Mbeya long time kitambo

Rungwe we acha tuu.rungwe the champion.kuna watu walikua wanajua hesabu balaa
 
Umenikumbusha mbali
 
Nakumbuka enzi zile kulikua na team daraja la tatu kama sikosei ilikua inaitwa cargo stars ilikua na cocha anaitwa Shungu, namkumbuka kuna mtu alikua anaitwa Weston jamaa alikua anapiga mashuti kama roberto carlos vile.. Enzi zile kulikua na ligi aisee
 
Nonde kulikuwa na Wababe Kama "Brother Shetani" Mwasimba huyu alikuwa na uwezo wa kumdondoshq Ng'ombe jeuri kabisa kwa mkono mmoja pale machinjio ya Nonde, walikuwepo na kina Chiba, Tonny,brother Chale, na wengine kibao, dah kina Amon Chihota!!!
 
Mzee umenikumbusha mang'ang'a, siku moja watoto wa uswazi mabatini tukapiga mguu mpaka Uzunguni. Tukaruka ukuta nyumba moja Hivi, tukapanda mti wa mang'ang'a, tukaanza uvunaji.

Lahaula, mwenye nyumba kutuona akafungulia mbwa..... Dah, tulikimbia mbio, ruka ukuta.... Kumbe mbwa kaishia getini, sisi kituo cha kwanza Azimio.
 
Karanja bus, southern cross tukuyu -Mbeya
Mgangaluma, sokolo bus, mbembela
 
Da! Umenikumbusha mbali sana mkuu. Enzi za "jesus" na "Shetani" pale juakali.
Kuna mbabe tenende mlima nyoka na kulikuwa na gari moja ina sura mbaya sana iliandikwa "kisonzo".
Enzi za kutizama sarakasi za kina wanne star na kiingilio cha shillingi 20 baada ya masomo.
Ilikuwa kama kuna mashindano ya mpira, watoto wa isanga ilikuwa tishio sana.
Mbeya....home sweet home.
That was life.
 
Na ile ya wauza mitumba ilikuwa inaitwaje mkuu?? Nawakumbuka kina shaban.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…