DAKA MTUMBA
JF-Expert Member
- Aug 4, 2014
- 1,288
- 805
Kwa mashabiki wa YANGA,
Hizi taarifa ni dhahili ingawa kuna mvutano mkubwa ukiendelea kikaoni kwa sasa.
Na tayari kocha wa zamani wa yanga Pluijm ameshatua Dar kwa ajiri ya kumalizana na Yanga endapo watafikia makubaliano.
Pia kuna taarifa kwamba kuna viongozi wa yanga ambao hawamtaki Maximo na waliitumia nafasi ya juzi mtani jembe ili kumfukuza Maximo kwani waliwashinikiza wachezaji wacheze chini ya kiwango.
Kuhusu Tambwe inasemekana wamefikia pazuri na pengine mpaka saa6 usiku mambo yote yakawa wazi.
Ntaendelea kuwapenyezea nyepesi nyepesi mpaka saa6 usiku.
................................................................................................
updates.:AMISI TAMBWE ASAINI MWAKA1 YANGA USIKU HUU ILI KUWAHI DIRISHA DOGO KABLA HALIJAFUNGWA.
................................................................................................
Updates:ITC yasitisha mkataba wa Emerson jangwani,TAMBWE achukua nafasi yake.
.....................................
Updates:
Maximo atupiwa virago,
Babu Pluijm na Mkwasa wakabidhiwa timu.
..........................
Updates:
Couitinho apewa siku90 kuonesha uwezo wake,vinginevyo nayeye atatupiwa virago.

PLUIJM ATUA JIJINI DAR ES ES SALAAM
![]()
Pluijm akiongea jambo na baadhi ya watu waliokuja kumpokea
Mholanzi Hans van der Pluijm amewasili Saa 8:30 usiku wa kuamkia leo kwa ndege ya Shirika la Ethiopia tayari kurudi kazini Yanga SC.
Baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam, Pluijm alisema amefurahi kurudi Yanga SC.
"Nimefanya mazungumzo na Yanga, natarajia kutasaini mkataba na kwenda kupumzika kwanza,"alisema.
Wakati huo huo Inarepotiwa kwamba Kocha Mbrazil Marcio Maximo ameondoka ndani ya klabu ya Yanga.
Maximo anaondoka Yanga baada ya uongozi wa klabu hiyo kukubaliana naye kuvunja mkataba baada ya kushindwa kuelewana juu ya jinsi ya kuiendesha klabu hiyo kwenye masuala ya ufundi.
Yanga ilishikilia msimamo wa kumuajiri Mkurugenzi wa ufundi ambaye alipangwa kuwa Charles Boniface Mkwasa jambo ambalo Maximo hakukubaliana nalo.
maximo
Nafasi ya Maximo sasa itachukuliwa na Mholanzi Hans Van Der Pluijm ambaye aliifundisha timu hiyo kwa nusu msimu baada ya kufukuzwa kwa Mholanzi mwenzie Ernst Brandts.
Tukio hili linaendeleza historia ya Yanga kufukuza makocha baada ya kufungwa na Simba kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe baada ya kufukuzwa kwa Ernst Brandts msimu uliopita kufuatia kipigo cha 3-1 mbele ya Simba iliyokuwa inaongozwa na Dravko logarusic.