Mbeya: Marufuku DVD na Kanda nyingine za Kukashifu Dini

Mbeya: Marufuku DVD na Kanda nyingine za Kukashifu Dini

Status
Not open for further replies.

Bubu Msemaovyo

Platinum Member
Joined
May 9, 2007
Posts
4,189
Reaction score
3,552
Hakika nimefurahi sana kwa tamko la Mkoa wa Mbeya kupiga marufuku kuonyesha kanda za video zinazo kashifu dini nyingine.

Ni hatua nzuri sana kwani chanzo cha machafuko ya kidini tumezungumzia hapa JF tatizo viongozi wanaona aibu kufuatilia eti watakuwa wameshinikizwa na JF kupiga marufuku kuonyesha kanda za kuchochea machafuko ya kidini hapa nchini. Tunashindwa kuelewa mtu unapoambiwa mgongoni umepakazwa kinyesi wewe bado unasema uko safi. Viongozi waandamizi ambao hasa tulidhani wangeshukuru sana kwa kuwakumbusha wamekaa kimya kana kwamba nchi inakwenda vizuri.

Bila shaka kufuatia Mbeya kuonyesha njia na mikoa mingine kama Dar es Salaam, Mwanza kwa yule Sheikh ambaye nadhani katumwa maana yanayofanywa na mtu huyu utadhani nchi haina RAIS. Si mikoa hiyo tu bali na mikoa mingine pigeni marufuku cinema hizo zinatupeleka kwenye vita vya KIMBARI kama RWANDA.
Mbeya wamepiga marufuku uuzaji wa CD na DVD zenye uchochezi zidi ya dini nyingine, pia wamepiga marufuku mihazara ya kukashifu dini zingine. Mimi binafsi naunga mkono hatua zilizochukuliwa huko Mbeya, watanzania wengi tunafahamu kuwa kwa sasa dini moja kukashifu dini nyingine ni jambo la kawaida, hakuna hatua zinachukuliwa, dini moja inakashifu nyingine waziwazi. CD na DVD chochezi zinauzwa waziwazi.

Kuna dini zingine bila kukashifu dini za wenzao hawawezi kuwa na ajenda katika mihadhara. Serikali ikitaka kukomesha uadui unaojengeka kati ya waislam na wakristo, izuiwe dini moja kujadili nyenzanzake. SERIKALI IGA MFANO HUKO MBEYA, KAMA UTAKI KUUBIRI IMANI INAYOKUHUSU WEWE BASI KAA NYUMBANI NA NKE WAKO

Tusipochukua hatua tutapigana wenyewe kwa wennyewe na hakuna faida itapatikana. Tuache upumbavu, tufanye kazi nchi yetu bado masikini

TAMKO LA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA MBEYA KUHUSU UCHOCHEZI WA KIDINI
​

Kwanza kabisa tungependa kutoa pongezi kwa Viongozi na Waumini wa Dini na Madhehebu mbalimbali hapo Mkoa Mbeya kuendeleza utamaduni wetu wa kuishi na kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kijamii. Bila kuweka hisia za udini. Tunawashukuru kwa kuendelea kuvumiliana. Pamoja na kuendelea katika hali hii, kumejitokeza viashiria mbalimbali vyenye kuonyesha dalili za kumomonyoka kwa maadili, katika Mkoa wetu.

2. Kumejitokeza baadhi ya viongozi wa dini ambao wamekuwa Wakuzitumia nyumba zetu takatifu za Ibada kuhubiri mambo ambayohayahusiani kabisa na mambo yanayohusu Mwenyezi Mungu na mafundisho yake, kwa kuhubiri mambo ya siasa za chuki kwa dhamira ya kupandikiza chukidhidi ya Serikali au dini na madhehebumengine. Baadhi yao wamediriki kuyasema hayo hadharani kwenye miadhara yao au mikusanyiko ya waumini wao.

Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya inaona hali hii haina afya njema kwa mustakabali wa amani na utulivu wa Mkoa wetu na Nchi kwa ujumla.

3. Pamoja na mahubiri hayo pia kumekuwepo nyaraka mbalimbali za kimaandishi za sauti katika kanda, CD zenye kuhubiri chuki, uchochezi dhidi ya dini au dhehebu lingine. Kumekuwepo na video katika kanda, CD au DVD zenye kuhubiri chuki, uchochezi, dharau na kebehi dhidi ya dini nyingine au Serikali na baadhi ya kanda hizo zimediriki kuhamasisha waumini wake vurugu na hata kuua jambo ambalo Kamti ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya inaamini hakuna dini ya aina yoyote dunianiinayohimiza waumini wote kutumia kwa jambo lolote lile.

4. Baada ya kutafakari, Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya imeamua yafuatayo:- inapiga marufuku:

(i) Kuuza, kusambaza au kuonyesha, Kanda za sauti CD za sauti, Kanda ​
za Video, CD, DVD, nyaraka na maandiko yoyte yenye uchochezi wa aina yoyote ile au kukashifu dini yeyote katika Mkoa wa Mbeya.​

(ii) Chombo chochote cha Habari kilichopo Mkoani Mbeya kiepuke kuandika makala, kunakili au kurusha hewani hotuba, mahubiri au kuonyesha video zenye kuchochea, kudharau, kuhubiri au kukashifu dini yoyote ile ​

5. Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa inawaasa viongozi wa diniMbalimbali kutohubiri siasa kwenye majumba ya Ibada kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanakiuka sheria za nchi. Mtawagawa waumini wenu kwa sababu waumini wanaelewa hayo si maagizo ya Mungu, na hayamo kwenye vitabu vitakatifu.

6. Waandishi wa Habari epukeni kushabikia matamko ya Viongozi wa Dini au Siasa yenye kulenga kuleta mgawanyiko katika taifa hili kwa Misingi ya kidini au kisiasa kwa kisingizio cha Uhuru wa Habari, kumbukeni Amani Umoja na Mshikamano wa Mkoa na Taifa
utategemea mchango wenu katika kushabikia au kukemea kauli hizobila kujali zimetolewa na kiongozi gani.

Mwisho, Serikali itamchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayekwenda kinyume na haya, bila kujali itikadi yake, dini yake au wadhifa wake. Wananchi wanaaswa kuzikabidhi nyaraka, kanda CD na DVD kwa ofisi za Serikali ngazi ya Vijiji, kata Wilaya na Mkoa au kituo chochote cha Polisi. Endapo watakabidhi kwa hiyari hawatachukuliwa hatua.

Imetolewa na:

MWENYEKITI
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA-MBEYA
 
Huwa namuaminia sana Abbasi Kandoro, ni mtu anayetumia akili sana. Alipokuwa DSM alikuwa akisolve matatizo kirahisi kabisa, tena kwa ushirikishi.

Na kwa vile kwao si mbali na Mbeya, huyu mtu anatufaa sana.
 
hawa viongoz utafikir wamefungiwa vyumbani hawaoni yanayotokea,,,kama vile hatuna rais, waziri mkuu naye yupo kwa ajili ya mshahara tu..au rais kwa vile ni muislam?
 
Mbeya wamepiga marufuku uuzaji wa CD na DVD zenye uchochezi zidi ya dini nyingine, pia wamepiga marufuku mihazara ya kukashifu dini zingine. Mimi binafsi naunga mkono hatua zilizochukuliwa huko Mbeya, watanzania wengi tunafahamu kuwa kwa sasa dini moja kukashifu dini nyingine ni jambo la kawaida, hakuna hatua zinachukuliwa, dini moja inakashifu nyingine waziwazi. CD na DVD chochezi zinauzwa waziwazi.

Kuna dini zingine bila kukashifu dini za wenzao hawawezi kuwa na ajenda katika mihadhara. Serikali ikitaka kukomesha uadui unaojengeka kati ya waislam na wakristo, izuiwe dini moja kujadili nyenzanzake. SERIKALI IGA MFANO HUKO MBEYA, KAMA UTAKI KUUBIRI IMANI INAYOKUHUSU WEWE BASI KAA NYUMBANI NA NKE WAKO

Tusipochukua hatua tutapigana wenyewe kwa wennyewe na hakuna faida itapatikana. Tuache upumbavu, tufanye kazi nchi yetu bado masikini
 
Wizara ya Habari inahusika na usambazaji wa CD na DVD za uchochezi za shehe Ilunga na Radio Imaan plus Alnuur newspaper ukihitaji mpigie ndg Dada Fene au Kaka Imma amesharudi toka zenji na studio za Ikulu production zinafanya kazi saa 24 mcheki blaza salva ana Bun CD na DVD kama zimeisha kitaa
 
Nimefurahishwa na hii ya huko Mbeya. Ila nina wasiwasi na utekelezaji wake kwani kusema sio kutenda. haikufafanuliwa itatekelezwa vipi. Nilimsikia RPC akiwataka watu kuzisalimisha DVD, CD, Cassettes, etc vinginevyo watachukuliwa hatua kali. Kwa kuwa naifahamu sana Tanzania kuwa hii itakuwa dili kwa polisi, ningeshauri kuwe na orodha ya majina ya DVD, Cd, etc ambazo zimepigwa marufuku. Bila hiyo orodha kutakuwa na mianya ya watu kuonewa na kubambikiwa kesi wasipokubali kutoa rushwa.

Hili litekelezwe kisayansi zaidi.

Pia ningependekeza itungwe sheria ya kupiga marufuku mihadhara ya kidini siku ambazo hazina umaalumu katika imani husika, kuainishwe nyakati za mihadhara (mwisho saa 12 jioni) na mahali pa kufanyika (Mbali na shule, hospitali, etc) na Kupiga marufuku matumizi ya vipaza sauti kwenye mihadhara hiyo.

Kwa namna moja au nyingine, hii ndiyo nafasi muafaka ya kupiga marufuku nyumba za starehe (baa, kumbi za harusi, etc) na maduka ya vifaa vya muziki au muziki kusumbua watu kwa sauti za juu. Walazimishwe kuweka vizuia sauti kwenye biashara zao ili wasisumbue wasiohitaji huduma yao.
 
Hakika nimefurahi sana kwa tamko la Mkoa wa Mbeya kupiga marufuku kuonyesha kanda za video zinazo kashifu dini nyingine.

Ni hatua nzuri sana kwani chanzo cha machafuko ya kidini tumezungumzia hapa JF tatizo viongozi wanaona aibu kufuatilia eti watakuwa wameshinikizwa na JF kupiga marufuku kuonyesha kanda za kuchochea machafuko ya kidini hapa nchini. Tunashindwa kuelewa mtu unapoambiwa mgongoni umepakazwa kinyesi wewe bado unasema uko safi. Viongozi waandamizi ambao hasa tulidhani wangeshukuru sana kwa kuwakumbusha wamekaa kimya kana kwamba nchi inakwenda vizuri.

Bila shaka kufuatia Mbeya kuonyesha njia na mikoa mingine kama Dar es Salaam, Mwanza kwa yule Sheikh ambaye nadhani katumwa maana yanayofanywa na mtu huyu utadhani nchi haina RAIS. Si mikoa hiyo tu bali na mikoa mingine pigeni marufuku cinema hizo zinatupeleka kwenye vita vya KIMBARI kama RWANDA.

Yap na sasa watu wote tuwe mabalozi wa kuwatambua watu wanaouza DVD hizi na wanaotoa mahubiri ya kukashifu dini za wenzao.
 
Kukashifu dini za wengine ndo kupi huko.?.
Au ukisema yesu sio mungu ndo umekashifu dini ya mtu mwingine?
 
  • Thanks
Reactions: mzm
Yaani ningependa marufuku hii ifike hadi Youtube

Inawezekana pia, given kwamba kuna kitengo cha malalamiko kule youtube ambapo kama mhusika atatoa genuine reasons, basi ile video ambayo ipo uploaded huwa inaondolewa. Hii ilishatokea pale kijana Eduardo (mchezaji wa Croatia aliyekuwa anachezea Arsenal) alipovunjwa mguu na ankle ikahama kabisa mahali pake, video yake iliondolewa baada ya wadau kuilalamikia kwamba ni too graphic!
 
Nimesikia habari hii kupitia RFA leo asubuhi, marufuku hiyo ilisema hivi, wauza kanda wote watachukulia hatua na hakuna kuonesha hiyo video/cidema popote mkoani Mbeya, nimejiuliza hivi, Kwani hizo kanda zimerekodia nje ya nchi? nani karekodi na nani aliye hata finance mradi huo si anajulikana? Mtu aliye andaa hizo kashfa pamoja na matusi hata kuelekeza wengine kuua viongozi wa dini nyingine, sura yake wala haijifichi, tena anajulikana mskiti anaoungoza/kusalia na hata mahali anapokaa panajulikana, hivi ni nini kinachozuia huyu mtu asikamatwe kwa uchochezi, kwangu mimi nadhani ni unafiki kumkamata muuza kanda while yupo aliyezizalisha, au may be Kandoro amefanya hivyo kwasababu huyu mkuu hatokei mkoani kwake? Well, labda mku wa mkoa wa Mwanza anaweza kuchukua hatua may be, shida yake nae ndio hivyo tena, ni Mjomba wa Vicky kamata!
 
Elungata ni kweli kabisa ukisema YESU siyo mungu umekashfu dini nyingine na dini yenyewe ni ukristu,kwani imani yao inasema Yesu ni mungu.Ni sawa na Mkristu akisema Mohamad siyo mtume ni kshfa kwa waislamu kwa hiyo usichoamini wewe usikiweke kuwa ni ajenda ya kumchokoza mwenzako asiyeamini kama wewe.Tuheshimiane tu kwenye imani zetu.
 
Kwani hii dini ya ukiristo imekaa kiuchiuchi? Mpaka waislamu wote wanaikashifu, huko mbeya nadhani hao viongozi wamekosa macho wanangalia kwa visigino vya miguu.

Hebu someni hapa nyinyi viongozi wa mkoa wa mbeya:

WAKRISTO WAACHE KUTULETEA POROJO ZAO ZA KANISANI,ukristo ni dini ya kusadikika isiyo ya Mungu,UKRISTO NDIO DINI INAYOENDESHWA KWA MABAVU DUNIANI KUTOKANA NA KUTOKUWA NA HOJA ZA WAZI ZA KUWAVUTIA WATU,kitabu cha Biblia kimeshindwa kuulinda Ukristo kama ilivyo Qurani tukufu,HAKUNA MTUME ALIYETOKEA BARA LA ULAYA,ajabu wazungu ndio wanaoueneza Ukristo je dini wameitoa wapi?NDIO SABABU YA KUMTUMIA MUISRAELI ILI AUSHIKILIE MJI ALIOZALIWA YESU WA JERUSALEMU,wangekwenda kuhiji wapi kama waislaamu usipokamatwa mji ule wa Waarabu wa kipalestina?HAKUNA YEYOTE HUMU ANAYEUFAHAMU UKRISTO NI KITU GANI?kila anayeufuata anafuata mkumbo tu na asiyeelewa wapi anapokwenda.UISLAAMU UNATEGEMEA HOJA,wakristo wanategemea nguvu za dola za kikafiri ili dini yao iendelee kuwepo.
 
Ndugu tumia muda wako kufanya mambo yanayokuhusu. Hakusaidii kushadadia dini ya mtu mwingine wakati dini yako wewe mwenyewe huijui. Kama yesu sio mungu wewe inakuhusu nini? au nani kakulazimisha umuamini? kama ukristo sio dini wewe kinakuwasha kitu gani? Kabla hujakosoa dini ya mtu mwingine ijue kwanza dini yako.

Hivi umewahi kusoma Al-tabari 6:111 ? kama bado ngoja nikupe kipande kidogo:

“I have fabricated things against God and have imputed to Him words which He has not spoken.”
~MUHAMMAD (Al-Tabari 6:111).

​
kama unweza kuelewa maneno hayo basi huna sababu yakuunyoshea ukristo kidole hata kidogo. Shughulika na yanayokuhusu
 
Mkuu wa mkoa wa Morogoro ndugu Joel Bendera, tunakusubiri na wewe upige marufuku kurushwa hewani redio na TV zinazokashifu dini za wengine.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom