Mazoezi ya miguu (lower body workout) hasa vigimbi

HumbleBoy98

JF-Expert Member
Aug 30, 2020
386
392
Mambo vipi wakuu? Natumaini mko poa.

Wakuu mimi ni mdau wa mazoezi ya kujenga mwili japo Sina hela ya kwenda Gym huwa najipigia push up zangu mwenyewe tu, hata hivyo sipo interested Saana na mazoezi ya kunyanyua vitu vizito.

Ninachohitaji sasahivi ni mazoezi ya miguu (lower body workout) hasa vigimbi vya miguu maana nina fito hizo mpaka naona aibu kuvaa pensi!

Kwa kifupi nataka kutengenexa lower body especially calf muscles ila bila kwenda gym.

So wadau nisaidieni mazoezi ambayo naweza nikayafanya hata nyumbani ya kutengeneza mwili wa chini ili na Mimi nikivaa jeans itune-tune kidogo nikivaa pensi nisichekeshe watu.

Karibuni!
 
Easy!

Una watoto? Kama unao na ni wakubwa kiasi, unaweza ukafanya calf raises huku umewabeba mabegani.

Au kama una begi la mgongoni, unaweza kuliwekea vitu likawa zito kiasi halafu unapiga hizo calf raises.

Piga sets na repetition za kutosha mara kama mbili au tatu kwa wiki.

81F7E715-D3B3-489A-8807-552E3EF2CB1C.jpeg
 
Mguu inabidi usiwe na kigimbi.

Kupata kigimbi siyo kazi na kama mguu wako ni mwembamba utazidi kuwa kituko.

Hauta furahia huo muonekano mpya.

Ingia YouTube andika foot exercise zitakuja video za muongozo kuna mazoezi hadi ya kiganja cha mguu.
 
Lakini mkuu huyu kajibiwa kutokana na hitaji lake, kataka Kigimbi, ila ulichofanya ni bora zaidi, umekuwa kama mchina ukiomba kitoweo anakupa ndowano kwa maana kajivulie mwenyewe na usijeomba tena kitoweo, ina maana hatokuja usingempa ushauri huu yawezekana kesho angekuja na jengine.
Bravo.
 
Easy!

Una watoto? Kama unao na ni wakubwa kiasi, unaweza ukafanya calf raises huku umewabeba mabegani.

Au kama una begi la mgongoni, unaweza kuliwekea vitu likawa zito kiasi halafu unapiga hizo calf raises.

Piga sets na repetition za kutosha mara kama mbili au tatu kwa wiki.

View attachment 1792306
Thanks mkuu!
Sina watoto Bado ila nitafanya hiyo ya kuweka begi lenye uzito mgongoni!e
Maybe reps20 kwa set 5 zinaweza tosha🤔
 
Kakimbie sehemu yenye mchanga mwingi sana, kama upo karibu na beach nenda ufukweni kimbia kwenye michanga.

Kimbia kupandisha vilima.

Fanya zoezi la kujinyanyua kama unataka kusimamia vidole vile.
Asante mkuu kwa mchango wako.
Nilipokuwa dar nilikuwa naenda Coco Beach ila saivi Niko Masasi huku!
 
Mguu inabidi usiwe na kigimbi.

Kupata kigimbi siyo kazi na kama mguu wako ni mwembamba utazidi kuwa kituko.

Hauta furahia huo muonekano mpya.

Ingia YouTube andika foot exercise zitakuja video za muongozo kuna mazoezi hadi ya kiganja cha mguu.
Mmh! Mkuu sijakuelewa, mguu unatakiwa usiwe na kigimbi? Na kwa Nini uwe kituko?
 
Mmh! Mkuu sijakuelewa, mguu unatakiwa usiwe na kigimbi? Na kwa Nini uwe kituko?
Hajui anachokisema huyo mguu unenepe bila kigimbi huo ni ubonge(mafuta) pia genetically ngumu sana mguu kunenepa ukiona mpaka mguu umenenepa basi Upper Body hutamaniki Fat as fak.
 
Hajui anachokisema huyo mguu unenepe bila kigimbi huo ni ubonge(mafuta) pia genetically ngumu sana mguu kunenepa ukiona mpaka mguu umenenepa basi Upper Body hutamaniki Fat as fak.
And kuwa na mguu ulonenepa bila kigimbi unakuwa kama mguu wa mwanamke tu .(mguu wa bia)
 
Back
Top Bottom