Mazuri ni pembejeo kuendelea kuwa Tax free...nakerwa na deni la Taifa kila linapopanda na nikioanisha maendeleo yetu sioni RATIO.Pia kama anavyosema Mkandara kuhusu budget mie uwa NAUMIA sana na STANDARD OF LIVING yetu na kila budget inapokuja sioni majibu ya TATIZO LA MAISHA YA WATANZANIA yakiboreka toka hatua moja kwenda mbele zaidi kila budget inapotoka ni Mwanzo wa ugumu mwingine wa Maisha WHY THAT?.Sio kuwa jibu lake sina ninalo ni RUSHWA Na UFISADI yani budget invyotoka hivi kuna watu wanatizama zipigwe zipi.
Kwanini tusiwe na TAIFA watu wawe PROUD siku moja mtu akiona WATANZANIA wanavyonawili kwa MAISHA BORa yeye anaona fahari kuwa HE HAS DONE IT.Roho ya kuona Mwanadamu mwenzio kapata furaha sababu umefanikisha furaha yake hiyo UMEPOTELEA wapi mbona wakina Nyerere kwa Budget ndogo walifanya Makubwa leo tuna Trioni 22 bado FURAHA za Watanzania ni MANUNG'UNIKO MBAYA.
Naota siku moja budget yetu inaweza kutoka mfano, sekta ya miundo mbinu ikaenda kujenga miundo mbinu kwenye viwanja ambavyo ni PLOT za kuuzwa ili watu wajenge viwanja vikiwa well planned na miundo mbinu yote ilishajengwa kama Sewage System, Umeme, Simu na Wasiliano Mengine Kama Internet, Barabara na Maji yako well fixed kila mtaa kisha walio uziwa plot wanaanza kujenga nyumba kwenye PLOT ambazo zilishapewa kila HUDUMA muhimu husika.
Ni msimu wa mafungu watu wakafanye yao!!!believe me kuna Matycoon huwa wanasubilia kuona safari wizara gani inapesa nyingi kwa ajili ya ununuzi wa MALI YA UMMA , magari, mitambo nk wawaweke sawa wanao husika watu wapige mambo...
Katika kuwaza sana hivi kuna any WATCHDOG maalumu kweli wa kuhakiki MAPATO NA MATUMIZI YA BUDGET kila inapotoka na kule inakokwenda kutumika na Je imetumika inavyopasa.Najua kuna kamati za Bunge lakini bado si JIBU sahihi...mimi ni muumini wa kutengeneza CONFLICT of INTEREST yani kuwepo kwa Taasisi zinazogangana wakati mwingine katika kufuatilia jambo moja kila kimoja kikitoka angle yake basi UWAFANYA wahusika wawe makini na matumizi kwa kuwa kila mmoja anakuja na Interest yake kufuatilia Jambo moja.