Mbaazi ni kilio mwaka huu

PACHOTO

JF-Expert Member
Dec 30, 2011
1,321
970
Habari wakuu!

Kama ilivyo kwa zao la CHOROKO, zao la MBAAZI nalo limeleta kilio kwa wakulima wa mkoa wa Mtwara kwani hadi leo hii linanunuliwa Tsh 300/= kwa kilo moja ukizingatia gharama ya uzalishaji ni kubwa sana ukilinganisha na bei ya kuuzia. kilio hiki kilianza kwenye choroko, kimefuata cha mbaazi sijui kwenye korosho itakuwaje, ki ukweli inakatisha tamaa sana!

DIaeZsYUQAAKteS.jpg
 
Halafu anatokea mpumbavu mmoja anawadanganya watu wa kusini kuwa kaleta bei kubwa ya korosho.

Kwanini mazao mengine kama mbaazi,vitunguu na nyanya asilete hiyo bei kubwa?

Bei kubwa ya korosho ililetwa na wanunuzi wenyewe kulingana na uhitaji mkubwa wa korosho duniani huku nchi kama Vietnam na India hali ya hewa kuchange na kupekea mwaka juzi nchi hizo zivune kidogo.

Kwa waliopitia masomo ya uchumi wanajua kanuni hii; Bidhaa kadri zinavyoadimika, ndivyo thamani inavyoongezeka.
Kwaujumla kilimo hapa Bongo ni majanga.
 
Hata huku Manyara ni majanga
habari wakuu!
kama ilivyo kwa zao la CHOROKO, zao la MBAAZI nalo limeleta kilio kwa wakulima wa mkoa wa Mtwara kwani hadi leo hii linanunuliwa Tsh 300/= kwa kilo moja ukizingatia gharama ya uzalishaji ni kubwa sana ukilinganisha na bei ya kuuzia. kilio hiki kilianza kwenye choroko, kimefuata cha mbaazi sijui kwenye korosho itakuwaje..........ki ukweli inakatisha tamaa sana![/QUOT
 
Tumeambiwa wakulima wamepata fedha sana mpaka kufikia hatua ya kuwanunulia mbuzi soda.
 
Hivi tulime nini maanake hakuna chenye afadhali, karibu kila mahali bila bila
 
Juzi nimeambiwa pale masasi kilo moja ya mbaazi ni tsh 600/=
Kweli nwaka huu majanga kwa ndugu zangu
 
Tatizo bei za bidhaa huzi zinapangwa na Mhindi ambaye naye anategemea soko la Dunia. Kwa kuwa mazao hayaozi, yahifadhini ghalani hadi hali itapokuwa njema.
 
Korosho Bong la Makinikia mkuu mwaka huu unaachia kwa 6000 for 1kg. But nanunua mbaazi kilo sh 400, kwa anaridhia ni-PM
 
Korosho Bong la Makinikia mkuu mwaka huu unaachia kwa 6000 for 1kg...But nanunua mbaazi kilo sh 400, kwa anaridhia ni-PM
 
Kwa hiyo ni vibaya au vizuri mbaazi zikishuka bei?

Mkulima, pambana na hali yako...sisi huku mjini hiyo ni habari njema, tumepata fursa ya kujamba kwa kuvimbiwa mbaazi.
 
Jamani, mbona hali inakuwa hivi? Masikini twende wapi? Rais katwambia tukalime, tumelima bado bei mbovu
 
Biashara ya kilimo unaweza kufilisika huku unajiona.Masasi mbaazi bei ni 300,hivyo ukiwa na tani 1unapata 300,000/.
 
Duh hiyo bei in huko kusini tu au hata hapa masoko ya Dar,ili nipige mbadala badala ya maharage mengi unaongeza stock ya mbazi ndani maana maharage yameshoot kama bei ya nyama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom