Kana-Ka-Nsungu
JF-Expert Member
- Oct 4, 2007
- 2,257
- 349
Ajali zote mbaya na zilizochukua maisha ya watu wengi mwaka huu zimetokea Mbeya.Lakini wakazi wa Mkoa huo nao kila kukicha wanaamka na balaa jipya, imani za ushirikina na watu kutaka utajiri bila kufanya kazi zinawafanya waendelee kutoana roho.
Juzi tena nimefanikiwa kukutana na mdau mmoja wa Mbeya ambaye pamoja na kunikumbushia enzi zile za watu kuchunwa ngozi na wenye vipara kukatwa vichwa pia amenipa mpya mbili ambazo zimeniacha kinywa wazi.
Inayotamba sasa hivi inaitwa "NONDO"- watu wenye imani za kishirikina, katika harakati zao za kusaka utajiri, wanatumia vipande vya nondo kuua binadamu wenzao then kipande cha nondo kilichotumika kinapelekwa kwa 'mtaalamu', kinachoendelea huko wanajua wenyewe.
Kali nyingine ni watu kuuwawa na kutolewa mioyo. Kuna imani kuwa yupo samaki mmoja mkubwa sana ambaye anaishi chini kabisa ya bahari, inasemekana samaki huyu ana madini ya thamani sana tumboni mwake, hupenda mioyo ya watu kwa chakula, ndo maana basi watu wanaitumia mioyo hiyo kama chambo cha kumuwinda samaki huyo.
Chanzo changu cha habari kilinijulisha pia kwamba waganga wengi wa kienyeji wanaowachuuza watu kufanya ukatili huu sio wa mkoani hapo bali wako kwenye nchi jirani za Malawi, Zambia na Kongo.
Je una ufahamu zaidi juu ya habari hizi? Umewahi kusikia lolote kuhusu haya?