Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi Prof. Mbarawa tunasubiri utekeleze ahadi yako ya kutumbua majipu TBA na TTCL. Ni ukweli usiopingika kutokana na uongozi mbovu kwenye Wakala wa Majengo (TBA) na kampuni ya simu (TTCL) taasisi hizi ni majipu.
TBA imeanzisha miradi mikubwa ya ujenzi wa nyumba za watumishi serekali na pia inasimamia nyumba za serekali. Lakini si watumishi ngazi zote wanaofaidika na nyumba hizi. Naamini ukifanyika uchunguzi katika taasisi hizi hasa TBA madudu mengi yanaweza yakaibuliwa.
Inasikitisha kuona hizi taasisi za serekali zikiendeshwa kwa hasara au faida kidogo, wakati zingeweza kuendeshwa kwa faida kubwa. Taasisi zikipata uongozi mzuri zinaweza zikaiongezea serekali mapato. Mfano wa kuigwa ni shirika la nyumba la Taifa ( NHC). Shirika hilo kabla ya kupata uongozi uliopo sasa mafanikio yake yanaonekana wazi.