DOKEZO Mazao ya chakula yasiuzwe nje ya Nchi, hali ni mbaya sana. Serikali zuieni haraka

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Arovera

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
10,985
28,566
Ukweli kwa sasa ni huu,

Kutokana na dunia kuwa na mvua chache, na ukanda wa Afrika pia kuathiriwa ni vyema sasa mazao yafuatayo yawekewe zuio la kuuzwa nje ya nchi ili kujihakikishia usalama wa chakula na kulinda soko la ndani.

Mchele, mahindi, muhogo, maharagwe, njegere, choroko, mtama mweupe na kadhalika. Mataifa mengi afrika yameweka zuio na mengine yameanza kutangaza hali ya hatari sababu ya njaa.

Mavuno yalikua kidogo na idadi ya watu imeongezeka maradufu. Wakati ambapo waziri wa kilimo anapambana na project za umwagiliaji na bado hatujakomaa kwenye umwagiliaji ili kua na uwezo wa kuvuna mazao misimu yote kwa mwaka tuchukue hatua hizo kwa sasa.

HAKUNA AMANI YA NCHI KAMA CHAKULA HAKITOSHI.
 
Mtatufidia wakulima? Nimelima bila msaada wenu wala wa serikali, nimevuna kwa kulala shambani kwenye baridi wiki nzima halafu unataka nizuiwe kulima. Hivi zinawatosha kweli? Napokea iliyo halali yangu. Ukikinga mwisho wa mwezi mbona sikuzuii?

Bei kwa soko pekee la ndani ni rafiki na mkulima hatoathirika na bei hazitoshuka kwani uhitaji ni mkubwa kuliko uwepo wa chakula
 
Braza nahisi hujaelewa sitaki urafiki na mimi nataka nitoke. Nimepigwa baridi isiyoelezeka aisee. Kila mtu ale kwa urefu na unene wa kamba yake.

Nina mpango wa kubeba mkopo nikalime kabisa. Ila sitaki kupangiwa bei. Ikishuka nijue ni forces of demand and supply and not government intervention.

Kuna mwaka nililimia tembo. Yani hata pole sikupewa. Acha tule acheni wivu.

Mkitaka sana bado kuna mapori mengi tena yanamilikiwa na serikali waambieni wawape
 
Unasema kuna soko la ndani, ila SSH alipotisha tu kufunga mipaka mahindi yaliporomoka ovyo hadi kwenye bei ya kumkata mkulima, bongo soko la ndani halipo na halitoshelezi, wanaonunua msosi sana ni watu wa Dar, wengine wengi wana japo mashamba, hivyo ukifunga mipaka tegemea maporomoko ya bei,

Naungana na SSH, wacha mazao yauzwe tu popote, wakenya ndugu zetu, wakulima wapate pesa nyingi msimu ujao walime zaidi
 
Ukweli kwa sasa ni huu,

Kutokana na dunia kuwa na mvua chache, na ukanda wa Afrika pia kuathiriwa ni vyema sasa mazao yafuatayo yawekewe zuio la kuuzwa nje ya nchi ili kujihakikishia usalama wa chakula na kulinda soko la ndani.

Mchele, mahindi, muhogo, maharagwe, njegere, choroko, mtama mweupe na kadhalika,
Mataifa mengi afrika yameweka zuio na mengine yameanza kutangaza hali ya hatari sababu ya njaa.

Mavuno yalikua kidogo na idadi ya watu imeongezeka maradufu,
Wakati ambapo waziri wa kilimo anapambana na project za umwagiliaji na bado hatujakomaa kwenye umwagiliaji ili kua na uwezo wa kuvuna mazao misimu yote kwa mwaka tuchukue hatua hizo kwa sasa.

HAKUNA AMANI YA NCHI KAMA CHAKULA HAKITOSHI.
Hii ni fursa kwa wakulima kupata pesa. Msimu ujao kalime ili uache kulialia huku
 
Ukweli kwa sasa ni huu,

Kutokana na dunia kuwa na mvua chache, na ukanda wa Afrika pia kuathiriwa ni vyema sasa mazao yafuatayo yawekewe zuio la kuuzwa nje ya nchi ili kujihakikishia usalama wa chakula na kulinda soko la ndani.

Mchele, mahindi, muhogo, maharagwe, njegere, choroko, mtama mweupe na kadhalika. Mataifa mengi afrika yameweka zuio na mengine yameanza kutangaza hali ya hatari sababu ya njaa.

Mavuno yalikua kidogo na idadi ya watu imeongezeka maradufu. Wakati ambapo waziri wa kilimo anapambana na project za umwagiliaji na bado hatujakomaa kwenye umwagiliaji ili kua na uwezo wa kuvuna mazao misimu yote kwa mwaka tuchukue hatua hizo kwa sasa.

HAKUNA AMANI YA NCHI KAMA CHAKULA HAKITOSHI.
Hali ingekuwa mbaya Sasa gunia lisingekuwa linauza elfu 75,000-80,000 mjini

Wewe Toka huko kwenye Mikoa yenu ya majangwa utakufa Rukwa,Ruvuma,Katavi,Kigoma,Mbeya,Songwe Gunia ni 60,000 Vijijini
 
Ukweli kwa sasa ni huu,

Kutokana na dunia kuwa na mvua chache, na ukanda wa Afrika pia kuathiriwa ni vyema sasa mazao yafuatayo yawekewe zuio la kuuzwa nje ya nchi ili kujihakikishia usalama wa chakula na kulinda soko la ndani.

Mchele, mahindi, muhogo, maharagwe, njegere, choroko, mtama mweupe na kadhalika. Mataifa mengi afrika yameweka zuio na mengine yameanza kutangaza hali ya hatari sababu ya njaa.

Mavuno yalikua kidogo na idadi ya watu imeongezeka maradufu. Wakati ambapo waziri wa kilimo anapambana na project za umwagiliaji na bado hatujakomaa kwenye umwagiliaji ili kua na uwezo wa kuvuna mazao misimu yote kwa mwaka tuchukue hatua hizo kwa sasa.

HAKUNA AMANI YA NCHI KAMA CHAKULA HAKITOSHI.
Wenzetu wafe na njaa na sisi tuna chakula? Kama kufa ni wote, kama kupona ni wote.

Binadam gani wewe usiyewajali jirani zako?
 
Uzeni yoote tu, tena mjitahidi kutouza kwenye soko la ndani ili mpate faida pomoni. Mkakarabati hizo nyumba za wazazi wenu.

Uzuri wa wakulima wengi wa TZ, tunaishi nao vijijini huku, tunayajua maisha yao; nadhani watakuwa na uwezo wa kununua chakula nje ya nchi pia!
Acha kukaza shingo,kuna watu wanafanya kilimo biashara. Hao wanaolima kwa ajili ya chakula gunia nne ndani zinamtosha chakula mpaka msimu mwingine wa kulima. Unadhan watu wanalima ekari 20 kwa ajili ya chakula cha familia?
 
Back
Top Bottom