Maxence Melo (Mkurugenzi Mkuu wa JamiiForums) apata ajali mbaya Maeneo ya Nzega

Status
Not open for further replies.

AshaDii

Platinum Member
Apr 16, 2011
16,190
18,080
Wana Jf,

Nina habari za kusikitisha za Maxence Melo na ndugu yake Chrispine Ndyamukama wamepata ajali mbaya ya gari katika barabara kuu iendayo Mwanza kilometa chache kutoka Nzega mjini.

Ndugu zak wamesema hali ya Maxence kwa sasa si mbaya sana na walikimbizwa katika hospitali ya Rufani ya Bugando kwa matibabu na uchunguzi zaidi.Pamoja na Maxence alikuwapo ndugu yake mmoja ambaye naye amejeruhiwa vibaya na wote wamekimbizwa Bugando.

Maxence na mwenzake walikuwa njiani kuelekea mkoani Kagera na gari walilokua wakisafiria (pichani) limeharibika vibaya.

Mwenyezi Mungu awawekee wepesi wa kupata nafuu haraka.

Asanteni.

AJALI.jpg

Mac.jpg

IMG-20130520-WA0028.jpg



========== Update ==========

Maxence anaendelea vizuri kabisa pamoja na ndugu yake ameendelea kupata matibabu hospitali ya Bugando. Taratibu za usafiri zinafanywa za kurudi kesho Dar es Salaam. Habari zaidi zitapatikana akisharejea.

Maxence anaendelea kawaida Fidel. So far getting better. Bado ana maumivu baadhi ya maeneo mwilini na kwa kiasi fulani bado kavimba upande wa usoni. Ndugu yake pia anaendelea vema. Hapa dawa iliyobaki ni time. With time Inshaallah watapona na kurudi hali zao.

==================
Latest Updates
==================

Naomba nitoe update zaidi..

Maxence kwa kiasi kikubwa amekuwa hayupo hewani kwa simu zake zote. Hii imefanya kuwe maswali toka kwa baadhi ya wadau kuhusu ajali yenyewe na maendeleo yao ki afya.
Naomba niwasilishe kuwa wote Maxence na Chrispine wanaendelea vizuri, Maxence more recovered thou kuliko aliyekuwa kavunjika mkono.
Baada ya vipimo Muhimbili, ilibainika Chrispine Muganyizi alivunjika mfupa wa mkono (kati ya kiwiko na bega) na madaktari walimpatia tiba iliyostahili na sasa ana P.O.P. Maxence alikutwa kapata uvimbe katika sehemu ya ubongo kuvimba kiasi lakini alihakikishiwa atakaa sawa kadiri siku zinavyokwenda.

Max ameahidi atakapokuwa sawa kabisa kuja kutoa ufafanuzi wa moja kwa moja na kutoa taarifa ya namna ajali hiyo mbaya ilivyotokea.Kwa kifupi ni kuwa 'sterling rod' ya mbele (chuma kinachoshikilia tairi za gari) ilikatika, upande wa dereva. Kwa sasa Maxence ameeleza na kutoa shukrani za dhati kwa wote waliokuwa nae bega kwa bega toka tukio hilo hadi sasa.

Katoa shukrani kwa Hussein Bashe na team yake yote pamoja na Polisi wa Nzega kwa msaada wao walipopata ajali katika eneo la tukio, anatoa Special thanks kwa madaktari wa Muhimimbili kwa huduma ya uhakika na ya haraka waliyowapatia regardless kuwa ilikuwa ni usiku na siku ya Jumapili.

Anatoa Shukrani kwa Wana JF wote wa Mwanza pia ndugu na Jamaa, anatoa shukrani kwa familia, ndugu na jamaa wote waliokuwa karibu wakati huu wa matatizo.Na pia kakiri kupata salamu zenu za pole kwenye thread hii, kwamba wameguswa na imekuwa faraja na kutia moyo; hivyo anaelekeza shukrani pia kwa members wote wa JF. Pamoja Saana.
 
Too bad!
Wanaendeleaje AshaDii?
Tunawaombea wapone haraka iwezekanavyo na kurudi kazini.
Sala za memberz wote zinaelekezwa huko kwa sasa.
Wanajf, huu ndio wakati wa kushikamana zaidi na kufuta tofauti zetu, tuweke juhudi zetu ktk kumtakia afya njema @Maxence.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom