Maximo, Coutinho out Yanga, Pluijm na Tambwe ndani

Maximo, Coutinho out Yanga, Pluijm na Tambwe ndani

*** you *** you *** you yanga.....mimi ni shabiki wa yanga sitashabikia tena yanga teeeeeeeeenaaaaaaaaaa,nahamia azam fc rasmi sasa,am doneeeee

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Jitahidi usioe maisha yako unaweza kuolewa kwa hasirahizi
 
Kwa mashabiki wa YANGA,
Hizi taarifa ni dhahili ingawa kuna mvutano mkubwa ukiendelea kikaoni kwa sasa.
Na tayari kocha wa zamani wa yanga Pluijm ameshatua Dar kwa ajiri ya kumalizana na Yanga endapo watafikia makubaliano.
Pia kuna taarifa kwamba kuna viongozi wa yanga ambao hawamtaki Maximo na waliitumia nafasi ya juzi mtani jembe ili kumfukuza Maximo kwani waliwashinikiza wachezaji wacheze chini ya kiwango.
Kuhusu Tambwe inasemekana wamefikia pazuri na pengine mpaka saa6 usiku mambo yote yakawa wazi.
Ntaendelea kuwapenyezea nyepesi nyepesi mpaka saa6 usiku.
................................................................................................
updates.:AMISI TAMBWE ASAINI MWAKA1 YANGA USIKU HUU ILI KUWAHI DIRISHA DOGO KABLA HALIJAFUNGWA.

................................................................................................
Updates:ITC yasitisha mkataba wa Emerson jangwani,TAMBWE achukua nafasi yake.

.....................................
Updates:
Maximo atupiwa virago,
Babu Pluijm na Mkwasa wakabidhiwa timu.

..........................
Updates:
Couitinho apewa siku90 kuonesha uwezo wake,vinginevyo nayeye atatupiwa virago.

Kua kocha wa mpira wa miguu tanzania hasa kwa simba,yanga ni shida.
 
PLUIJM ATUA JIJINI DAR ES ES SALAAM
attachment.php

Pluijm akiongea jambo na baadhi ya watu waliokuja kumpokea

Mholanzi Hans van der Pluijm amewasili Saa 8:30 usiku wa kuamkia leo kwa ndege ya Shirika la Ethiopia tayari kurudi kazini Yanga SC.

Baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam, Pluijm alisema amefurahi kurudi Yanga SC.

"Nimefanya mazungumzo na Yanga, natarajia kutasaini mkataba na kwenda kupumzika kwanza,"alisema.

Wakati huo huo Inarepotiwa kwamba Kocha Mbrazil Marcio Maximo ameondoka ndani ya klabu ya Yanga.

Maximo anaondoka Yanga baada ya uongozi wa klabu hiyo kukubaliana naye kuvunja mkataba baada ya kushindwa kuelewana juu ya jinsi ya kuiendesha klabu hiyo kwenye masuala ya ufundi.

Yanga ilishikilia msimamo wa kumuajiri Mkurugenzi wa ufundi ambaye alipangwa kuwa Charles Boniface Mkwasa jambo ambalo Maximo hakukubaliana nalo.

maximo

Nafasi ya Maximo sasa itachukuliwa na Mholanzi Hans Van Der Pluijm ambaye aliifundisha timu hiyo kwa nusu msimu baada ya kufukuzwa kwa Mholanzi mwenzie Ernst Brandts.

Tukio hili linaendeleza historia ya Yanga kufukuza makocha baada ya kufungwa na Simba kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe baada ya kufukuzwa kwa Ernst Brandts msimu uliopita kufuatia kipigo cha 3-1 mbele ya Simba iliyokuwa inaongozwa na Dravko logarusic.
 

Attachments

  • pj.jpg
    pj.jpg
    44.2 KB · Views: 2,001
Tatizo kubwa la Maximo tangu ameanza kufunza haonyeshi welekeo wa soka la Yanga ni lipi?
 
Mi nilisha sema kuwa huyo Maximo amekuja kutafuta aibu tu na kupoteza heshima yake aliyondoka nayo.Hizi timu za yanga na simba kwa sarakasi tu ni kama magamba, wao kushindwa ni msamiti lazima kinuke tu!!
 
du watu wako fasta sana..uckute nae alikua amekaa hko anatuma maombi ya kazi wee hta hapati...ss kama zali anashangaa anapigiwa cmu na vibopa wa yanga..hzi timu zetu akiweza kuzishika akili zao utakula sana hela yani..Maximo aendoke vizur tu kwan unaweza kuta akarudishwa baadae...kama ilivokua kwa phiri..
 
*** you *** you *** you yanga.....mimi ni shabiki wa yanga sitashabikia tena yanga teeeeeeeeenaaaaaaaaaa,nahamia azam fc rasmi sasa,am doneeeee

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Kuwa mpole ndugu, hauwezi hama! Hiyo ndo timu nafsi yako iliichagua bila wewe kujua.
 
Ni nani wamefanya makubwa Simba na Yanga kati ya kina Tabu Mangala na hawa wasomi wa leo?
Matola umezungumza vizuri hapo sema tatizo hawa washabiki wengi wa soka kwa sasa ni zao la millenium.. Hawaijui historia hata kidogo.. Vilabu hivi vilikuwa vinaongozwa na wazee ambao hawakuwa na elimu lakini walikuwa na vipaji vya hali ya juu vya kuongoza soka kwa busara na hekima.. Viongozi ambao wali-sacrifice muda na pesa zao kuhakikisha vilabu vya simba & yanga vinakuwa na wachezaji wenye vipaji na waliojua kuucheza mpira uwanjani.. Wazee ambao waliunda vikosi b vya timu zao kwa ajili ya kuwaanda wachezaji wenye umri mdogo kuingia kwenye timu za wakubwa..

Leo wameingia viongozi "wasomi" ambao baada ya kuona mpira unalipa kibiashara wameamua kujali maslahi yao zaidi kuliko ya timu.. Leo kiongozi haogopi kuiingiza timu yake kwenye pambano dhidi ya mtani wake hata kama timu haina maandalizi mradi tu aingize pesa mfukoni.. Yaani viongozi wa simba na yanga wakishirikiana na tff wanakaa kama kamati na kuangalia jinsi gani wanavyoweza kuchuma pesa ili wajitajirishe wao.. Hawajali feelings za wapenzi na mashabiki wa vilabu vyao as long as wao wanapata pesa..
 
Last edited by a moderator:
Ningekua wazili wa michezo ningefanya kila juhudi kuhakikisha nazifuta yanga & Simba.

Na kabla hujaanza kutekeleza hiyo ilani yako ..... ungekua umeishatimuliwa huo uwaziri wako na una kesi ya maadili mahakani ikichunguzwa na takukuru kwa miaka mitatu...baada ya hapo unapoteza ubunge hadi uanachama na kutoweka katika ramani ya tanzania.
 
Back
Top Bottom