Mbatia: Rais Magufuli si msafi

akina mbatia hamna asili ya uongozi nyumba za osterbay zilipitishwa kihalali
 
Kwahiyo yy alitimiza wajibu wa kitu kibaya
 
Wakina martin lutter king walipigania Uhuru wao wazungu pamoja na baadhi ya waafrica waliokuwa wananufaika waliwadharau hata Obama alipokuwa anaomba urais kwama mwafrika wakwanza alidharauliwa
 
JPM sio malaika kama tulivyo binsdamu wengine ila Kazi anayofanya nii nzuri sana. Huyo Lowassa wenu mliyetaka awe Rais ana usafi gani? Acheni kudanganya watu.
Lowassa kaingiaje kwenye uzi huu ?!.
 
Jamani ifikie mahali tukubali kuwa hakuna binadamu asiye na makosa. Hata kama suala la uuzaji nyumba by then lilikuwa tatizo lakini ni ngumu sana kuaminisha watu kuwa JPM alifisadi nchi kupitia mradi ule. Ni makosa ya serikali nzima, haukuwa uamuzi sahihi.

Hata kama hatukuabliani naye kwa baadhi ya mambo kama vile issue ya Zanzibar, bunge live, kuzuia maandamano, n.k lakini nafsi yangu inakubali kuwa bado Magufuli ni alama sahihi ya usafi na uadilifu katika kizazi cha viongozi walioko madarakani.
 
JPM sio malaika kama tulivyo binsdamu wengine ila Kazi anayofanya nii nzuri sana. Huyo Lowassa wenu mliyetaka awe Rais ana usafi gani? Acheni kudanganya watu.

Mmemtumia sana Lowassa kuficha udhaifu na ufisadi wa viongozi wengine katika chama na serikali. Kwa kuwa Lowassa mwenyewe ni mkimya mmempatia kila jina baya wakati mafisadi halisi wa mali za nchi na vyeo vyao wanalindwa.Hakuna hatua sahihi zilizochukuliwa kwa mafisadi halisi wa nchi hii.

Hatukubali tena kudanganywa kuwa Lowassa ni fisadi, ila ni shujaa mnyenyekevu anayeweza kuacha cheo na madaraka pale anapoona kuna unafiki mwingi.
 
Richmond ni ya kikwete
Lowasa hajakanusha hivyo ukikaa kimya maana yake umekubali. Kikwete aliwaambia watanzani kule mwanza tarehe 24 oktoba kuhusu Richmond Lowasa hajajibu. Kama unakubali richmond ya kikwete basi ukubali uuzaji nyumba si wa magufuli maana magufuri kicheo alikua waziri mdogo kwa sumaye. Tafuteni namna nyingine ya kumkashfu Magufuri. Kosa kubwa kina Mbatia limewakumba ni kuwa silaha zote ambazo wangezitumia kumshambulia magufuri ni batili maana makombora yameelekea kwao. Mbatia asingekua ktk muungano wa ukawa angetumia makombora ya cdm kuwapiga ccm na cdm lakini kitendo cha kuwepo kundini kupokea fataki ambaxo zingewasaidia amekosa credibility ya kumshambulia magu
 
Ungetuambia haya maneno mwaka 2008 ama mwaka jana kabla ya july wengi wetu tungekuelewa lakini kwasasa unajifurahisha na kujidanganya. Ulikaa kimya kina Mbowe walivyotuaminisha Lowasa ni fisadi. Ulimshabikia Slaa aliposema Lowasa ni fisadi lini ulipata ukweli kuwa Lowasa hakua fisadi? Kosa kubwa alulolifanya Lowasa lilikua kukubali kujitoa mhanga kutetea rafiki zake na hilo yeye mwenyewe analijutia hivyo kwangu si shujaa ninachokijua mimi alikaa kimya kwa makusudi maana alitarajia kupata nafasi kubwa ktk nchi ni ubinafsi na uchu wa madaraka aliuweka mbele kuliko maslahi ya nchi. Hili kosa hatasamehewa kamwe. Kama Lowasa angekua mzalendo alitakiwa kuitisha waandishi wa habari na kuueleza umma wa watanzania nini kilitokea kiwaziwazi na baadae ajiuzuru hapo angeonyesha kuwa yupo innocent lakini kwakua hakufanya hivyo anabaki tu kuwa moja wa lile genge la wezi na kikwete akiwemo na ndilo litamfuata huko baada ya mkutano mkuu wa kumkabidhi chief wa kisukuma mgolore wake.
 
Mbatiaaaaa, nae ni msafi kweli!!!! kweli Nyani..............
Hata mimi nimejiuliza swali hili, huyu Mbatia huyu ninayemfahamu mimi toka mwaka 47? au kuna mwingine?
Magufuli awe Mchafu awe msafi tunaipenda kazi yake, tumemkubali, na kwasababu ameazimia kuisafisha Nchi na kuleta ari ya kazi na uwajibikaji, mwachieni afanye kazi, Period.
 
Kwahiyo yy alitimiza wajibu wa kitu kibaya
Sioni kama kuna ubaya wowote ule kwani nyumba hizo wamenunua watanzania[wafanyakazi] na zingeuzwa soko huria karibu zote zingemilikiwa na waarabu/wahindi. Pia pesa zilizopatakana zimeweza kujenga na zinaendelea kujenga nyumba mpya za seerikali kutokana na mtaji huo [hebu nenda pale TBA utaona]. Mimi nionavyo ni kuwa wivu na ubinafsi ndiyo tatizo hasa wale wa kubwa ambao aidha walikuwa wanaishi kwenye nyumba zao wakati wa mchakato huo au wale ambao wangependa wanufaike bila kuwa watumishi wa umma.
 
Naomba kwanza amuulize maswala ya nyumba Sumaye....
 
Aliishazungumzwa sana, ila yuko kwenye kundi la untouchables.
p
 
kweli huyu ni mama Tanzania katika UBORA WAKE...... mtu anayetoa haya maoni ni mmoja kati ya genge la watu wanaowakumbatia lOWASSA na SUMAI...... kama JPM si Msafi!! status za hao waandamizi wawili wa CHADEMA zitakuwaje? kwani hao wote walikuwa ni MABOSS wakubwa wa JPM....
 
JPM anahusika na kashfa nyingi tu, ikiwemo Meli Chakavu, kuhamisha fedha za umma kinyume na Mamlaka ya Bunge na kukandamiza Demokrasia ya Vyama vingi na Uhuru wa kupata Habari, kinyume na Katiba aliyoapa kuilinda na kuitetea.
Hiyo meli si ndio imekabidhiwa geshi,,,,eti isizungumzwe tena?
 
Kama wastaafu hawatakiwi kuguswa na tumeshaonywa, je aliyepo online?
 
Wapinzani wamepwaya sana...mnatakiwa kupigania vitu vya msingi kama uvunjwaji wa katiba...bila ya mikutano ya wazi mnakwisha..nendeni mahakamani...
 
mbatia kapoteza moral authority baada ya kuungana na chadema kumsimamisha Lowasa waliyekua wakimtuhumu kwa ufisadi.
 
JPM anahusika na kashfa nyingi tu, ikiwemo Meli Chakavu, kuhamisha fedha za umma kinyume na Mamlaka ya Bunge na kukandamiza Demokrasia ya Vyama vingi na Uhuru wa kupata Habari, kinyume na Katiba aliyoapa kuilinda na kuitetea.
Hiyo meli imeishakabidhiwa jeshini , tafadhari vijana msiendelee kujadili .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…