dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,502
- 3,486
James Mbatia Mwenyekiti mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James Mbatia, ametoa Sh. Milioni 200 kwa ajili ya kujenga upya Shule ya Msingi Mawala, Jimbo la Vunjo, Wilaya ya Moshi.
Akizungumza jana wakati wa kufunga mikutano ya kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji iliyofanyika katika vijiji vya Mamba-Kotela, Sembeti, Samanga, Ashira, Mshiri, Lyasongoro na Lamrakana, wilayani hapa, Mbatia alisema amelazimika kutoa fedha hizo kwa kuwa maisha ya wanafunzi zaidi ya 349 wa shule hiyo yapo hatarini.
Shule hiyo iliyopo Kata ya Kahe Magharibi, iko katika hali mbaya ya kuanguka baada ya kuta zote kuliwa na magadi.
"Wakati wenzetu, wamechota bila huruma mabilioni ya fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow iliyopo chini ya Benki Kuu (BoT) na kugawana; mimi na marafiki zangu tutaijenga upya shule ya Msingi Mawala ambayo iko hatarini kuanguka.
Natoa milioni 200 kwa kuwa hatuwezi kuwabana wananchi wajenge shule halafu wakati huo huo uwachangishe fedha za ujenzi wa maabara mashuleni, hii ni fedheha," alisema Mbatia.
Wagombea wengine waliotangaza nia ni Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri wa Chadema, John Mrema na Mtangazaji wa zamani wa Shirika la Utangazaji la Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Ukanda wa Afrika Mashariki, Peter Makyao.
Alisema haiwezekani shule hiyo ikaendelea kutishia uhai wa wanafunzi pamoja na walimu wao, wakati wapo Watanzania kama yeye wenye uwezo wa kusaidia maendeleo katika maeneo yao na kwamba tayari amekubaliana na mamlaka husika kuibomoa na kuanza kuijenga upya mwezi Januari mwaka ujao.
Mbali na ahadi hiyo, Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR- Mageuzi, mwezi uliopita, alitoa kiasi cha Sh. milioni 58 kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya elimu jimboni humo.
"Mwezi uliopita nilipita Vunjo na kukuta shule zetu zipo katikahali mbaya na nikaamua kuipatia Sekondari ya Pakula milioni 20, Kisuluni Sekondari milioni 14 za ujenzi wa maabara, Lyakirimu Sekondari milioni 11.1 za ujenzi wa nyumba za walimu lakini pia Shule ya Kumbukumbu ya Askofu Stepahano Moshi niliwapa milioni 10…Huko ndio kuwatumikia watu wako,"alisisitiza.
Katika hatua nyingine, Mbatia amewataka viongozi wa vijiji vyote vya jimbo hilo watakaochaguliwa leo kushika nyadhifa mbalimbali kuandaa mpango kazi wa miradi ya jamii ambayo itakuwa ya miaka mitano na kumkabidhi kabla ya mwezi Februari mwaka 2015 ili waweze kuanza utekelezaji wake.
Chanzo: Nipashe