Mazuri ya CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mazuri ya CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlenge, Jun 11, 2011.

 1. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #1
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 433
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  Hapa hebu tuposti mambo mazuri ya CCM.

  1. Kukubaliana na hali halisi ya kuruhusu uhuru wa kuongea, ukilinganisha na ilivyokuwa miaka ya zamani; na hata wakati mwingine ukilinganisha na nji fulani za Kiafrika.

  2. Hebu ongezea hapo...

  NB: Haina maana kwamba CCM haina mabaya inayofanya. Hapa tutaje mazuri. Mabaya ya CCM yapo karibu kila mjadala mwingine hapa ukumbini. Hata Idd Amin (S.I. Unit ya ubaya kwa Watanzania tuliosikia kuhusu Amin kupitia vita vya Kagera) alifanya mazuri kwenye baadhi ya mambo (gazeti la Serikali ya Uganda The New Vision lilipata kuandaa makala mahsusi kwa ajili hiyo).


  Baada ya mada hii tutajadili mabaya ya CHADEMA (mazuri ya CHADEMA yapo kila mahali ukumbini hapa).
   
 2. h

  hans79 JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Uliwe kidogo nalo umelisahau
   
 3. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Huko miaka ya zamani aliyezuia uhuru wa kuongea alikuwa nani? anayesema mwisho saa 12 jioni kufanya mkutano wa kisiasa ni nani? anayesema ili uandamane unahitaji kibali kutoka polisi ni nani vile?
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Yaliyokuwa Mazuri ya CCM
  1. Matabaka --- Hatukuwa na Matabaka yeah kuna watu walikuwa na pesa lakini hawakuwa wanakufuru kama sasa hivi Majumba ya $2m Dollars
  Lakini hauoni wapi angeweza kupata hizo pesa kujenga hilo hekalu na kukimbilia Ardhi hii itatuua
  2. UDINI --- Kweli hatukuwa tunanyanyasana kidini kama hivi; yaani watu wana redio na kusema mabaya ya dini za wengine; hata Viongozi hao wa CCM wanunga mkono hizo radio
   
 5. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #5
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 433
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  Safari bado ndefu! Ikiwa mawazo yetu yatakuwa ni kwamba lazima sote tuwe na mtazamo mmoja, ndio maana nchi yetu inadidimia!

  Ninayo mengi ya kuishutumu CCM, kama ambavyo watu wengi wanavyoweza kukishutumu chama-dola chochote, lakini hii si sababu ya kuzuia mtu kuona mazuri ya CCM (hata kama ni machache) na mapungufu ya vyama vya upinzani.

  Hata hapa pakiwa "zidumu fikra..." tutafika?
   
 6. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,057
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  CDM haijawahi kuunda na kuongoza serikali sasa iweje tujadiri kitu ambacho madhara yake yanaishia kwa wanachama tu,ya nini?ukisema CCM ni sawa kwa maana ndo kimetengeneza serikali tokea 77 na kwa maana hiyo hata asiye mwanachama bado anadhurika na serikali ya CCM indirectly

  Ntarudi baadae
   
 7. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Kwa nia njema na kwa lengo la kutaka kujielimisha naomba watu ambao wanayajua mazuri ya CCM wanitajie; Hii ni pamoja na yale yaliyofanywa na TANU na ASP

  1. CCM kama TANU walileta uhuru
  2. CCM ilijenga umoja wa kitaifa
  3. CCM ilitetea wakulima na wafanyakazi
  4. CCM ilifanikisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar
  5. Zanzibar ilijenga nyumba za makazi kwa watu masikini
  6. CCM iliruhusu mfumo wa vyama vingi
  7. CCM ilianzisha azimio la Arusha (misingi ya utu)
  8. CCM elimu kwa wote, elimu bure kwa shule za misingi
  9.
  10.
  11.
  12.
  13.

  .
  .
  .
  Nawasilisha, nataka kujifunza ili nijue kama natoa hukumu ya kweli au nakosa taarifa sahihi
   
 8. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wanajf, Pamoja na shida na mapungufu yote ya serikali yetu ktk kutimiza ahadi zake, Je ikiwa utalazimika kutaja ( sincerely and honestly) jambo ambalo unadhani serikali imejitahidi, litakuwa lipi?? Nasema hivi kwa sababu uongoz hauwezi kuwa mbaya na mbovu asilimia mia, na wala haiwezekani ukawa mzuri asilimia mia. Tujadili kama great thinkers!!
   
 9. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mimi walivyomaliza mgogoro wa serikali na madatari walinikosha sana,
  Na walimu hawa watu wasumbufu bwana, viva ccm vivaaaaaaa!
   
 10. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Duuuh... nachungulia nachungulia sana ... lakini..duuh... ngoja nikachukua microscope
   
 11. Senkenke1

  Senkenke1 Member

  #11
  Aug 14, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Wanajamvi nimeona leo tujadili mazuri ya CCM ambayo wameyafanya ili tuone upande mwingine wa shilingi maana hapa kila kitu kina pande mbili.
  1. Uomoja kitaifa
  2. Amani na Utulivu
  3. Kuondoa udini
  5. kuukema ukabila
  6. Daraja la Kigamboni coming soon
  7. kukubali upinzani
  8. Ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wote ambapo collateral ni deposits zao za NSSF na PFPF PPF
  9. Ujenzi wa babrara nchi nzima
  10. Ujenzi wa Udom na vuo vikuu vingi vya kumwaga.
  11.
  12.
  13.
  14.
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Aug 14, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mbona sisi bei ya pamba kila mwaka anatupagia tu.
   
 13. igwana123

  igwana123 Senior Member

  #13
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Usisahau Mabasi ya mwendo kasi
   
 14. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #14
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Safii in short mazuri ni mengi sana sana tunaweza kuandika vitabu kadhaa ukifanya uchambuzi yakinifu na kuacha kusikiliza kelele za hao wanaolialia kama mbuzi
   
 15. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #15
  Aug 14, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mengine haya hapa...

  [​IMG]
  Akina mama wakiwa hospital, DSM Tanzania.


  [​IMG]

  Dr. Ulimboka baada ya kupata kipigo. LIWALO NA LIWE.
   
 16. mito

  mito JF-Expert Member

  #16
  Aug 14, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,643
  Likes Received: 2,030
  Trophy Points: 280
  Yaani tangu uhuru (miaka 50 iliyopita) ndo haya tu mnajivunia, loh!
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  Aug 14, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Yaani wewe umeongea kinyume kabisa umoja gani wa kitaifa uliko kwasasa...Wazanzibar wanataka nchi yao, tulisikia kisiwa kimoja huko mwanza kilijitangazia nchi yake na hata huko singida kuna sehemu walijitangazia nchi yao huo ndiyo umoja wa kitaita kwanini watu walifikia kujitangazia nchi yao ndani ya nchi, je huko Loliondo si kuna nchi ndani ya nchi.
  2. watu wameuwawa sana na jeshi la polisi mfano Arusha kwenye maandamano, Arumeru vijana wanne walokotwa wakiwa wameuliwa kwa kunyongwa na mauwaji mpaka leo yanaendelea, huko mara mauwaji kila mara....
  3. udini umeshamili kuliko kipindichocho kama una bisha sikiliza redio Imani.
  4. Udini unakemewa kinafiki huku CCM ikijaribu kutumia ukabila na udini kuwa gawa watanzania.
  5.Daraja kama watajenga siyo kitu cha kujivunia kiivyo ukizingatia ni mifuko ya jamii ambazo ni haki yetu licha ya kwamba tuna lipa kodi lakini imeshindwa kulisaidia taifa wameingilia kwenye mifuko hii kutukamua.....
  7. kukubali upinza si kwa mapenzi ya kikwete ni ya mataifa makubwa ukizingatia kila kukicha anaenda kuombaomba...
  8.....hili silijui
  9.barabara zilianza kujengwa kipindi ya kuuza mashika ya umma kipindi cha mpaka kikwete akaingia na chuki zake binafsi akamwondoa Magufuli madokeo yake ikawa ujenzi wa kilomita 1 bil 1.6 kutoka milioni 700 kama sikosei lakini naona sasa hivi Magufuli karudi amepuguza kwa kasi ya jabu hivyo kama kikwete angekuwa makini angechuguza na nina uhakika kuna watu wange nyea debe.
  10.Vyuo vya kumwaga hebu tuwekee hapa na vilianza lini kujengwa.
   
 18. Las Mas Bobos

  Las Mas Bobos JF-Expert Member

  #18
  Aug 14, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 993
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii ndio nzuri zaidi

  [​IMG]
   

  Attached Files:

 19. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #19
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mleta hoja anaishi nchi gani? Kama ni mzima kiakili basi ni mzembe wa kufikiri.

  Hayo anayosema yameletwa na CCM hakuna hata moja zaidi ya CCM kuyahujumu.

  AMANI-Tanzania hakuna amani bali woga wa kawaida wa watanzania kupambana na majambazi yenye madaraka yanayowaibia. Sana sana CCM inavuruga amani kama kuwapiga waandamanaji kila mara huku ikivuruga amani kama vile kuteka watu wanaoipinga au kuwatishia.

  UMOJA- Hakuna umoja zaidi ya umoja wa kifisadi. Ungekuwapo umoja watanzania wangeishaitimua CCM.

  UDINI- Udini upo sana hadi kufikia kutumia bendera ya taifa kwenye meli za taifa la kiislam la Iran. Pia rejea Kikwete kuchagua watendaji kama vile majaji na wakuu wa mikoa na wilaya kuzingatia dini huku akiacha mihadhara ya kukashfu dini nyingine ikishamili.

  KUKUPALI UPINZANI- Tanzania upinzani haukubaliki. Rejea mfumo wa vyama vingi kuanzishwa kwa shinikizo la wafadhili. CCM imekuwa ikihujumu upinzani kwa njia zote kuanzia kuwazuia kujitangaza na kutuma nyemelezi kama Maalim Seif Lipumba, Mrema, Mbatia, Zitto, Cheyo, Kaboro na wengine wengi kuuvuruga.

  BARABARA-Zinajengwa kwa pesa ya wafadhili huku CCM ikiziiba na kujenga barabara zisizofikia hata viwango.

  DARAJA LA KIGAMBONI- Halijengwi CCM bali pesa za watanzania zinazoibiwa na mafisadi waliomo serikalini.

  UJENZI WA NYUMBA-CCM iliiba nyumba za umma chini ya utawala wa Mkapa na kugawana miongoni mwa wezi wakubwa.

  VYUO VIKUU-Havijengwi na CCM bali mashirika ya dini na pesa ya umma.
   
 20. peri

  peri JF-Expert Member

  #20
  Aug 14, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  ccm wana mazuri yao na mabaya pia. Kinachonishangaza ni watu wanaojifanya vipofu na kujaribu kupotosha hata pale wenzao wanapopatia.
  Tuache unafik, penye ukweli pasemwe tu, kama mtu kapatia msifie, akikosea mkosoe.
  Tuache ushabik wa kibubusa.
   
Loading...