Mbeya na mambo yao


Mbeya, pia iliitwa Moon Bay na wazungu!
 
According to Nyakyusa ancients ni kuwa ziwa hilo lilikuwa maeneo ya Mwakaleli, ikatokea watu wakipeleka mifugo kunywa maji kwenye hilo ziwa ikawa inazamishwa na kupotezwa kimaajabu ajabu, baadaye watu pia wakaanza kuzamishwa katika hilo ziwa.
Ndipo machifu walipoitana na kufanya kikao kirefu na maamuzi waliyokuja nayo ni kuwa inabidi either walifukuze au walihamishe ziwa hilo.
Baadaye wakakubaliana kulihamisha na taratibu za kijadi kuhamisha ziwa hilo zikafanyika ambapo walichukua mawe na kuyachoma moto mpaka yalipoapata moto sana na kubadirika rangi. Hapo machifu wakaanza kuchukua yale mawe na kuanza kuyarushia katika lile ziwa, kwa maajabu ya wote wakaona maji yanajikusanya na kuinuka juu na kuondoka kama wingu la mvua, maji hayo yakaenda kutua katika mlima unaouongelea na mpaka sasa yapo pale.
Simulizi zinasema kuwa ziwa lile lilikuwa 'limekasirika' kwa kuondolewa sehemu yake ya asili na kupelekwa 'ukimbizini' hivyo ikawa ukifika katika vilima na misitu ile izungukayo lile ziwa halafu ukaongea kinyakyusa unapotea.
Hapo ikabidi machifu wakae tena vikao vyao kujua kwanini wanyakyusa wanapotea kule na si wasafwa (Ieleweke kuwa eneo lile wengi ni wasafwa), ndipo wakagundua kuwa ni lille ziwa 'lililofukuzwa' kule miaka iliyopita limehamia pale na lina 'hasira' na wanyakyusa, ikabidi machifu wafanye tena utaratibu kuondoa hali ile na walifananikiwa japo mpaka sasa kuna hako kahofu ka kuongea kinyakyusa ndani ya vilima vile.

Nawasilisha
 



...wakuu naomba mnijuze, hivi jina Mbeya lina maana gani? ni nani aliupa mkoa huu jina hilo? je jina hilo limeanza kutumika mwaka gani?
 
Hapo kwenye hiyo pombe kiduchu me ndo nimewakuli wambeya, au mna matumbo ya chuma nini! Pombe inayovimbisha chupa tumboni inakuwaje?
 
...wakuu naomba mnijuze, hivi jina Mbeya lina maana gani? ni nani aliupa mkoa huu jina hilo? je jina hilo limeanza kutumika mwaka gani?
Jina Mbeya linatokana na lugha ya kisafwa ambacho kinafanana na kindali, likiwa na maana ya chumvi, yaani imbeeje. Miaka ya nyuma palikuwa na soko na chumvi iliuzwa pale. Wazungu, kama walivyotohoa majina ya maeneo mengi, wakapaita Mbeya. Mwaka gani, really, sijui. Loli nine kokukaja, gwe nakumis sana.
 
kama kindali hukijui ni bora unyamaze kimya KINDALI HAKIFANANI NA KISAFWA HATA KIDOGO. KINYAKYUSA SIO KINDALI, KISUKUMA SIO KINYAMWEZI. take that to the bank
 
Nashukuru consigliere. Unafanya mambo yako proper! We ni consigliere wa maisha!
 

Aisee historia tamu sana.....ukiwa unaangalia isidingo haya utajulia wapi?
 
Hatari sana hii mkuu!
hawa watoto hata wakifika shule wataelewa kweli???!!


mkuu angalia wingi wa maji hapo chini na aina ya daraja lilivyo

hii situation inawafundisha ujasiri.......daraja la manzese kamwe halifundishi ujasiri
 
Wasanii wakubwa wametoka Mbeya japo wamejikausha. Kama AY {Ambwene Yesaya}, GK {Gwamaka Kaighula}. Rais wa Kongo Joseph Kabila kasoma Mbeya, Wasanii kama vile Prof. Jay, Soggy Dog, Jay Moe wamesoma Mbeya pamoja na wengineo kibao. Hata wasomi wengi wenye uelewa mzuri wametoka Mbeya.
 
Thread imenikuna kweli, nimepitia post zote. Hata miye natokea Mbeya tena Kyela>kikubwa tunajazana ujinga tu hapa, ktk wilaya zilizoshindwa kutumia fursa basi kyela inaongoza, huko watu wanavuavua badala ya kuvua samaki, badala ya kulima wao wanalimalima, wakati Tukuyu wanafuga huko Kyela wanafugafuga> mboga za majani na maziwa vyote vinatoka Tukuyu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…