Nahonyo
JF-Expert Member
- Dec 28, 2012
- 5,404
- 5,084
Ni kweli, ila hebu tuone huyu Shekhe ambae amefanya nje msikiti, alafu tuangalia hawa ambao wamefanya yafuatayo, na wengine wanayafanya ndani ya makanisa, alafu tujiulize je ndivyo ukristo ulivyo.Mkuu huwezi tenganisha dini na mienendo ya waumini wake.
Ndio maana Biblia inasema dini iliyo ya haki mbele za Mungu ni ile ya kuwasaidia Yatima, wajane, wasiojiweza na kuepuka udhalimu.
Dini ni matendo ya waumini.
1. Kwa wafuatilia habari tunakumbuka Kisa Cha wale mapadri waliokua wakiwalawiti watoto, makanisani.
2. a. Wengi tumeona visa vya mtu anaejiita Nabii Titto, Huku akitumia vifungu vya Bibilia vibaya, Mfano kile cha kula mfanyakazi wake, huku mkewe akitambua hilo, kupiga kilaji.
b. Titto, aliulizwa na wanahabari pale mlimani City, alipoenda kwe birthday, mama yake Diamond, kwanini amejiremba vile, kwa kupaka lipstick, kunyoa nyusi, kupaka rangi nywele, kuvaa heleni, na kuvaa nguo inayofanana Dela.
Akajibu: kwa kutumia vifungu vya Bibilia, alisema: Mwili ni hekalu, na hekalu maana yake ni nyumba,
nyumba inahitaji kupambwa, kwa kupanga rangi na mapambo mengine, Sasa kama nyumba inapambwa nae haoni kosa kupamba hekalu lake ambalo ni mwili wake.
Hebu tafakari ulete jibu, mbali na yanayoendelea ndani ya baadhi ya makanisa kuwatapeli waumini, kupitia vifungu vya Bibili.