Mazuri ya mahusiano/ndoa

Of course, hakuna ukiona mchele tu, jua kuna aliyechambua chuya.

Hakuna mchele bila chuya, ishu huwa ni ratio ya mchele na chuya.

Ishu ni co-existence...kama mamba wapo then kenge lazima....mchele kwa chuya.....mwambie Husninyo mapenzi yapo hivyo....kung'ata jiwe wakati unakula ubwabwa hakufanyi ubwabwa wote uwe mbaya...kifundo cha muwa kina utamu wake pia...
 
Last edited by a moderator:
Ndoa huwa ni nzuri sana ukijua upo kwenye ndoa kufanya nini..... hii ni kwa wote, wakaka na wadada.......
Mapenzi/karaha/raha/shida/migogoro/machungu/n.k. vinaingizwa ndoani na wenye ndoa wenyewe.....
Tunaamini kuwa hakuna mkamilifu hapa duniani, unajiinuaje unapoanguka, hilo ndio la msingi zaidi..... je mwenzio anakusaidiaje anapogundua umeanguka, hilo pia ni swala jingine.
Mimi ninapoanguka, kama binadamu wa kawaida, kama nipo kwenye ndoa na mtu ambaye anajua kuwa mimi ni wake nategemea atanisaidia nisimame, na siyo kuendelea kunikandamiza ili nisiinuke. Mkiwa mnasaidiana hivi basi mtaona maisha yenu yanaendelea vizuri sana hata kama hampelekani honeymoon HongKong, au kununuliana expensive gifts.
Raha kubwa kabisa ya ndoa ni maelewano. Kwangu sioni kama nitakuwa na raha ndoani kama nanunuliwa liVX, napelekwa expensive treatments na kupewa kila kitu na hapo hapo sina maelewano mazuri na huyo mtoaji (Hii ni kwangu, kila mtu ana uzuri anaoutaka)
 
Back
Top Bottom