Mbatia Mbona wabunge CHADEMA na CUF wamerudi bungeni kabla ya kujadili ombi la viongozi wa dini?

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Takribani siku mbili zimepita toka Mbatia alipoitisha mkutano wa waandishi wa habari makao makuu ya NCCR-Mageuzi Ilala akieleza kupokea ushauri kutoka kwa viongozi wa dini wa kurudi bungeni, lakini cha kustaajabisha kwa sasa takribani wiki moja wabunge wa CUF, CHADEMA wameonekana Dodoma kuhudhuria vikao vya kamati pamoja na wabunge wa CCM ilihali waliapa kutoshirikiana nao.

Mbatia inapaswa ujibu swali hili na sio kukaza mishipa ya shingo huku ukipokea posho kabla ya kikao;

Je imekuwaje wanahudhuria vikao vya bunge kabla ya makubaliano?

Nawasilisha
 
Akili yya kushikiliwa hiyo, ungetuwekea kauli hiyo ya kutoshirikiana ungekuwa umerejeshewa akili kidogo ya akiba.
 
Mleta post unapoandika uwe unashirikisha viungo vyako vyote maana ukawa walisema hawatashiriki shughuli yeyote inayoongozwa na naibu spika sasa hizo kamati za bunge zinaongozwa na tulia?
 
Wabunge wa CHADEMA,CUF na UKAWA kwa ujumla walichosusia ni vikao vya bunge vinavyoendeshwa na Tulia na siyo bunge la Tanzania.
 
Wewe ulitaka kila wanachofanya na kuamua waripoti kwenu, wacheni umbwiga nyie misukule,ndiyo maana mumetoswa kwenye teuzi za mtukufu kwa ujinga wenu huu.
 
Back
Top Bottom