Maxence (baada ya ajali ya gari): Ahsante Mungu, ahsante watanzania!

Status
Not open for further replies.
Pole sana Maxence itabidi niwe natembelea majukwaa mengine maana nasikia hili kwa mara ya kwanza. Namshukuru Mungu kwa wema wake kwako. Ugua pole na Mungu akusaidie ktk yote wewe pamoja na mdogo wako
 
Hii thread tangu imewekwa naifuatilia. Naona wadau wametoa pole nyingi sana, nikiwemo mimi.

Lakini najiuliza hivi pole is the best we can do to a person who created JamiiForums anapopatwa na tatizo kubwa kama hili?

Guys, we can do more than empty words. Nilishashambuliwa earlier kwa kusema hivi ndio maana nimejaribu kukaa kimya may be mtu mwingine atasema lakini naona masaa yanazidi kwenda na zinamwagika pole za maneno tu.

Pole ni nzuri lakini mdau gari lake mmeliona hapo. Je, tunaweza kufanya pole ya vitendo, ambayo itamuwezesha kupata a car similar to that? Au angalau kumpunguzia burden ya kiuchumi kiasi fulani?

Naomba Invisible na wadau wengine mtoe mwongozo kwenye hili...
Mkuu wewe kijana wa lumumba mmezoea kula michango ya watu kupitia matatizo yao , mkuu Invisible simamia hii issue hata kwa kuweka namba ya mpesa lakini siyo huyu tapeli wa lumumba
 
Last edited by a moderator:
Acha kujikomba komba na kutafuta umaarufu wa kisiasa kupitia ajali za watu wewe gamba.

Hili ndiyo tatizo letu umeishaleta habari za siasa
watu wanadhani mkiwa tofauti misimamo mnakuwa maadui hapa mkuu, Maxence ndiyo mdau mkuu hapa JF.

Wala hakuna sehemu alipojikomba mwenzetu Maxence kapata matatizo kuna haja ya sisi wanafamilia ya JF kumsaidia kwa chochote siyo pole za maneno wakati kuna matibabu yanaitaji pesa kama anavyosema bado anaumwa hujui kwa matibabu yetu bongo bado anatatizo, JF tumekuwa na utaratibu wa kuwasaidia wenzetu wanaopatwa na majanga baadhi ya members tunafanya ivyo.

Gari hilo limechoka linaitaji kutengenezwa haliitaji pole hata wewe inaweza ikatokea ukapata tatizo JF kama mwezao ukasaidia kwa kidogo kitakachopatikana.

Mkuu Invisible, fanya utaratibu mwenye chochote atupie kwa ajili ya matibabu na matengenezo ya gari.
 
Last edited by a moderator:
Poleni sana Mkuu Maxence Melo ila to be fair hii habari ipelekwe jukwaa husika; hapa Jukwaa la Siasa sio mahali pake. Once again poleni sana.
 
Last edited by a moderator:
Acha kujikomba komba na kutafuta umaarufu wa kisiasa kupitia ajali za watu wewe gamba.

Mkuu migisha... Msome Ritz huo ni ujumbe tosha kwako. Tujitahidi kuepusha mzaha katika masuala ambayo yapo serious sababu tu wazo limetolewa na mtu ambae ni kikawazo kwako. Hiyo ni moja ya dalili ya kutokomaa kifikra na ki umri pia.

Mkuu wewe kijana wa lumumba mmezoea kula michango ya watu kupitia matatizo yao , mkuu Invisible simamia hii issue hata kwa kuweka namba ya mpesa lakini siyo huyu tapeli wa lumumba

Mama toto samahani, lakini umemsoma Zemarcopolo vizuri?

Hili suala si Siasa... Si siasa kabisa. Ndio; Maxence yupo hapa kapost na katoa Shukrani zake, ila haina maana kuwa kila kitu sasa kipo sawa na back to normal ama kua sasa ndio kapona kabisa (Suala ambalo majority haipo aware)!

Marcopolo kaliangalia suala hili ki utu na ubinadamu, hakuna haja ya kumshambulia kwa hoja zisizo hoja. Hajasema kua anataka kuchangisha... Anauliza maswali ambayo kimsingi umeyaruka na hujajibu bado. Na pia kamuomba huyo huyo Invisible uliyemtaja wewe kwa ajili ya muongozo. Tafadhali tuepusha kuleta dimba za Siasa katika hili suala. There was no need ya masuala ya Lumumba hapa.
 
Last edited by a moderator:
Hii thread tangu imewekwa naifuatilia. Naona wadau wametoa pole nyingi sana, nikiwemo mimi.

Lakini najiuliza hivi pole is the best we can do to a person who created JamiiForums anapopatwa na tatizo kubwa kama hili?

Guys, we can do more than empty words. Nilishashambuliwa earlier kwa kusema hivi ndio maana nimejaribu kukaa kimya may be mtu mwingine atasema lakini naona masaa yanazidi kwenda na zinamwagika pole za maneno tu.

Pole ni nzuri lakini mdau gari lake mmeliona hapo. Je, tunaweza kufanya pole ya vitendo, ambayo itamuwezesha kupata a car similar to that? Au angalau kumpunguzia burden ya kiuchumi kiasi fulani?

Naomba Invisible na wadau wengine mtoe mwongozo kwenye hili...

Kaka umeongea suala la msingi saana... Hili suala tupo pamoja na nipo radhi kabisa kuhusika moja kawa moja kuhakikisha linafanikiwa endapo likapitishwa lifanywe.

Kushambuliwa kwako hakuepukiki sababu kiota chako ni Jukwaa la Siasa. Bahati mbaya sana ni kua baadhi ya wanajukwaa hili hukosa hekima/busara na ufikiri. Anapowasiliana na mtu ambae anakutana nae Siasa yeye ni malumbano tu. Na hii inawezekana wengi pengine ni watoto wadogo hasa tokana na kua access ya net ipo sasa hadi kwa wadogo zetu ambao hawajakomaa kiakili na pengine hawakustahili kujihusisha katika mijadala inayohitaji utulivu wa akili na mawazo. Hivyo tokana na uchanga wake huo kazi ni kukurupuka.

Kuna lingine pia... Utayari na nia ya members. Tunaweza kutoa wazo hapa kua hili lipitishwe; wanao toa ahadi wanakua wengi sana, ila watendaji ni wachache. Ni suala ambalo linasikitisha kwa kweli... Hata hivyo wacha tuwasiliane na Utawala tuone nini kifanyike.

Nashukuru kwa mawazo yako. Pamoja Saana.
 
Mkuu Maxence anayestahili kupewa shukrani ni Mungu kwani sioni ni katika mazingira gani mtu angeweza toka mzima hapa kama si mkono wa Mungu kumkinga.
Katika hali kama hii yatosha kuendelea kumtukuza Mungu!!!. Tunakuombea upone haraka kiongozi.
 
wema wa mungu umewazunguka bro! poleni xana xana!!!!! mods mngeweka kautaratb kakusaidiana kwa jf members kwenye ishu tyt kama iz, leo max kesho mim au wewe.. xamahan kama kuna in4 sijaiona wakat napost.
 
Poleni sana Melo na mdogo wako, M/Mungu awajaalie maisha marefu zaidi, pia huwa nina mtazamo kuwa mara nyingi ni vizuri kutosafiri pamoja kwa ndugu moja kabisa kama kaka, dada au mdogo mtu na pia baba, mama na watoto unless iwe ni lazima sana kusafiri pamoja. Kwa mara nyingine poleni sana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom