MB au data zinatengenezwa wapi?

Nimesoma coment zote ila bado sijajua MB zinatengenezwaje na wapi labda nina kichwa maji
 
MB - kwa kirefu ni Mega Bytes, ni kipimo cha mawasiliano (data connection)anachopewa mteja kutoka kwa mtoa huduma kwa kipindi fulani au kwa speed fulani, Au vyote kwa pamoja.
 
Wakuu me najua mahindi aliumba Mungu watu wakapanda mbegu na kuvuna mpk leo hii tuna kula ugali.

Sasa tunataka kujua hzo MB wamechukua Nini na Nini tukapata access za kufikia server flan na huku kwetu Kwan hatuwezi kuunganisha hvyo vtu tukawa na mb zetu.


Mpk Sasa hakuna majibu.
Na isitoshe IT wamejaa humu.
 
Aje mtu aseme Kuna components gan mpk Elon anaweza kuwa nazo kutokea juu au sisi tunaweza kuunda kupata hizo MB
 
Hujajibu swali bado. Ameuliza hizo Mb zinatengenezwa wapi? Je mtu anaweza kijitengenezea za kwake binafsi?
 
Na mimi nauliza data budlles zinatengenezwaje?
 
Hujajibu swali bado. Ameuliza hizo Mb zinatengenezwa wapi? Je mtu anaweza kijitengenezea za kwake binafsi?
Umesoma uzi wote kuona comments za watu wengine au umekuja kwangu moja kwa moja?
 
Naelezea kwa namna nyengine

Internet inafanya kazi kwa mechanism mbili downloading na uploading.

Kuna policies wameziconfigure kwenye vifaa vya mtandao mfano IN (intelligent node) labda mtu akilipa 2000 apewe ruhusa ya kutumia infrastructure kwa siku 7 kwa MB 1000, hii inamaana utaruhusiwa kudownload na kuupload MB1000 ndani ya siku 7

Hivyo MB za kwenye internet ni ruhusa tu ya wewe kutumia infrastructure au miundombinu ya mtandao muda wako ukiisha wanakudisconect.

Au mfano mwengine

Barabarani nimeweka barrier

Nakuruhusu kupitisha magari matano badala ya hapo nafunga barrier

Barabara ni miundombinu ya internet

MB ni magari matano uliyoyavusha kwenye barrier

Internet ni ile ruhusa ya kupita akifunga barrier hakuna internet
 
na kuna watu hawajui MB ni nini na wameshonola tu hapa
 
Yaani unatakiwa uwe na nini na nini uwe na uwezo wa kutengeneza Mb zako? Hao wenye miundombinu mikubwa wanafanyaje ili wauze mb? Nadhani mtoa mada anataka aweze kuzitengeneza bila kupitia kwa mtu,au miundombinu ya mtu.
 
Shukran kiongoz nyiny ndio munatakiwa hapa jf
 
Umesoma uzi wote kuona comments za watu wengine au umekuja kwangu moja kwa moja?
Nadhani nimejibu baada ya kusoma yako,anyway kuna wengine wamejazia nimepata mwanga,ni mada nzuri ya kujifunza/ kufikirisha. Tuendelee kuelimishana.
 
Ivi mbona watu wanajibu tofauti kabsa na walichoulizwa na mleta mada ?

Mleta mada kauliza Mbs zinaundwa kwa kutumia vitu gani au kwa maana nyingne ni vitu gani vya kushikika unaweza kuviunganisha pamoja vikatengeneza hizo Mbs.... Lakini naona watu wanajibu vitu tofaut kabsa, sasa sijui tatizo ni ujinga au ni nini shida ?
 
Yaani unatakiwa uwe na nini na nini uwe na uwezo wa kutengeneza Mb zako? Hao wenye miundombinu mikubwa wanafanyaje ili wauze mb? Nadhani mtoa mada anataka aweze kuzitengeneza bila kupitia kwa mtu,au miundombinu ya mtu.
Ili usitumie miundombinu ya mtu inabidi usambaze waya mwenyewe dunia nzima. Kama unataka kumtext mtu China uhakikishe waya zako zinatoka Tanzania hadi China, kifupi sio realistic kutotumia miundo mbinu ya Mtu, Hata Hao Mapapa kina Voda na Tigo waya za watu zilivyo katika na wao Waliathirika, Internet ni muunganiko wa miundombinu ya watu wengi mno.
 
Kwahiyo ukiwa na miundombinu mfano ka mnara na vifaa vingine(intaneti). Je unaweza kutengeneza Mb? Kuwa na ule uwezo wa kampuni kama airtel na Tigo?
Je wao kampuni za simu wana miundombinu tu au wanalangua uwezo wa kuchakata mb kupitia hiyo mikongo ya baharini inayozunguka dunia nzima?
 
Ewaaaa... hapo sasa nimekulewa vyema. Kwahiyo kuna namna nao akina tigo wanalipia waya za watu na wao wakipata huduma zinazotokana na waya hizo wanatuizia sisi,ndio maana bei hazitofautiani sana za vifurushi. Asante sana !
 
Huyu mwamba ana akili kubwa mno. Naomba namba yako japo nikununulie maji unywe.
Huyu anaumiza kichwa namna ya kutatua tatizo na sio Hawa wanaowaza namna ya kula mbususu kimasihara.
Nishawahi fuatilia namna ya kutoa hela benki ama kwa ATM.
Yaani ningesoma hacking ningekuwa na hack mbaya Kuna saivi wakenya wanavyowaibia watanzania eti mchongo wa UNICEF unaambiwa tuma hela ili utumiwe hela na watu wanatuma
 
MB ni Si unit ya Data tu, popote pale kwenye kifaa kinachopitisha data kuna MB.

Mfano una Deki na TV na waya HDMI, Deki na TV umeziunganisha na HDMI na unaangalia movie kila sekunde ikipita kuna mb kadhaa zinapita Toka kwenye deki kwenda kwenye tv.

Kina voda na Tigo nao ni hivyo hivyo wana waya zao kama HDMI zinazopitisha data, zinaitwa Fiber, kikawaida ulitakiwa tu ukilipia utumie internet bila bugudha ya kupimiwa utumie mb ngapi, ila sababu tupo wengi na minara haina uwezo wa kutuhudumia wote kwa pamoja ndio wanaweka hio limit ya MB.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…