Marehemu Idi Amin Dada aliiongoza Uganda kwa miaka minane kati ya mwaka wa 1971 hadi 1979
Mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu ujao nchini Uganda ameahidi kurejesha nyumbani mabaki ya aliyekuwa rais wa nchini hiyo Idi Amin Dada na kuujengea makavazi.
Aliyekuwa waziri mkuu wa Uganda Amama Mbabazi,alisema endapo atachaguliwa kuwa rais azimio lake la kwanza itakuwa kuwapatanisha waganda wa kila tabaka na kabila.
Kwa madhumuni hayo anapanga kuwaleta pamoja watu anaohisi kuwa wanaomuunga mkono Idi Amin wale waliomuunga mkono Milton Obote na wale wanaomuunga mkono rasi wa sasa Yoweri Kaguta Museveni.
Viongozi hao watatu ndio waliochangia kwa njia moja au nyengine mwelekeo wa kisiasa wa Uganda.
Image caption Amama Mbabazi ameahidi kurejesha nyumbani mabaki ya aliyekuwa rais wa nchini hiyo Idi Amin Dada na kuujengea makavazi.
Marehemu Idi Amin Dada aliiongoza Uganda kwa miaka minane kati ya mwaka wa 1971 hadi 1979 utawala ambao ulishuhudia mauaji ya wapinzani wake wengi.
Vilevile anatuhumiwa kwa kuwatimua wahindi wote nchini Uganda kabla ya kupinduliwa na Milton Obote.
Marehemu Idi Amin aliaga dunia akiwa uhamishoni nchini Saudi Arabia.
Rais Yoweri Museveni, anatarajiwa kuchaguliwa tena kuongoza taifa hilo la Afrika Mashariki kwa hatamu ya tano.
Chanzo: BBC