kikoozi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2015
- 2,030
- 2,929
Ndugu zangu, niende moja kwa moja kwenye mada yangu, baada ya kutafuta kazi muda mrefu mpaka nikahisi nimerogwa pasipo mafanikio yeyote yale, hatimaye Mungu akaniona nikapata kazi kwenye mradi mmoja hapa hapa nchini, ndani ya mwaka mmoja nimejipinda na kujichanga aswaaaa mpaka ninapoongea na ninyi nimefikisha Milioni 15, ndugu zangu huko nyuma nimepitia maisha magumu mno ya kukosa ajira, nilishindwa ata kupata hela ya kula kwa siku wala ya kubadilisha nguo zangu za ndani, na hii project imeshakwisha.
Wana Jamii Forums, najua humu kuna watu wana mawazo bora na yenye kujenga naombeni mnishauri. Kwa mawazo yangu, mpaka sasaivi yapo hivi:
Je kama ni wewe una milioni hizi 15 ungefanyaje na umetoka maisha magumu mnooo ya kukosa ajira kwa muda mrefu.
Wana Jamii Forums, najua humu kuna watu wana mawazo bora na yenye kujenga naombeni mnishauri. Kwa mawazo yangu, mpaka sasaivi yapo hivi:
- Nitoe milion 2.5/3 nikanunue eneo (kiwanja) maeneo ya Mwanza. Nataka eneo kubwa na zuri ambalo ntaweza kufanya maisha yangu na kufanya ufugaji (eka moja sio mbaya).
- Nitoe milion 6 nijenge vyumba viwili na sebule basi kwaajili ya kuweka mtu akae wa kuniangalizia eneo langu (hapa nimelenga kuwa, sitakosa mtu ambaye naweza kumweka sehemu yangu akakaa kwa ajili ya kuniangalizia ufugaji wangu wakati huo huo mimi nikikimbizana na maisha mengine ya utafutaji) note: hapa sijajua changamoto yake itakuwaje maana sina uzoefu wa kumpa mtu eneo akae kwaajili ya kukuangalizia eneo na uzalishaji wako wa ilo eneo.
- Pesa inayobaki nianze kufanya biashara sijajua biashara gani aswaa ila nilifikiria kati ya kununua mazao kwa wakulima na mimi kwenda kuuza kwa wanunuzi (hapa sijawahi kuifanya hii biashara).
Je kama ni wewe una milioni hizi 15 ungefanyaje na umetoka maisha magumu mnooo ya kukosa ajira kwa muda mrefu.