Mayai na Michele ya Plastiki

lucky lefty

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
496
500
Kumekuwa na wimbi la uingizwaji na utengenezwaji wa mayai na michele feki nchini Tanzania na Afrika kiujumla.
Nachotaka kufahamu kwa wenzetu watanzania ambao wameajiriwa kwenye hivyo viwanda vya uchochoroni vinavyotengeneza hizi bidhaa, implications zao kisheria zinakuaje. Maana kwa hali tata ya sasa ya ajira nchini sidhani kama mtu atakataa ajira yoyote itayojitokeza, sasa kisheria nao ni wataajibishwa au ni wamiliki tu ambao wataajibishwa, naomba kufahamu hilo.

Pili ni nini madhara ya kutumia hizo bidhaa kiafya kwa mtu ambaye hajajua au akiwa tayari keshatumia.

\
 

Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
42,861
2,000
Mmmh mayai tena?? Daaah

*Consumers' Tip Mchele Fake*
Unaponunua mchele tafadhali chukua kiasi kidogo tia katika kikombe kisha jaza maji, tingisha mchanganyiko wa maji na mchele uone kama mchele una elea ama uko chini ya maji.

Kama unaelea basi huo umetengenezwa kwa plastic na haufai kwa matumizi ya binadamu.

Kuwa makini mtumie na mwengine kunusuru afya zao.

Piga simu hii 022 245 0512 TFDA kuwajulisha umeununua wapi au polisi ili wahusika wakamatwe.

Kwapamoja tuzilinde afya zetu..
 

lucky lefty

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
496
500
Mmmh mayai tena?? Daaah

*Consumers' Tip Mchele Fake*
Unaponunua mchele tafadhali chukua kiasi kidogo tia katika kikombe kisha jaza maji, tingisha mchanganyiko wa maji na mchele uone kama mchele una elea ama uko chini ya maji.

Kama unaelea basi huo umetengenezwa kwa plastic na haufai kwa matumizi ya binadamu.

Kuwa makini mtumie na mwengine kunusuru afya zao.

Piga simu hii 022 245 0512 TFDA kuwajulisha umeununua wapi au polisi ili wahusika wakamatwe.

Kwapamoja tuzilinde afya zetu..
Yani hawa watu wanataka kutumaliza huku Afrika sio watu salama kabisa
 

Kanye2016

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
2,080
2,000
Yani watanzania nao wanashiriki kuingiza na kusambaza hizi bidhaa hatari.
 

Kanye2016

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
2,080
2,000
Mimi ni mwendo wa Ugali na Uono kwisha habari, ishu za michele nimepunguza sana tena siku hizi hata michele ya kawaida wanatengeneza tofauti na mwanzo ilikuwa ya Basmat tu
 

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
9,633
2,000
Nchi yetu haingizi mayai kutoka nje....
Ni vyema ukaweka na ushahidi wa statement yako. Yawezekana kuna viwanda ndani ya nchi tayari vya kutengeneza hayo mayai. Kwa hiyo huyo dada kwenye video haukubaliani nae?

Phonex sio salama kabisa na bila ubabe wa Eagle hali ingekuwa mbaya sana.
 

lucky lefty

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
496
500
Ila twende mbele, turudi nyuma, je mamlaka ziko wapi?
Mamlaka zimelala kabisa, walitakiwa wawe wanafanya uchunguzi unapotokea huo mchele na hayo mayai, Kupitia hizo video wangefanya followup kwa wakwanza aliye upload aseme alipouziwa michele ya aina hyo ili wakamatwe, na pia kama pangekuwa na reward ya kutoa info sehemu inapozalishwa hapa TZ pia ingesaidia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom