Mazingaombwe yanayotokea Uturuki

mzaramo92

Member
May 3, 2016
7
16
MAZINGAOMBWE YANAYOTOKEA UTURUKI.

Tarehe 16-17 mwezi wa saba mwaka huu dunia ilipata mshtuko baada habari za kuwapo
Kwa jaribio la kupindua nchi uturuki kupitia vyombo mbalimbali vya habari duniani na baadae zikaenea habari kuwa jaribio hilo limeshindwa.

Itakuaje kama ntakwambia kwamba hakukuwa na jaribio la kupindua nchi uturuki, lakini kama hakukuwa na jaribio la mapinduzi ya nchi ni nini kilitokea? Kwa maono yangu kilichotokea Uturuki ni mazingaombwe. Kwanini?

Mosi, katika jaribio lolote la kupindua nchi waasi lazima wamuweke rais wa nchi husika kwenye himaya yao (kumteka) au ikiwezekana kumuua kabisa, na hapo mapinduzi hayo yatakuwa yamefanikiwa kwa asilimia zaidi ya 70. Lakini kilichotokea Uturuki ni waasi kukataa kumuua rais wakati walikuwa na uwezo wa kufanya hivyo, wakati jaribio la mapinduzi linatokea rais Tayyip Erdogan alikuwa kwenye ndege anatokea kwenye mapumziko mjini Marmaris na waasi walikuwa wameshatuma ndege mbili aina ya F-16 (kumbuka ndege aina hii ndio ilitumika kuiangusha ndege ya kivita ya Urusi Su-24) na zikafanikiwa kuikaribia ndege ya rais lakini Hamna ndege Hata moja kati ya hizo mbili zilizotumwa na waasi hao ilithubutu kuishambulia ndege ya rais. Kwa kauli ya kawaida unaweza kuona kama kweli walikuwa waasi kwanini wasitungue ndege ya rais na process zilizobaki (ambazo zingekuwa ndogo zifanyike), unaweza kuona hizi ndege zilitumwa kuilinda ndege ya raid na sio kuitungua kama ilivyolipotiwa.

Pili, waasi hao hawakuwa na sababu ya kushambulia Ikulu isiyo na rais ndani yake na kushambulia madaraja kwa vifaru. Kama kweli hao waasi walitaka kupindua nchi basi wangefanya kama uasi ulivyofanyika Rwanda mwaka 1994 tarehe 6 ya mwezi wa 4, ambapo waasi waliitungua ndege ya rais Habyarimana akiwa anatokea Tanzania na baada ya hapo uasi wao ukawa umefanikiwa. Hawa walichofanya Ni kushambulia madaraja kwa vifaru na kusababisha "public fear" ndani ya mji was Ankara na nchi kiujumla, mpaka hapo utaona lengo kuu la waasi wa Uturuki halikuwa kumtoa rais madarakani bali ni kusababisha uoga ndani ya jamii.

Tatu, maamuzi ya kwanza ya rais baada ya jaribio hill kufeli Ni kufukuza na kusimamisha wakuu wa vyuo na ma-dean wa vyuo vikuu nchi nzima. Hivi fikiria kama nchi imetoka kunusurika kwenye kupinduliwa kijeshi lakini maamuzi ya mwanzo badala ya kusafisha jeshi kwanza unasafisha wakuu wa vyuo vikuu, mfano kutokee tukio kama hili Tanzania alafu baada ya kushindwa Mh. Rais wangu mtukufu Dr. Magufuli awafukuze Prof. Mlacha wa UDOM na Prof. Mukandala wa UDSM. Inakuingia akilini? Unahisi mini kinaendelea? Hauwezi kuwaogopa wakuu wa vyuo vikuu kwenye kipindi kigumu kama hicho kuliko kuwaogopa wanajeshi waasi.

Nne, ndoto za rais Tayyip Erdogan kurudisha enzi za Ottoman Empire na kujirundikia madaraka baada ya tukio hill la uasi. Tarehe 30/05/2016 rais Recep Tayyip Erdogan was Uturuki akuhutubia taifa na dunia katika maadhimisho ya miaka 526 baada ya ushindi wa Ottoman empire rais huyo wa Uturuki alipamba ikulu kuwa kama kasri ya mfalme wa tawala ya Ottoman, na kuweka kiti cha mfalme mbele yake na yeye kuketi hapo huku akizungukwa na vijana waliovalia kama vijakazi wa mfalme. Hii ilipelekea mashirika mengi ya habari kujadiri kama rais Taccep anataka rudisha tawala ya kifalme Uturuki na ikathibitika kuwa Ni mtu anayetaka kuongoza Uturuki kwa miaka yote ya uhai wake, ili kuhakikisha hayo juzi baada mazingaombwe ya mapinduzi mtawala huyo alipata nguvu na nafasi ya kufanya mabadiliko ya katiba ili kumpa nguvu yeye (rais) kufanya maamuzi bila kushirikisha bunge, pia kutunga sheria bila kushirikisha bunge na mwisho vyombo vyote vya ulinzi pamoja na shirika la ujasusi la Uturuki (MIT) Ku ripoti kwake moja kwa moja.

JE KWANINI MAZINGAOMBWE YOTE HAYA YAMETOKEA?

Lengo kuu la mazingaombwe ya mapinduzi ni kutafuta sababu ya kuwatoa Wote wanaompinga kisiasa ndani ya system ya uongozi. Inaonekana dhahiri shahiri kuwa rais alikuwa na majina ya watu wanaompinga kuanzia Ikulu, wizara mbalimbali, jeshini, polisi, idara ya ujasusi na kwenye taasisi za elimu Ila alikosa njia ya kuwatoa maana angewatoa Wote kwa wakati mmoja bila sababu kuu nchi za ulaya zingemtenga.

Hii imeshawahi tokea Marekani, pale walipotaka kuivamia Cuba kijeshi kipindi cha vita baridi lakini wakakosa sababu. Ndipo CIA walipobuni Mazingaombwe yao mwaka 1961 ambapo walitengeneza waasi nchini Cuba na kuwapa support ili wachukue baadhi ya maeneo ya Cuba arafu waasi hao kwa uangalizi wa CIA wapige makombora jiji la NewYork kutokea Cuba na mwisho ionekane Cuba wamewachokoza Marekani (Wapate sababu ya kuivamia Cuba), operation hii ilijulikana kama "Bay of pigs operation" na haikufanikiwa sababu rais J.F Kennedy alikataa kuidhinisha ulipuaji wa NewYork.

Mazingaombwe huwa yanafanyika ili taifa lipate sababu ya kufanya jambo Fulani, ya Uturuki yamefanikiwa.
 
MAZINGAOMBWE YANAYOTOKEA UTURUKI.

Tarehe 17 mwezi wa sita mwaka huu dunia ilipata mshtuko baada habari za kuwapo
Kwa jaribio la kupindua nchi uturuki kupitia vyombo mbalimbali vya habari duniani na baadae zikaenea habari kuwa jaribio hilo limeshindwa.

Itakuaje kama ntakwambia kwamba hakukuwa na jaribio la kupindua nchi uturuki, lakini kama hakukuwa na jaribio la mapinduzi ya nchi ni nini kilitokea? Kwa maono yangu kilichotokea Uturuki ni mazingaombwe. Kwanini?

Mosi, katika jaribio lolote la kupindua nchi waasi lazima wamuweke rais wa nchi husika kwenye himaya yao (kumteka) au ikiwezekana kumuua kabisa, na hapo mapinduzi hayo yatakuwa yamefanikiwa kwa asilimia zaidi ya 70. Lakini kilichotokea Uturuki ni waasi kukataa kumuua rais wakati walikuwa na uwezo wa kufanya hivyo, wakati jaribio la mapinduzi linatokea rais Tayyip Erdogan alikuwa kwenye ndege anatokea kwenye mapumziko mjini Marmaris na waasi walikuwa wameshatuma ndege mbili aina ya F-16 (kumbuka ndege aina hii ndio ilitumika kuiangusha ndege ya kivita ya Urusi Su-24) na zikafanikiwa kuikaribia ndege ya rais lakini Hamna ndege Hata moja kati ya hizo mbili zilizotumwa na waasi hao ilithubutu kuishambulia ndege ya rais. Kwa kauli ya kawaida unaweza kuona kama kweli walikuwa waasi kwanini wasitungue ndege ya rais na process zilizobaki (ambazo zingekuwa ndogo zifanyike), unaweza kuona hizi ndege zilitumwa kuilinda ndege ya raid na sio kuitungua kama ilivyolipotiwa.

Pili, waasi hao hawakuwa na sababu ya kushambulia Ikulu isiyo na rais ndani yake na kushambulia madaraja kwa vifaru. Kama kweli hao waasi walitaka kupindua nchi basi wangefanya kama uasi ulivyofanyika Rwanda mwaka 1994 tarehe 6 ya mwezi wa 4, ambapo waasi waliitungua ndege ya rais Habyarimana akiwa anatokea Tanzania na baada ya hapo uasi wao ukawa umefanikiwa. Hawa walichofanya Ni kushambulia madaraja kwa vifaru na kusababisha "public fear" ndani ya mji was Ankara na nchi kiujumla, mpaka hapo utaona lengo kuu la waasi wa Uturuki halikuwa kumtoa rais madarakani bali ni kusababisha uoga ndani ya jamii.

Tatu, maamuzi ya kwanza ya rais baada ya jaribio hill kufeli Ni kufukuza na kusimamisha wakuu wa vyuo na ma-dean wa vyuo vikuu nchi nzima. Hivi fikiria kama nchi imetoka kunusurika kwenye kupinduliwa kijeshi lakini maamuzi ya mwanzo badala ya kusafisha jeshi kwanza unasafisha wakuu wa vyuo vikuu, mfano kutokee tukio kama hili Tanzania alafu baada ya kushindwa Mh. Rais wangu mtukufu Dr. Magufuli awafukuze Prof. Mlacha wa UDOM na Prof. Mukandala wa UDSM. Inakuingia akilini? Unahisi mini kinaendelea? Hauwezi kuwaogopa wakuu wa vyuo vikuu kwenye kipindi kigumu kama hicho kuliko kuwaogopa wanajeshi waasi.

Nne, ndoto za rais Tayyip Erdogan kurudisha enzi za Ottoman Empire na kujirundikia madaraka baada ya tukio hill la uasi. Tarehe 30/05/2016 rais Recep Tayyip Erdogan was Uturuki akuhutubia taifa na dunia katika maadhimisho ya miaka 526 baada ya ushindi wa Ottoman empire rais huyo wa Uturuki alipamba ikulu kuwa kama kasri ya mfalme wa tawala ya Ottoman, na kuweka kiti cha mfalme mbele yake na yeye kuketi hapo huku akizungukwa na vijana waliovalia kama vijakazi wa mfalme. Hii ilipelekea mashirika mengi ya habari kujadiri kama rais Taccep anataka rudisha tawala ya kifalme Uturuki na ikathibitika kuwa Ni mtu anayetaka kuongoza Uturuki kwa miaka yote ya uhai wake, ili kuhakikisha hayo juzi baada mazingaombwe ya mapinduzi mtawala huyo alipata nguvu na nafasi ya kufanya mabadiliko ya katiba ili kumpa nguvu yeye (rais) kufanya maamuzi bila kushirikisha bunge, pia kutunga sheria bila kushirikisha bunge na mwisho vyombo vyote vya ulinzi pamoja na shirika la ujasusi la Uturuki (MIT) Ku ripoti kwake moja kwa moja.

JE KWANINI MAZINGAOMBWE YOTE HAYA YAMETOKEA?

Lengo kuu la mazingaombwe ya mapinduzi ni kutafuta sababu ya kuwatoa Wote wanaompinga kisiasa ndani ya system ya uongozi. Inaonekana dhahiri shahiri kuwa rais alikuwa na majina ya watu wanaompinga kuanzia Ikulu, wizara mbalimbali, jeshini, polisi, idara ya ujasusi na kwenye taasisi za elimu Ila alikosa njia ya kuwatoa maana angewatoa Wote kwa wakati mmoja bila sababu kuu nchi za ulaya zingemtenga.

Hii imeshawahi tokea Marekani, pale walipotaka kuivamia Cuba kijeshi kipindi cha vita baridi lakini wakakosa sababu. Ndipo CIA walipobuni Mazingaombwe yao mwaka 1967 ambapo walitengeneza waasi nchini Cuba na kuwapa support ili wachukue baadhi ya maeneo ya Cuba arafu waasi hao kwa uangalizi wa CIA wapige makombora jiji la NewYork kutokea Cuba na mwisho ionekane Cuba wamewachokoza Marekani (Wapate sababu ya kuivamia Cuba), operation hii ilijulikana kama "Bay of pigs operation" na haikufanikiwa sababu rais J.F Kennedy alikataa kuidhinisha ulipuaji wa NewYork.

Mazingaombwe huwa yanafanyika ili taifa lipate sababu ya kufanya jambo Fulani, ya Uturuki yamefanikiwa.
Kwa hiyo Rais wa Uturuki alifanya kama wale jamaa zetu "wanaojiteka".
 
Edogarn ni dictator haswa. Kama alivyokua Saddam enzi zake
Mh nahis hujamtendea haki sadam husein kwangu alikua ni MTU tofauti nikifuatilia historia ya Iraq alikua no kama mtu alotumwa kuikomboa iraq iwe sehem Salama kuuwawa kwa sadam Hussein Iraq ni sawa na kuuwawa kwa gadafi Libya hakuna faida kwa wananch zaid ya mateso yasiyo mwisho hawakuwa madikteta zaid ya watu waliopenda amani na utii udumishwe kwa njia yeyote salut kwa baada ya vifo vyao dunia imetambua umuhim wao
 
Duuh.. Kweli ikulu kuna raha yake... Ila inawezekana... Vipi kuhusu zile email zilizotolewa wikileaks..
Email niwatu wa chama tawala (chama chake) walikuwa wanatumiana. Hazikuhusisha wapinzani, so utaona mwenyewe nani kaandaa jaribio hili.
 
Mh nahis hujamtendea haki sadam husein kwangu alikua ni MTU tofauti nikifuatilia historia ya Iraq alikua no kama mtu alotumwa kuikomboa iraq iwe sehem Salama kuuwawa kwa sadam Hussein Iraq ni sawa na kuuwawa kwa gadafi Libya hakuna faida kwa wananch zaid ya mateso yasiyo mwisho hawakuwa madikteta zaid ya watu waliopenda amani na utii udumishwe kwa njia yeyote salut kwa baada ya vifo vyao dunia imetambua umuhim wao
Sadam na Iraq hazikuvamiwa sababu ya utawala wa mabavu au silaha za hatari. Bali sababu halisi ni kuwa Sadam na nchi yake walikataa system ya kuuza mafuta kwa kutumia dola na wakaanza majaribio ya kuuza mafuta kwa kutumia pesa ya Iraq.

Wa america waliogopa kama watamwacha Saddam na Iraq waendelee na utaratibu huo basi nchi nyingine za kiarabu zitawafata Iraq kutumia mfumo huo wa kuuza mafuta bila kutumia dola na itasababisha thamani ya dola kuporomoka na mfumo wa uchumi wa marekani ungeyumba.
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom