Mbeya: Mtuhumiwa adai nyeti zake kutoweka baada ya kudharau onyo la Shekhe la kutembea na bintiye

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Mshtakiwa Faraji Ramadhani mwenye umri wa miaka 27 ameiomba Mahakama imruhusu ajidhamini mwenyewe kutokana na sehemu zake za siri kutoweka hivyo kupata maumivu makali anapokuwa Mahabusu.

"Hakimu nilikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Mtoto wa Shekhe, Ustadhi huyo alinionya sana kuachana na Binti yake lakini sikusikia ndio chanzo cha sehemu zangu za siri kupotea, nikiwa nyumbani natumia dawa za miti shamha kutuliza maumivu"

Kutokana na malalamiko hayo Hakimu Manase aliamuru mtuhumiwa huyo aliyefikishwa Mahakamani hapo kwa kosa la wizi wa Kompyuta akaguliwe na baada ya askari kumkagua ilibainika anachokisema ni kweli.

Hata hivyo Hakimu Diana Manase wa Mahakama hiyo ya Mwanzo Jijini Mbeya aligoma kumruhusu kujidhamini kwa madai akitoroka hawezi kujua wapi kwa kumpata na kumtaka avumilie kwakuwa tatizo kalitafuta mwenyewe maana shekhe alimuonya aachane na Binti yake akakaidi, Kesi imeahirishwa hadi September 27 mwaka huu.
IMG-20190924-WA0014.jpg
 
Nukuu

... avumilie kwakuwa tatizo kalitafuta mwenyewe maana shekhe alimuonya aachane na Binti yake akakaidi,...
 
Back
Top Bottom