MBATIA kufukuzwa Ubunge?

Mbona kawambwa alipotakiwa na mbatia ampe alishindwa?Magamba mnayo kazi.
 
kaka mbona unakuwa mkali, taratibu. utaandaje mitaala bila kujua ni namna gani itakuwa delivered kwa wanafunzi wako kwa kila level ili wafikie lengo lililokusudiwa? kama ni maandishi tu basi hapo ndipo kwenye tatizo. nafikiri hata Mbatia wote hamkumwelewa aliposema hatuna mitaala.
 
Sasa kama ulikuwepo kabatini ni swa na kutokuwa nao au kuna faida gani ya kuutoa sasa?? kutuonyesha Watanzania then .............. baada ya kuthibitishwa utaburishwa tena kabatini!! Mbatia yuko right kama ulikuwa hautumiki then ni sawa ni kutokuwepo!!
 

Mpinzani wa kweli hawezi kukubali kirahisi rahisi uongozi katika serikali anayoipinga. Kwa hiyo mtu wa namna hiyo hawezi kusimama kwenye maneno yake kamwe.
 
Nategemea nikasome hilo gazeti sasa hivi. Napenda kukutahadharisha kwamba sio kila kinachoandikwa gazetini au hata vitabuni ni sahihi. Waandishi wengine wamejaaliwa convincing power, hata baadhi ya wanasiasa pia.
 
MAMA POROJO kama ulimsoma vizuri mbatia alisema alikwenda hadi wizarani akaomba mitaala akaambiwa hakuna!
Kinachotokea sasa ni dhahiri serikali amefanya magumashi ili kumkomoa tuu; si oni sababu ya mbatia kujiuzulu na hakuna wa kumfukuza labda aamue mwenyewe!

Wamechukua takribani wiki nzima kumjibu, umeshindwa kujiuliza ujasiri wa mbatia ulitoka wapi?
Hapa kuna mchezo unachezwa na ukweli utajulikana!

 
Last edited by a moderator:

ndugu, usikurupuke kuongea na kufanya conclusion ya jambo usilolijua! 100% Mbatia hakukurupuka... yuko sahihi. Serikali haina MTAALA RASMI ila ina MTAALA USIO RASMI. sasa mtaala usio rasmi sio mtaala maana hautambuliki kisheria! ndio maana Serikali imeshindwa kuwasilisha mtaala Bungeni! jiulize kwa nini Serikali ishindwe kufanya jambo dogo kama hilo la kuwasilisha mtaala Bungenikama kweli mtaala huo upo! Take this...MTAALA WA ELIMU HAUPO...I repeat again..HAUPOO! Kuna professor mmoja mashuhuri alifanya utafiti na kubaini haupo na ndipo akampasia mhe. Mbatia. kwa hiyo suala la Mbatia kujiuzuru HALIPO na SAHAU!
 
Mbona kawambwa alipotakiwa na mbatia ampe alishindwa?Magamba mnayo kazi.

mim nazungumzia suala hili kwa kuwa ni sehemu ya taaluma yangu. siangalii chama katika hili. kama kwako mtu akisema mwakyembe anafanya kazi vizuri basi atakua mwanaccm, elewa kuwa uko dunia ya giza. mwakyembe aangaliwe kama mtanzania mzalendo. ukikataa mema anayoyafanya mwakyembe kwa sababu ww siyo mwana ccm, hapo utakua umeharibu. siasa isitupeleke huko. hoja yangu ni kwamba mitaala ipo kwa sababu nimewahi kuiona. pili vile tuna mihutasari, muhtasari hauwezi patikana bila mtaala kwa sababu muhtasari unatokana na mtaala. hiyo ndiyo hoja yangu. hapo siangalii ubora wa elimu au abovu wake hapa nchini. mataala ipo haipo? hilo ndiyo swali lililopo ukumbini.

acha ushabiki wa siasa za majitaka!
 

we pia kilaza
 

Walikuwa wanachanganywa na mitaala isiyo rasmi. Mara michezo ondoa, kisha michezo rudisha. Mara somo moja la sayansi, mara yarudi kama ilivyokuwa. mara kitumike kitabu hiki leo, kesho kinachotumika ni kingine.
 
Ni lazima aitende kauli yake....................hata hivyo, hakuna hasara kwa sababu hata ubunge wake amepata kwa hisani..........hakuna mtu anayemshinikiza bali ni yeye mwenyewe alijishinikiza kufanya hivyo pindi ukweli ukianikwa.............kuruhusu kuendelea kama mbunge ni kuendelea kukumbatia uongo wa wanasiasa kitu ambacho ni hatari katika ustawi wa taifa..................kujiudhuru kwake litakuwa ni fundisho kwa wanasiasa wengine kuwa waangalifu na kauli zao kabla ya kufanya tafiti mbadala. LAZIMA AJIUZURU.
 

kwanza nakupongeza kwa kufuatilia hiyo makala niliyokuwa nimeomba ucheki ili nikuonyeshe umepotosha namnukuu mkumbo '' kimsingi si rahisi kuwa na nyaraka moja na ukaiita mtaala kwa sababu mtaala ni mkusanyiko wa nyaraka nyingi'' naendelea kunukuu ''kimsingi kama waziri kawambwa angeamua kuleta nakala za mitaala ya elimu tanzania huko bungeni ukumbi wa bunge usingetosha!'' wewe unawapotosha watu kwamba kuna nyaraka zinayoitwa mitaala zipo wizarani zimetoka wapi? Tatizo la mbatia lilikuwa dogo sana kama angeelimishwa na wataalam wa mitaala. Waziri aliingizwa kingi naye akakurupuka kusema kuwa anajiandaa kuleta kitu ambacho hakipo. Nasikia jana amelepeleka hizo nyaraka zinazoitwa mtaala,nitaenda wizarani nikajionee hayo maajabu
 
scramble naona hapa una scramble kutetea kisicho weza kutetewa! Najua fika wewe ni mwalimu lakini umeshindwa kujiuliza maswali kadhaa kwenye hoja ya mabatia!

Hebu twambie kama mitaala imekuwa siri kiasi kwamba wengine wasiione?

Hivi unajua mbatia alisema amekwenda wizara kuulizia mtaala huo unaosema hupo na akaambiwa hukana?

 
Last edited by a moderator:
Wakuu,
Tunachobishania watanzania ni hiki: Mtaala UPO au HAKUNA.
Wanaosema UPO, wanarejea mtaala usio rasmi
Wanaosema HAKUNA, wanataka ulio rasmi

Wanaosema UPO wanaona kwamba mtaala sio lazima uandikwe
Wanaosema HAKUNA wanaona kwamba mtaala sharti uandikwe

Lakini je, Tanzania yetu na hali ya Elimu tuliyonayo, tuwe na mtaala ambao haujaandikwa au tuwe na ulioandikwa?
Haya changueni

 
iliyowakilishwa na serikali ni MITAALAM badala ya MITAALA.
 
unajua usemalo mkuu,kama unauwezo wandikie wizara ya elimu pengine wataamka.ni aibu kwetu sote.tunaonekana vilaza wote
 


inaelekea huelewi siasa ya vyama vingi. palikua na mvutano. ccm walitaka kumtega mbatia kwa kumtoa kwenye mstari. kawambwa alikua ameshikilia vitabu viwili vya mtaala. naibu spika alimuomba mbatia kuwa ahitimishe hoja yake kisha atapewa mtaala lkn mbatia aligoma kufanya hivyo. siasa ni mchezo mchafu. hiyo rasmi na isiyo rasmi sijui unamaanisha nini? kitu kimeandaliwa na wataalamu. wakasaini na kuwasilisha wizarani. kikahifadhiwa wizarani na pale taasisi ya elimu bado unasema siyo rasmi! au hadi aiguse mbatia ndiyo iwe rasmi?

nilifurahishwa na hoja ya mbatia. kilichomponza ni uhuni wa lissu wa kutaka wenzake wote waige ubishi wake. mbatia asijiuzulu bali awaombe watanzania radhi kwa kuwadanganya kuwa serikali haina mitaala. wattalamu wametumia mitaala hiyo kuandaa syllabus zinazo tumiwa na waalimu kote nchini kisha unasema hiyo mitaala siyo rasmi! ajabu!
 
wewe ni mwanasiasa si mtaalam,mtaalam gani? Haujui kuwa hatuna mtaala ila tuna mitaala tena ya wanasiasa
 

najua tutabishana mpaka kesho. jambo la maana subiri uone who is right and who is wrong! najua ninachoongea 100%. . from the inside job!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…