina ya Coco Pulp kopo 90 kwenye Gari yenye namba za usajili T.512 DCS aina ya Toyota Hilux Surf.

Mtuhumiwa ni mnunuzi, msafirishaji na muuzaji wa bidhaa hizo.

WITO WA KAMANDA:

Ninatoa wito kwa wananchi na wafanyabiashara kufanya biashara halali na kuacha kukwepa kulipa ushuru kwa bidhaa wanazonunua nje ya nchi vinginevyo watafilisika kwani Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limejipanga vizuri kuhakikisha ulinzi na usalama, hakuna mwanya wa kupitisha bidhaa za magendo.

Aidha ninatoa rai kwa wale wanaoendelea kuingiza na kusafirisha vipodozi vyenye viambata sumu na pombe kali zilizopigwa marufuku nchini kuacha mara moja vinginevyo mkono wa serikali hautowaacha salama.

Imetolewa na:

[ULRICH O. MATEI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
 
Back
Top Bottom