Mbagala chafu sana, CCM yatumia Rapid Force (kikundi cha uhamasishaji) kuficha malalamiko ya wananchi

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,670
22,262
Jana Jumanne tarehe 21/11/2023 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam alifanya mkutano Mbagala, mkutano huo ulikuwa ni wa kulifungua soko la Mbagala Zakhiem.

Kama kawaida yao mabingwa wa kuficha ukweli huwa wanaambatana na kikundi cha vijana wapatao 30 hivi, hawa vijana wanaokusanywa sehemu mbalimbali za jiji kazi yao ni kuunga mkono lisemwalo na kiongozi na kushangilia hotuba na hulipwa kwa kazi hiyo, bahati nzuri malipo haya hutangazwa rasmi.

Kwenye mkutano huo alikuwepo mbunge Chaurembo ambaye si kawaida kuonekana Mbagala kwenye shughuri zozote zile, mbunge huyo alichukua muda kujisifu kwa kuiendeleza Mbagala japo wananchi wengi hawamfahamu, na muda wote kikundi cha uhamasishaji kilikuwa kikipiga kelele za kumtukuza na kuwafanya wananchi washindwe kuyapinga maelezo ya mbunge huyo.

Nachikua nafasi hii kumjulisha Mkuu wa Mkoa kuwa atumie muda wake kulitembelea eneo la Biasi ambalo liko nyuma ya Rangitatu huko atashangaa mwenyewe kwa kile atakachokiona, kwani ni kuchafu sana licha ya kuwa ni eneo linaloliingizia nchi pesa za kigeni kila sekunde inayopita, huko kuna badari kavu inayohudumia magari ya mizigo toka Rwanda na Burundi na magodauni ya mbolea, mazao na viwanda vya chuma na bidhaa nyingine.
 
Back
Top Bottom