Mazishi ya Kamanda Shelembi Shinyanga Mjini

Dumelambegu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,052
257
Wandugu,

Jamani wadau mliopo huko Shinyanga Mjini mtuhabarishe na ikiwezekana hata ku-post picha za mazishi ya Kamanda Shelembi aliyepokwa ushindi wa Ubunge wa Jombo la Shinyanga Mjini. Kuna ndugu yangu mmoja amenidokeza anasema njia zote hazipitiki huko jinsi watu walivyofurika kuaga mwili wa marehemu kwenye viwanja vya Shycom.
 
GreatThinkers;

Watu wamejazana sana hapa viwanja vya Shycom, wananchi wanahasira iliyochanganyika na majonzi.

Pande za Ngokolo nimeshuhudia jamaa kapigwa makofi kisa kavaa kofia lile la kijani.

Viongozi wa chama tawala (mioyoni mwa wananchi) wa CDM wako hapa karibu wote Dr Slaa, Mh Mbowe, Mh Kabwe, KIna Mh Wenje, Mh Lema, Mh Tundu Lisu nk

FFU wametawanywa kila mahali na magari yao ya maji machafu na mabomu ya machozi.

Hali si shwari kabisa.

Frontliners wote muwe makini sana saivi hilo gamba halivuliwi kwa heri, naamini kuna jambo linawauma.

Wana CDM wote waliowahi kugombea jimbo lolote na bado wanakubalika wawe very makini.
 
Poleni sana Shy.

Shy ni stratergy area kwa Tanzania kwa kila jambo. hayo yote yatapita haki ipo njiani inakuja kwa kasi kubwa hawataweza kuizuia kwa maji ya kuwasha wala mauwaji ya raia wasio na hatia.

Wana-hubiri amani wakati roho zao zimejaa chuku na ubaguzi!
 
Jana mji wa shinyanga ulizizima kwa majonzi kwa kifo cha mpigania haki na mmpenda mageuzi ndg magadula philip shilembi ambaye ni m/kiti wa cdm mkoa wa shinyanga na diwani, mgombea ubunge aliyeshindwa kwa kura mmoja.

Viongozi wakuu wa cdm waliongoza mazishi yake, burian mpigania uhuru wa kweli
 
Back
Top Bottom