Mayalla tupo pamoja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mayalla tupo pamoja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ringo Edmund, May 19, 2012.

 1. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Naangalia star tv tuongee asubuhi naona pascal mayalla amenikuna kweli kwa sababu kila siku nilikuwa sipati usingizi kwa sababu nilikuwa namfikiria rais kuwa ana mamlaka ya kuteua mbunge na kumpa uwaziri hapohapo?
  Jibu nililopata kuwa wizara bado hazijapata mawaziri ila zimepata viongozi na katiba haiwatambui kwa hiyo kazi zote wanazofanya kwa niaba ya waziri ni batili.
  Wiliam mgimwa haruhusiwi kufanya kazi yoyote kwa niaba ya waziri wa fedha wa tanzania.

  Pascall big up simamia ukweli na taifa litakukumbuka baadae.
   
 2. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Amefafanua vizuri sana huyu Pasco. Pia na Ansbert Ngurumo naye ameeleweka.
   
 3. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Amenifurahisha ngurumo alipoambiwa na mayalla kuwa rais ana mazuri ya kusifiwa majibu yake hana sababu ya kumsifia rais kwa kazi aliyoomba mwenyewe ila atamlaumu kwa kazi aliyiomba na kushindwa kuifanya.
   
 4. K

  Kwakanga Member

  #4
  May 19, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 41
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Mkuu Ringo Edmund, Mh. William Mgimwa ni mbunge wa jimbo la Karenga- Iringa si mbunge wa kuteuliwa hivyo alishaapa kiapo chake cha ubunge siku nyingi, hivyo anauhalali pande zote kuutumikia uwaziri wa fedha mkuu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. maulaga

  maulaga JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 472
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Upo sahihi kabisa mkuu.
   
 6. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  sorry, nilikuwa namzungumzia sospeter muhongo kaka.[/QUOTE]Sasa huyu jamaa mbona leo alikuwa pale Tanesco makao makuu kujitambulisha kwa menejiment ya tanesco na wafanyakazi wake?
   
 7. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  jamani mimi naitwa RINGO EDMUND na sina id nyingine na nimeshawaambia kuwa nimeshindwa kutumia jina la bandia kwa sababu toka nikiwa mdogo moja huwa naiiita moja hata kama mtu hataki.
  nakushukuru sana kaka MATOLA kwa kutolea ufafanuzi post yangu.mbarikiwe.
   
 8. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Sasa huyu jamaa mbona leo alikuwa pale Tanesco makao makuu kujitambulisha kwa menejiment ya tanesco na wafanyakazi wake?[/QUOTE]
  kaka nielewe huyu jamaa si waziri kwa katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania na hapaswi kulipwa mshahara wa waziri mpaka atakapokuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania.
   
 9. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #9
  May 19, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hapa tunachotaka ni kuchangia hoja! Hilo la nani ni nani halina mashiko. Swala ni mtu na maoni yake! Kuna watu wapo kwaajili ya kudivert mada na tusipokuwa makini tutaingia porini!
   
 10. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #10
  May 19, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,275
  Trophy Points: 280
  Huogopi tena Mambumbu kukwambia umejiuliza mwenyewe kwenye red hapo halafu ukaja kujijibu mwenyewe huku chini!!??.....teh!teh! teh! teh! teh! teh!
   
 11. engwe1980

  engwe1980 Member

  #11
  May 19, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ukiwa muongo usiwe msahaulifu!
   
 12. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #12
  May 19, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hili tatizo la reply with quote kwa nyie mnaotumia simu ndio naona linawachanganya.
  Ringo Edmund yuko sahii sema kamchina kake kanamzingua kureply with quote, na watumiaji wenzie wa cm nao wanazugika!
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  May 19, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Mkuu Ringo Edmund, Mh. William Mgimwa ni mbunge wa jimbo la Karenga- Iringa si mbunge wa kuteuliwa hivyo alishaapa kiapo chake cha ubunge siku nyingi, hivyo anauhalali pande zote kuutumikia uwaziri wa fedha mkuu[/QUOTE]

  Kikwete ni mbumbumbu wa sheria. Anakidhalilisha UDOM
   
 14. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #14
  May 19, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kuna watu wana vijembe humu ndani, Bi Mkubwa Hadija Kopa cha mtoto!
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  May 19, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Pacso ametoa ufafanuzi mzuri lakini bado Ngurumo kamfunika kwa kitu kimoja. 'utetezi wake wa jinsi alivyomsifu Kikwete jf lakini watu wakampiga chini.

  Ngurumo akuuma maneno kwa kutoboa kwamba kwa maoni yake Kikwete hajafanya zuri lolote. teh teh teh teh
   
 16. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #16
  May 19, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Here have great thinkers.
  Tuko pamoja mnaonielewa lakini kwa wasioelewa ni watanzania wenzetu na katika mabadiliko inabidi tuwa bebe.
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Aug 9, 2016
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,531
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ringo Edmund, huwezi amini hili bandiko lako la 2012 ndio nimeliona leo kibahati tuu kufuatia bandiko jingine fulani.
  Nadhani hukunielewa vizuri, kama ili kwa mbunge, baada ya kuchaguliwa huwa ni mbunge mteule hadi atakapoapishwa ndipo anakuwa na mamlaka ya kufanya kazi za kibunge!. Vivyo hivyo kwa mawaziri, wakiishateuliwa wanakuwa ni mawaziri wateule, hawawezi kufanya majukumu rasmi ya uwaziri kabla hawajaapishwa!. Kutokuapishwa hakumzuii kufanya lolote ila anakuwa sio rasmi!.

  Paskali
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Aug 9, 2016
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,531
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kaa la Moto, ni kweli tulitofautiana na Ansbert kwenye eneo hili, mimi nilisisitiza Kikwete apongezwe kwa mazuri yake na kulaumiwa kwa mabaya yake, nikasisitiza haiwezekani iwe ni kulaumu tuu, mwenzangu akadai hayo mazuri ni katika kutimiza wajibu wake!, hoja yangu mimi ni kuwa na shukrani, hata kama ni kutimiza wajibu wake, kama ametimiza vizuri anastahili pongezi.

  Paskali
   
 19. Papushikashi

  Papushikashi JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2016
  Joined: Feb 28, 2016
  Messages: 4,800
  Likes Received: 4,086
  Trophy Points: 280
  Mkuu Jana wakati unamuulizia Kailima swali kuhusu vituo ambavyo vilivamiwa wakati wanahesabau kura naona uliegemea upande mmoja kwa sababu hata ccm nao walikuwa wanahesabau lakini wao hawakuvamiwa, halafu wewe ukatoa conclusion ya moja kwa moja kwamba eti wale wanaosema wana Rais wao wa mioyo waache kwa sababu uchaguzi ulikuwa huru na haki..... Kwa kweli hapa hukutenda haki
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Aug 9, 2016
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,531
  Trophy Points: 280
  Mkuu Edi Ringo, mimi na Ngurrumo letu moja kwenye kulaumu kule watawala wanaposhindwa, ila pia nikasisitiza wanapofanya vizuri, tuwapongeze!, hata katika ngazi ya familia, kuna wajibu tunatimiza na tunapeanza sio tuu asante hata tujizawadi!. Kila mtu anastahili pongezi pale anapofanya vizuri hata kama jambo hilo ni wajibu wake!.

  Paskali
   
Loading...