Mbeya na fedha za Manyoka(kuku+ulezi)

It is Sur_Plus

Senior Member
Sep 28, 2010
167
7
Habari zenu wanajamvi wa Jf. Kiukweri Mbeya ni mji ambao una wajasiliamali wengi sana. Hawa wajasiliamali ni vijana ambao wameweza kufanikiwa katika umri mdogo na kuweza kumiliki mitaji mikubwa hasa katika maeneo ya Tunduma, mbeya mjini, kyela na sehemu nyingine za mkoa huo. But kuna jambo kubwa ambalo limekua likinitatiza hasa katika ukweli wake. Kumekua na imani kwamba wafanya biashara wengi wamekua wakishukiwa kwenda Tunduma na Malawi kwa waganga kutafuta utajili unaoitwa huku "UTAJIRI WA MANYOKA". Ambapo inasemekana huko huchukuliwa ulezi au mahindi kisha humwagwa chini ili kuku ale. Inasemekana kwamba idadi ya mahindi au ulezi ambao kuku atakula ndio urefu wa maisha mtu atakayoishi mfano kukuakila punje 5 za mahindi basi utaishi katika maisha ya utajili kwa miaka 5 kisha unakufa. Habari hizi zimekua zikisikika hasa wakati wa misiba pindi wafanyabiashara wengi wanapofariki. "JE, Tuta uona ufalme wa kesho?
 
Je hao waganga wanaogawa utajiri au kuulinda wana hali gani kimaisha na uelewa wa contemporary issues za fedha na biashara?
 
kwa west africa na nchi zingine kama mnavyoona kwenye movie zao yote hayo yanatokea na sana ni mtu kuambiwa asacrifice mtu ampendaye zaidi hiyo mara nyingi watoto wazazi mke mume na huwezi danganya na hizo cult zikijisikia utoe tena unatoa mwingine umpendaye au zaidi ya mmoja pamoja na kuna masharti usipotimiza

Inasikitisha sana hii ila mtu unaomba partner wako kama anakupenda zaidi asiende, mie nahisi hapo tanzania ipo maana kuwa tajiri zaidi mara nyingi huwa wanatoa watu.

Waganga wengi wanaserve evil spirits kwa hiyo kazi yao ni kutumwa kutafuta binadamu kuwaingiza mitengoni mwao kama kwenye marine spirit etc

Ndio maana waganga na wachawi wote sawa tu wanajuana

Mungu tu ndio kiboko ya wote.
Salini
 
Ni kweli hicho kitu kipo ila waganga hao wanapatikana mbele ya eneo la Nakonde. Zambia kama KM 50 Kutokae Tunduma,Mbozi. mbona kuna nyumba nyingi zinaonekana maeneo ya Mpemba mpaka sogea hazijamalizika ukiuliza unaambiwa mmiliki alichukuwa pesa za manyoka kafa ghafla hata kabla ya muda wa masharti ni watu wachache waliobahatika kupata kuishi zaidi ya miaka mitatu tokea achukuwe hesabu yake iliotokana na idadi ya udokowaji wa Kuku aidha mahindi,Ulezi au mtama. Duniani kuna mengi maajabu inasemekana kuna kijana mmoja kutoka Mpanda yeye kaweka rekodi kwani Jogoo kadonoa punje 18 za mahindi haijawahi kutokea pia kuna ushahidi kuwa alikwisha 'jianda'kitaalam pia
 
Yaani anadonoa halafu anakinai au? kuku huyo anakuwa na njaa au ? Wadanganyika bana..lahaula lakwata.
 
Ni kweli hicho kitu kipo ila waganga hao wanapatikana mbele ya eneo la Nakonde. Zambia kama KM 50 Kutokae Tunduma,Mbozi. mbona kuna nyumba nyingi zinaonekana maeneo ya Mpemba mpaka sogea hazijamalizika ukiuliza unaambiwa mmiliki alichukuwa pesa za manyoka kafa ghafla hata kabla ya muda wa masharti ni watu wachache waliobahatika kupata kuishi zaidi ya miaka mitatu tokea achukuwe hesabu yake iliotokana na idadi ya udokowaji wa Kuku aidha mahindi,Ulezi au mtama. Duniani kuna mengi maajabu inasemekana kuna kijana mmoja kutoka Mpanda yeye kaweka rekodi kwani Jogoo kadonoa punje 18 za mahindi haijawahi kutokea pia kuna ushahidi kuwa alikwisha 'jianda'kitaalam pia

nadhan huyo atakua kabahatika
 
Mbeya nako..................unajua hata mambo km ya loliondo yaliwahi kutokea pale mbozi jirani na mlowo, alitokea bibi mmoja alikuwa anagawa maji ila ulikuwa unaruhusiwa kwenda na dumu kuwachukuliwa na wengine wasiokuwa na uwezo lakini hakuchukua muda mrefu akapotea..........................alikuja kuwa maarufu kwa jina la bibi wa kidumu
 
Hiyo hata mie nimewahi simuliwa kwamba kwa maeneo ya mbeya ipo sana na imezoeleka. Inasemekana hata unapokwenda kununua bidhaa za jumla si kila duka unaweza kununua bidhaa maduka mengine ukinunua ukienda kuuza hupati faida; faida inarudi kule uliko nunua.
 
Ndio sababu; kijana mdogo masharti kibao. miaka saba tajiri alafu wanakufa bila sababu, nitaacha kula kuku wa Mbeya yawezekana wot ni tego.Ushetani una mwisho wake..
 
kumbukeni watu wa mbeya wanapenda sana shortcuts za kupata pesa,hivyo sishangai kwa hilo.
 
NASKIA NA IRINGA NAKO...ETI NDO MAANA KUNA VICHAA WENGI..KILA UKIULIZA UNAAMBIWA HUYU ALIKUWA MAPROSOO ENZI ZAKE...MAKUBWA.:tape::tape::bored:
 
Hayo mambo kwa mbeya na Iringa ni kawaida sana. Wafanyabishara wengi mikoa hiyo hupata utajiri kwa mtindo wa kishirikina. Tatizo linakuja wengi wao hupewa masharti magumu sana kwa mfano usiwe unalala kwenye kitanda na godoro zuri, usivae nguo nzuri, usile chakula kizuri, au hakikisha unapofungua sehemu yako ya biashara e.g. duka asingie kwanza mwanamke. Kuna mfanyabiashara mmoja sehemu ya mbeya mjini karibu na lililokuwa soko la uhindini ambalo liliungua moto mwaka jana amefungua duka lakini nje kuna wateja wa kike watatu wamesimama kuuliza wanadai muuzaji amegoma tusiingie kwanza mpaka atakapoturuhusu tulipofika sisi tukaingia na wao wakaruhusiwa kuingia.Wanapata utajiri lakini wanaishi maisha fulani ya ajabu sana na utajiri wao huwa haudumu muda mrefu.:mmph:
 
Yupo dogo mmoja maeneo ya Mwanjelwa anabiashara ya kuuza vocha, betri za simu ni vimfuko. Kwa harakaharaka biashara yake yaweza kuwa na msingi Wa sh 300,000 lakini anamiliki Prado GX model ya 2002 ambazo kwa showroom za bongo zinauzwa Kati ya sh 25 mpaka 30 milioni. Utajiri Wa Mbeya na Iringa ni magumashi tu
 
kwa west africa na nchi zingine kama mnavyoona kwenye movie zao yote hayo yanatokea na sana ni mtu kuambiwa asacrifice mtu ampendaye zaidi hiyo mara nyingi watoto wazazi mke mume na huwezi danganya na hizo cult zikijisikia utoe tena unatoa mwingine umpendaye au zaidi ya mmoja pamoja na kuna masharti usipotimiza

Inasikitisha sana hii ila mtu unaomba partner wako kama anakupenda zaidi asiende, mie nahisi hapo tanzania ipo maana kuwa tajiri zaidi mara nyingi huwa wanatoa watu.

Waganga wengi wanaserve evil spirits kwa hiyo kazi yao ni kutumwa kutafuta binadamu kuwaingiza mitengoni mwao kama kwenye marine spirit etc

Ndio maana waganga na wachawi wote sawa tu wanajuana

Mungu tu ndio kiboko ya wote.
Salini

Ni kweli kabisa, nasisitiza hapo kwenye blue
 
Yupo dogo mmoja maeneo ya Mwanjelwa anabiashara ya kuuza vocha, betri za simu ni vimfuko. Kwa harakaharaka biashara yake yaweza kuwa na msingi Wa sh 300,000 lakini anamiliki Prado GX model ya 2002 ambazo kwa showroom za bongo zinauzwa Kati ya sh 25 mpaka 30 milioni. Utajiri Wa Mbeya na Iringa ni magumashi tu

wengine hizo biashara ni sehemu ya kushindia mchana, usiku wanakamata machine gun
 
Back
Top Bottom