Maxmalipo, Samsung, hamjawatendea haki Tecno

Maxmalipo, Samsung, hamjawatendea haki Tecno

Hapa ishu sio ubora wa simu, ishu hapa ni maadili ya matangazo ya biashara, hutakiwi kuonesha, kutaja au kuandika jina la mpinzani wako kibiashara unapotengeneza tangazo iwe ya picha (video) au sauti au printed media.
Nadhani Tecno wanaweza kuchukua hatua za kisheria.
 
Wala usijali mkuu kimpe hii siyo hapa tu hapo zamani za miaka ya 80 magari ya kijapani yalipigwa vita sana kwenye matangazo ya biashara huko Marekani mimi niliona matangazo ya wazi kabisa yanasema don't buy Japannese.,lakini miaka ilivyozidi kwenda pumba zilijulikana ni zipi na ngano ni ipi magari ya kijapani soko lake lilikua kiasi cha baadhi ya viwanda vya magari ya kimarekani kufunga matawi yao na kuuzwa kwa makampuni ya nje.
Tecno simu zao ziliingia hapa nchini watu wakadhani ni michina ile iliyokuwepo wakati rule lakini mda ulivyozidi kwenda ziliendelea kuzoeleka sasa hivi tunapoyaongea haya simu za tecno zimekamata asilimia kubwa katika soko la simu kuna baadhi ya brand kama Siemens,motorola n.k zimepotezwa kabisa na myama Tecno, Samsung wajiandae kunyolewa kiwembe kikali kinakaribia.

Siemens na motorola hawajapotea kwa sababu ya tecno, siemens ana deal na vitu vingine motorola aliinunua google na sasa hivi kaiuza kwa lenovo
 
Usiendeshwe kihisia na watu wengine wote hatuwez kumiliki iphone au samsung hata kama ni matajiri.. Fanya kile kinachoufurahisha moyo wako sio mioyo ya wengine..
 
Kimfaacho ntu chake jamani mimi nina Tecno yangu ya line tatu wala sina shida yoyote. Tigo, airlel na voda zote kwa pamoja na zote zina pesa kibao!
 
Yani hio techno unakua unasikia raha kuitumia ukiwa alone ila ukiwa na washkaj afu wakakuuliza hio ni simu gani unatumia unaanza kujibu ooh hii techno afu usiione hivi ina speed kali, ram kubwa, camera ya kutosha yan lazima utoe maelezo ya kutosha wkt ukitoa Samsung au iPhone huna haja ya kujieleza, hahah

Mkuu hii post yako imenifanya nicheke peke yangu kama chizi

Ulichosema kina ukweli asilimia kubwa sababu watu wameaminishwa tecno ni vimeo, sasa ili kuondoa hiyo dhana watumiaji wengi wa tecno ukiwauliza unatumia simu gani majibu huwa marefu kweli kujaribu kuonyesha ipo vizuri kuliko inavyo semwa
 
Ubora wa Tecno ni sawa sawa au hata zaidi ya Samsung, ila tatizo letu wabongo tunameza sana. Kamata Phantom Z ndio utajua what I mean here. Samsung ni very expensive for nothing.

Mkuu ongea kwa hoja na ushahidi vinginevyo hizi ni kelele!! Weka specs za kila simu hapa.
 
Samsung ni world brand, tecno imetengenezwa kwa ajili ya watu wasiojiweza

Upo sahihi kabisa, Tecno ni kwa ajili ya watu wa chini kabisa...ubora wake ni mdogo sana...afadhali hata ya Huawei kidogo
 
Wabongo bhana, mtu kapanga, anapanda daladala kila siku, mlo mara mbili au moja, kijijini kwenu hata bati umeshindwa kuwanunulia wazee wako, chumba chenyewe ulichopanga hata marafiki kuwapeleka unaona aibu, leo hii unasema Tecno is inferior, too low, haina hadhi. Hizi tabia za kimaskini tuziache we kama unaona haikufai n wewe lakini usikashifu wengine wakati unaishi kwa kujionyesha tu.

Note: walengwa wanajijua sio wote.


Utawaweza wa tz kwa mbwembwe kaka
 
Tecno itasubiri sana kwa Samsung. Ni sawa na kulimganisha kiwango cha Ngasa na Messi.
 
economics inasema hivi, A giffen good occurs when a rise in price causes higher demand because the income effect outweighs the substitution effect. Suppose you have a very low income and eat two basic food stuffs rice and meat. Meat is a luxury and is much more expensive than rice.kwenye rice weka tecno kwenye meat weka samsung.Ukiwa mchumi utanielewa tu
 
Samsung ni world brand, tecno imetengenezwa kwa ajili ya watu wasiojiweza

Kwani wewe unajiweza! Simu sio kipimo cha maendeleo as most of people think rafiki. Halafu uko too general maana huyo samsung ana simu hadi za elfu 35,000. Maendeleo kwangu mimi naona yanaanzia kwenye fikra, tunatawaliwa kifikra sasa na ukombozi wa fikra ndio utatutoa hapa tulipo.
 
Mkuu hii post yako imenifanya nicheke peke yangu kama chizi

Ulichosema kina ukweli asilimia kubwa sababu watu wameaminishwa tecno ni vimeo, sasa ili kuondoa hiyo dhana watumiaji wengi wa tecno ukiwauliza unatumia simu gani majibu huwa marefu kweli kujaribu kuonyesha ipo vizuri kuliko inavyo semwa

Hahaha asante sana mkuu kumbe na wewe umeshakutana na hivo vioja, Tatizo Team Techno humu Jf itajua tunaponda tu simu zao kumbe ni kweli mkuu.
 
Usiendeshwe kihisia na watu wengine wote hatuwez kumiliki iphone au samsung hata kama ni matajiri.. Fanya kile kinachoufurahisha moyo wako sio mioyo ya wengine..

Nashukuru sana mkuu umeamua kusema ukweli Tatizo hapa kinachotusumbua wengi ni uwezo mdogo wa kifedha tulionao ndo mana tuna kimbilia Techno
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom