Mbele ya watoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbele ya watoto

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by funzadume, Aug 3, 2010.

 1. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,480
  Likes Received: 2,076
  Trophy Points: 280
  Kwa wale wenzangu na mie wanandoa kuna ile hali kipindi cha uchumba na kipindi cha ndoa kabla ya kupata watoto na kuwa na wafanyakazi ndani ya nyumba kuna zile za kukumbatiana au kupigana mabusu, kulaliana kwenye makochi mkiangalia TV na vimbwanga vingine vya kimahaba vinavyofanyika nje ya chumba mfano sebuleni, jikoni na sehemu nyingine.

  Je mkipata watoto inabidi vitu vile mviache na kuvifanya chumbani tu ambako kwa kawaida hamshindi huko muda mrefu au viendelee tu mbele ya watoto?
   
 2. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Watoto wa siku hizi ukiwaacha peke yao utakuta wananyonyana ndimi, wanakumbatiana, wanafanya miujiza mikubwa usiyoitarajia.
  Sijui ni wapi wanakojifunzia hizi mambo?
  Mkifanya mbele yao si ndio mtakuwa unawaongezea mambinu na maujuzi?
   
 3. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...viendelee tu almuradi mjue wapi pa ku stop!
  Watoto uwaleavyo "kwenye mazingira ya mapenzi," ndivyo wakuavyo.
   
 4. JS

  JS JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Inabidi uache kufanya mbele za watoto. kipindi cha likizo watafutie watoto na mayaya wao likizo kwa bibi wakakae huko hata wiki mbili nyie huku mnajinafasi
   
 5. I

  Ikunda JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2010
  Joined: Jul 12, 2010
  Messages: 722
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kunatakiwa kuwe na mipaka, vinginevyo mtakuwa mnaharibu watoto
   
 6. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...No wonder wengine wakilalamikiwa "siku hizi hunijali wala hunifanyii yale ulokuwa unanifanyia zamani" wanabakia kushangaa!

  Yaani usubirie mpaka mid-term au Annual leave ndio uanze 'kuibia' kwa mkeo/mumeo?
  eti kwakuwa tu watoto hawapo?

  aaarrggh!
   
 7. T

  Tall JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  1.watoto wanatabia ya kucopy kila mzazi akifanyacho.
  2.akiwaona mnafanya mnachokifanya,usishangae akafanya hivyo hivyo iwe shuleni,kanisani,au popote pale
  3.acha kabisa kutekenyana tekenyana au kufanya jambo lolote la kimapenzi mbele ya mwanao. haifai
   
 8. malisak

  malisak JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2010
  Joined: Mar 16, 2006
  Messages: 425
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 80
  mmh mtihani utakua wa hesabu leta LOGARITHIM usipotumia four figure unaweza kukosa,
   
 9. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Kutekenyana sawa lakini kupakatana na ku busiana je............kwenda kuoga pamoja?
   
 10. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Jamani kwani ukikaa sebuleni baada ya msosi wa usiku, si watoto wana lala? mpigie sebuleni ili akome kulaumu kuwa humfanyii kama zamani!
   
 11. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,480
  Likes Received: 2,076
  Trophy Points: 280
  MBU umeongea point sana maana utakuta wanawake wanalalamika kuwa mbona siku hizi mapenzi yamepungua sio kama enzi za uchumba au wanamwambia mwenzake wanaume anakupenda ukiwa kwenu akikuweka ndani yale ya uchumba yote yanaisha hajui kuwa kuna vingine huwezi vifanya kukwepa watoto
   
 12. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,480
  Likes Received: 2,076
  Trophy Points: 280
  hapo muwe hamna housigelo au housiboi maana nao utakuta baada ya kazi anashindilia tamthilia mpk saa sita usiku na vitoto vingine havilali mpaka viangalie kina Marichuy na Juan Miguel sasa hapo mtafanya nn zaidi ya kusubiri wakati wa kulala
   
 13. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #13
  Aug 3, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,480
  Likes Received: 2,076
  Trophy Points: 280
  halafu watoto uwa wana wivu kwa mama zao utadhani wamemuoa wao mie nikijaribu kumshika mamsapu utakuta katoto kanaingilia nako kanataka kukaa na mama yake kanaona kuwa kanastahili kushikwa kenyewe tu au kuwa karibu na mama sio mtu mwingine
   
 14. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #14
  Aug 3, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  TV zetu zina haribu watoto wetu huu utandawazi umewatandaa vibaya.
  Kuna vitu ambavyo mnaweza kuviendeleza kama kuoga pamoja, kupigana mabusu ( sio denda) mkatumia glass moja kunywea kama ni wine, juice nk wakati mnaangalia TV mkakaa kochi moja kkuangalia tv unaweza hata kumwekea mwenzi wako miguu wakati wa kuangalia TV wakati mwingine hata kupika pamoja pia mnaweza pika siku mama yuko jikoni sio vibaya baba nae akawa nae jikoni wakapika pamoja
   
 15. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145

  Si wanaona kwenye Ma-TV matamthilia ya mapenzi yamejazana huko tena mida ya usiku unashangaa watoto hawaendi kulala kumbe mitamthilia ya mapenzi inasubiriwa, msipo fanya mbele yao wala haisaidii wataona huko kwenye ma-tv
   
 16. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #16
  Aug 3, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,480
  Likes Received: 2,076
  Trophy Points: 280
  hiyo ya kupika pamoja mie siwezi yaani katika vitu ambavyo sipendi duniani ni kupika kuna siku nilijaribu vitunguu vikaniingia machoni toka siku ile imepita miaka zaidi ya 15 sijaingia jikoni na nimeajiri house girl kumsaidia wife kwenye hiyo sector so siwezi kuingilia kabisa
   
 17. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,480
  Likes Received: 2,076
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo tufanye nn kimbweka tufanye mbele yao?
   
 18. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Fanya vile ambavyo si vikali sana kama kunyonyana ndimi(hii haifai) ila kukumbatiana, kukaa pamoja hivi havina noma
   
 19. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mkuu Funzadume sio lazima ukate vitunguu hata kugeuzakeuza vilivyopo jikoni ukimsaidia kukarangiza sio mbaya, HG nae anatakiwa apumzike akapunguze uzito nje jamani
   
 20. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #20
  Aug 3, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Nimewasoma wakuu loud and clear mie kukwepa masahibu yote house girl na jr lazima waingie kulala ifikapo saa 3 ispokuwa Friday na saturday
   
Loading...