Mbeya: Aliyeoa Yatima Mlemavu Gumzo, Wanavyoishi Utashangaa

Mbeya: Aliyeoa Yatima Mlemavu Gumzo, Wanavyoishi Utashangaa

Inawezekana ni mapenzi tu manengelo lakini katika wanaume milioni moja kupata mmoja atakayekubali kuingia kwenye ndoa ya hivi ni nadra sana. Mwenyezi Mungu awakuzie na awape furaha na amani kwenye ndoa yao.

😂😂 mie kwa jicho la kihenga nahis huyu jamaa amemuoa kwa force za ushirikina..mbeya sio kbs..akiaminjshwa na mganga atakuwa tajiri
 
Wahuni waliliita bara letu " the dark continet" lkn huwa na maana ya watu weusi au lenye joto i.e africa. Ngono ni moja ya kitu pendwa. Pia ushirikina
Huwa ktk mazungumzo yetu huwezi kukosa hivi viwili kwa asilimia za kutosha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati nasoma hii habari hadi nilipoimaliza nilipata hamasa sana, lakini nimevunjwa moyo kwa maoni ya wachangiaji walio wengi!

Watu wamekosa ustaarabu na utu kwa kiwango cha kutisha, nimesikitika sana.

Yeyote uliyechangia kwa maneno ya kejeli ktk thread hii... imagine Salome ni ndugu yako na Mungu kamjaalia mwanaume tena kijana mzuri tu wa kumpenda pasi na kujali hali yake, ungesema sawasawa na ulichokisema hapa? Kwanini mmekuwa wanyama kiasi hiki?
Kwanini mnajisahaulisha Mungu wetu ni huyuhuyu mmoja aliyempa Salome ulemavu na sisi utimilifu?
Hiki kiburi na majivuno kinatoka wapi ilhali hakuna aliye na uhakika wa kesho yake ikoje?

Mimi nimewapenda, nimefurahi zaidi kuona wapo wanaume wenye maoni chanya juu ya ulemavu. Timotheo anaweza kuwa na elimu ndogo kuliko wanaume wengi waliochangia hapa lakini ameonesha uelewa mkubwa sana.

Mungu awasaidie kutatua tatizo lao la kipato pamoja na kudumisha upendo baina yao, kwa maana huu ndio upendo wa kweli.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom