mito
JF-Expert Member
- Jun 20, 2011
- 10,811
- 11,032
Jamani naenda moja kwa moja kwenye mada.
Mazuri
1) Kwa mara ya kwanza Bajeti hii haijaongeza kodi za magari, sigara na vinywaji kama ilivyozoeleka. Hii nimeipenda sana.
2) Bajeti hii pia imeendelea kumjali mfanyakazi kwa kupunguza PAYE kutoka 12% to 11%. Hii ni hatua nzuri ingawa mngeipunguza hadi 9% ndo ingekuwa safi sana.
3) Bajeti hii imeweka kodi katika vyuma, sukari, na mchele unaoingizwa nchini. Huko nyuma hivi vitu vilisamehewa kodi ili kuhamasisha uingizaji wake kwa vile tulikuwa na upungufu wa bidhaa hizi katika soko letu.
Waziri kasema sasa hivi tunajitosheleza katika bidhaa hizi, hivyo Serikali imeweka kodi kwa bidhaa za nje ili kulinda wazalishaji wa ndani. Kama kweli tunajitosheleza, lengo ni zuri kabisa.
Mabaya
1) Bajeti hii imeongeza kodi kwenye mafuta ya dizeli, petroli na mafuta ya taa. Wenyewe wanadai ongezeko hili ni kutunisha mfuko wa umeme vijijini (REA). Sawa ni wazo zuri, lakini mjue ongezeko hili litasababisha kila kitu kupanda na maisha kuzidi kuwa magumu zaidi kwa wananchi. Napendekeza ongezeko hili liondolewe tu zibakie kodi za zamani za REA. Vinginevyo usafiri wa daladala utapanda, nauli za mabasi zitapanda, chakula kitapanda sokoni mpaka Wananchi watachukia na kuona ni Bajeti ya hovyo kabisa.
2) Bajeti hii imeanzisha kodi mpya bandarini ambayo haikuwepo, inaitwa Tozo ya Kuendeleza Miundombinu (Infrastructure levy) ya 1.5% ya CIF value. Kama hii kodi inahusu kila bidhaa inayopitia bandarini inamaana tumepigwa changa la macho kwenye magari. Pale juu (No.1) wamejifanya hawajaongeza kitu, kumbe tunakuja kupigwa kupitia kodi hii. Binafsi sikuelewa vizuri Waziri aliposema wanaanza na Reli, so aliyeelewa vizuri tafadhali nielemishe vizuri kuhusu kodi hii.
Changamoto
1) Bajeti yetu ina jumla ya Trilion 24 (kama sikosei), cha ajabu deni la taifa ni Trilion 35 haaaaa yaani tunadaiwa zaidi ya Bajeti nzima ya Serikali, khaaa!! Hizi figure zimenisikitisha sana.
2) Sijui Serikali imejipanga vipi kupambana na Wafanyabiashara wasio waaminifu, wasiojali kabisa Wananchi. Hapa namaanisha hapo No 3 katika listi ya mazuri. Mnaofuatilia mambo mtakumbuka kuwa wafanyabiashara wa sukari wamekuwa na mchezo mchafu wa ku-create artificial scarcity ili kupandisha bei ya sukari. Wananchi waliumizwa sana na bei za kilanguzi za sukari. Kilio chetu kilipelekea Serikali kuruhusu sukari ya nje ikiamini kuwa tuna upungufu wa sukari nchini. Lakini baada ya sukari ya nje kuanza kuingia na kufanya bei ku-stabilize wafanyabiashara hao walianza kuilalamikia Serikali kwa kuruhusu sukari ya nje ingie nchini bila kodi na kufanya ya kwao yenye bei ya kilanguzi isinunulike.
Mchezo huu pia ulifanywa na wafanyabiashara wa mchele, nao huwa wana create articial scarcity ilihali wamefungia mpunga kwenye magodauni yao. Hapa pia serikali iliamua kuruhusu mchele wa nje ili kutusaidia na bei za kufa mtu tulizokuwa tunapigwa huko sokoni. Kama mnavyojua hawa nao walikuwa wanailalamikia serikali kila kukicha. Hata humu JamiiForums kule kwenye jukwaa la biashara kuna mabandiko kibao ya kulalamikia Serikali.
Wafanyabiashara wa vyuma nao hali ilikuwa ile ile, tena wao wakawa wanasingizia eti ujenzi wa uwanja wa taifa ndo umesababisha vyuma vimekuwa adimu nchi. Cha ajabu Serikali ilipoamua kuruhusu vyuma vya nje viingie nchini, leo wanadai eti wana vyuma vya kutosha kusupply soko la ndani.
Kimsingi ni wafanyabiashara hao hao ndo walio lobby kwa Serikali kuweka kodi kwa bidhaa hizi ili kulinda soko la bidhaa zao nchini. Sasa swali langu liko pale pale, baada ya serikali kuwakubalia ombi lao na sasa imeweka kodi kwenye bidhaa hizo, je Serikali imejipangaje kuwadhibidi wasirudie huo mchezo wao wa kuwakamua wananchi?
Jamani haya ndo niliyoyaona mimi kwenye hii bajeti yetu iliyotangazwa jana. Usisite kunisahihisha pale nilipoelewa vibaya, na wewe pia unaweza kuongezea uliyoyaona.
cc The Boss, BAK, Kimweri, MTAZAMO, Mkandara, Lizabon, Rweye, Edson, baro, DSN, JokaKuu, Rahim Jr, eddy, Matola, Pasco na wengineo