Chalamila asema ataka Dar iwe ya mfano katika urejeleshaji taka

kevylameck

Member
Nov 3, 2013
18
19
1DCB0BC5-2AA0-4A45-959D-125BAFB87AC0.jpeg


✍🏽 Kevin Lameck.

Kulingana na ripoti Ya U.S Recycling Economic Information (REI), San Francisco - Marekani ni jiji la kijani kibichi hasa, linatajwa kama kinara kwa urejeshaji wa taka (recycling), kwa zaidi ya asilimia 80 ya taka zake.

Wanafanyaje? Kwa kushikamana na mipango madhubuti ya kuchakata taka na sera ya kulipa fedha kadri wakazi wake wanavyotupa taka zisizoweza kutumika tena, huwafanya wananchi wawe na ufahamu zaidi wa mazingira hasa kuhusu bidhaa wanazonunua katika kuepuka kulipishwa fedha zaidi za taka.

Majiji mengine yanayofanya vizuri kwenye urejeshaji wa takataka ni pamoja na Curitiba - Brazil, iliyofanikiwa kwa asilimia 70 pamoja na Vancouver-Canada waliofanikiwa kwa asilimia 60 wakiwa na lengo la kufikia asilimia 100 ifikapo mwaka 2040.

Sio siri kuwa kuchakata taka kunanufaisha mazingira, lakini pia kunakuza uchumi. Kwa kutenganisha taka zinazoweza kutumika tena kama karatasi, nguo chakavu, glasi, plastiki, aluminium na mabaki ya vyakula na taka za elektroniki, watumiaji wanaweza kusaidia kuunda kijani kibichi kwenye majiji makubwa duniani.

Urejelezaji wa taka (recycling) ni mchakato wa kutibu taka kwa lengo la kuokoa malighafi zilizopo ndani ya taka na kuzirejesha kwenye matumizi ya kiuchumi.

Vifaa vya kielektroniki kama simu na kompyuta huweza kurejelezwa na kutumika tena katika kutengeneza matofali, saruji na vyombo vipya vya glasi huku taka za kaboni kama maganda ya matunda na mbogamboga zikitumika kutengeneza mbolea na karatasi zikirejelezwa na kutumika kama makasha ya mayai na vifungashio vya bidhaa mbalimbali.

Kadhalika mabaki ya chakula pia hutumika kuzalisha funza ambao wana protini nyingi kuliko dagaa na ambao hutumika kama chakula cha Kuku, nguruwe na samaki.

Ripoti ya benki ya dunia kuhusu maendeleo ya miji, inaonesha kuwa Afrika huzalisha tani Milioni 70 za taka kwa mwaka.

Wakati huu ambapo ongezeko la watu wanaohamia mjini linaongezeka kwa kiasi kikubwa, Benki ya dunia inasema kufikia mwaka 2025, uzalishaji wa taka huenda ukafikia tani milioni 160 kwa mwaka.

Jiji la Dar es salaam lenyewe linakadiriwa kuzalisha zaidi ya tani 4,252 za taka kwa siku moja. Kati yake ni asilimia 50 tu ndizo zinazopokelewa kwenye maeneo maalumu, nyingine zikisalia na kutupwa kwenye mitaro, maeneo ya wazi na barabarani.


Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila anaiona fursa kubwa kwenye wingi wa taka hizo na tayari alisafiri mara moja kwenda kwenye jiji la Bursan nchini Korea Kusini kujifunza namna wenzetu walivyofanikiwa kwenye urejelezaji wa taka na kuzifungamanisha na fursa kwa vijana wa rika mbalimbali.

Chalamila anasema malengo yake ni kuitumia Dar es salaam kama mfano kwa majiji mengine ya Tanzania na Afrika Mashariki.


Mkuu huyo wa mkoa anasema urejelezaji wa taka na mifumo mizuri ya kushughulika na majitaka utasaidia kuongeza ajira, kuongeza viwanda vidogo vidogo, kuongeza teknolojia mpya pamoja na kipato ambacho kimekuwa kikipotea ikiwa ni pamoja na kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa.

Tafiti zinasema ni rahisi kutengeneza bidhaa kutoka nyenzo zilizorejelezwa kwani bidhaa kama ya aluminium iliyorejelezwa inaweza kuandaliwa tena na kuuzwa kwa bei nusu,kutokana na kuhitajika nishati kidogo kuchakata aluminium iliyorejelezwa kuliko kutumia aluminium mbichi ya kiwandani inayotumika kwa mara ya kwanza.

Urejelezaji pia huepusha gharama ya utupaji wa taka kwenye dampo na vichomaji kwani baada ya kuanza kwa urejelezaji, dampo chache zitahitajika na ardhi zaidi zilizokuwa zimetengwa kuhifadhi taka huweza kutumika kiuchumi.

Aidha Mapato ni sehemu nyingine aliyoiona Chalamila kwani urejelezaji huimarisha tasnia ya uchakataji na hivyo kutengeneza nafasi mpya za kazi kwenye viwanda vidogo vitakavyoundwa kama viwanda vya chuma, karatasi, glasi pamoja na ajira kwenye vituo vya ukusanyaji taka na hata warejeshaji husika.

Utafiri wa U.S Recycling unaonesha kuwa nguvukazi ya kuchakata na kutumia tena malighafi zinazotokana na taka imekuwa kubwa zaidi kwenye mataifa mengi zaidi ya nguvukazi inayotumika kwenye uchimbaji wa madini na usimamizi wa taka zisizorejelezwa.Mashirika yanayorejeleza taka huzalisha takribani dola bilioni 240 kwenye mapato ya kila mwaka.

Huko Carolina kusini pekee, zaidi ya wafanyakazi 15,000 na dola za Marekani milioni 69 za ushuru hutokana na uchakataji wa taka huku Carlifonia urejelezaji wa taka ukiahiri watu 85,000.
 
Nikakumbuka ule mradi hewa wa kupulizia dawa enzi za makonda Mwenda zake akashtukia dili.
Tusubirie tuone kama itazaa matunda.
Btw angeanza na moango wa kukusanya na kuzoa taka kwanza .
Kila mkazi au mfanyabiashara kupigwa faini pindi taka zinapotupwa au kukusanywa kwemye makazi au eneo la.biashara yake.
Sidhani wangwruhusu wauza miwa na kuchoma mahindi waache taka kwenya maeneo yao.
Nakazia taka zi I usanywe na kusimbwa muda huo huo sio kulundija taka eneo pembezoni mwa marabara halafu zikae hapo wiki moja bila kuzolewa.
Mitaro wanaisafisha wanalundika taka pembezoni mwa barabara kisha zinarudi mle mle mitaroni.
Barabara hazifagiliwi hata mistari ya kuonyesha mwisho wa barabara hakuna michanga ndo inaonyesha sehemu ya lami ikoishia.
Angeanza na mambo madogo madogo ndo afikirie haya ya Korea
 
Back
Top Bottom