Mawazo yangu binafsi, naombeni na ushauri wenu juu ya hii Milioni 15

kikoozi

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
1,263
2,000
Ndugu zangu, niende moja kwa moja kwenye mada yangu, baada ya kutafuta kazi muda mrefu mpaka nikahisi nimerogwa pasipo mafanikio yeyote yale, hatimaye Mungu akaniona nikapata kazi kwenye mradi mmoja hapa hapa nchini, ndani ya mwaka mmoja nimejipinda na kujichanga aswaaaa mpaka ninapoongea na ninyi nimefikisha Milioni 15, ndugu zangu huko nyuma nimepitia maisha magumu mno ya kukosa ajira, nilishindwa ata kupata hela ya kula kwa siku wala ya kubadilisha nguo zangu za ndani, na hii project imeshakwisha.

Wana Jamii Forums, najua humu kuna watu wana mawazo bora na yenye kujenga naombeni mnishauri. Kwa mawazo yangu, mpaka sasaivi yapo hivi:
  1. Nitoe milion 2.5/3 nikanunue eneo (kiwanja) maeneo ya Mwanza. Nataka eneo kubwa na zuri ambalo ntaweza kufanya maisha yangu na kufanya ufugaji (eka moja sio mbaya).

  2. Nitoe milion 6 nijenge vyumba viwili na sebule basi kwaajili ya kuweka mtu akae wa kuniangalizia eneo langu (hapa nimelenga kuwa, sitakosa mtu ambaye naweza kumweka sehemu yangu akakaa kwa ajili ya kuniangalizia ufugaji wangu wakati huo huo mimi nikikimbizana na maisha mengine ya utafutaji) note: hapa sijajua changamoto yake itakuwaje maana sina uzoefu wa kumpa mtu eneo akae kwaajili ya kukuangalizia eneo na uzalishaji wako wa ilo eneo.

  3. Pesa inayobaki nianze kufanya biashara sijajua biashara gani aswaa ila nilifikiria kati ya kununua mazao kwa wakulima na mimi kwenda kuuza kwa wanunuzi (hapa sijawahi kuifanya hii biashara).
Naombeni mawazo yenu wana JF.

Je kama ni wewe una milioni hizi 15 ungefanyaje na umetoka maisha magumu mnooo ya kukosa ajira kwa muda mrefu.
 
Napoleone

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
7,448
2,000
Bwana mdogo...mawazo nitakayokupa hapa wenzio hulipia ila sabab malaika wako mkubwa leo wacha nikupe mawazo.

1.achana na kwenda mwanza..kama uko dar..nenda rufij au bagamoyo kuna maeneo nayajua ekar utapata kwa lak4..ila angalizo..ukienda usinunue nunue tuu...kule kuna maeneo fertile na maeneo ambayo sio fertile...chkua ekar zako 4...fanya hyo mambo ya ufugaj
Hyo nyumba ya kujenga jenga vyumba viwil visizid mil5..yaan hapo kiila kitu.

Hela inayobak..mil5..weka bank..ipige fix kabisaa...sasa hyo nyingne inayobak ndo uanze hangaika nayo..na tena usianze biashara ya zaid ya 2m....yaan rud 0 kabisa..kama huna aibu anza kukomaa.hakikisha hyo biashara inakupa hata elf10 kwa siku.

Na hapo ndo kwenye mtihan.umiza sana kichwa kujua ufanye biashara gan...sabab amini nakwambia..ukifata ushaur wa watu wanaokwambia uanze tu biashara na hyo hela..hela yoote hyo itaisha na hutaamin ila utanikumbuka.

Na pia hyo biashara unayoanza usianze tu mwenyew..tafuta mentor yaan mtu ambae tayar anafanya nawew uingie kat hapo.mwombe akuelekeze anafanyaje uende nae sawa..

Nmemaliza.
 
mukaruka mzee

JF-Expert Member
Jan 22, 2020
915
500
Bwana mdogo...mawazo ntakayokupa hapa wenzio hulipia ila sabab malaika wako mkubwa leo wacha nikupe mawazo...
1.achana na kwenda mwanza..kama uko dar..nenda rufij au bagamoyo kuna maeneo nayajua ekar utapata kwa lak4..ila angalizo..ukienda usinunue nunue tuu...kule kuna maeneo fertile na maeneo ambayo sio fertile...chkua ekar zako 4...fanya hyo mambo ya ufugaj
Hyo nyumba ya kujenga jenga vyumba viwil visizid mil5..yaan hapo kiila kitu...

Hela inayobak..mil5..weka bank..ipige fix kabisaa...sasa hyo nyingne inayobak ndo uanze hangaika nayo..na tena usianze biashara ya zaid ya 2m....yaan rud 0 kabisa..kama huna aibu anza kukomaa.hakikisha hyo biashara inakupa hata elf10 kwa siku...

Na hapo ndo kwenye mtihan.umiza sana kichwa kujua ufanye biashara gan...sabab amini nakwambia..ukifata ushaur wa watu wanaokwambia uanze tu biashara na hyo hela..hela yoote hyo itaisha na hutaamin ila utanikumbuka...

Na pia hyo biashara unayoanza usianze tu mwenyew..tafuta mentor yaan mtu ambae tayar anafanya nawew uingie kat hapo.mwombe akuelekeze anafanyaje uende nae sawa..

Nmemaliza.
Pia kwa kuongezea kwa hayo aliyokuambia Napoleone hapo juu, fanya biashara unayo IPENDA. Hata kama ni kujifunza kwa huyo mentor, jifunze biashara unayo IPENDA. Jifunze kwa moyo wako wote hata kama itakubidi kuchangia kidogo, changia, ili mradi upate hayo MAUJUZI unayotafuta.

Chukua muda wa kutosha then ukishaifahamu hiyo biashara basi na wewe tafuta "goli" au eneo lako na usonge mbele. Tusifanye hizi biashara kwa kufuata mkumbo, tutakumbwa na matatizo jamani.
 
  • Thanks
Reactions: rr3

Kamawewe

JF-Expert Member
Jan 16, 2013
473
500
Mkuu ili nikupe mawazo naomba kujua kwenye hiyo project ulikuwa unafanya kazi gani, umesoma hadi kiwango gani na profesion gani (ata kama la saba haina shida), sasa hivi unaishi wapi na uko tayari kuhama unapoishi?
 
masagati

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
469
500
Nilisha wahi nunua duka miaka ya nyuma na lipo mpaka leo , nilisha wahi nunua kijiwe cha chipsi mikocheni kipo mpka leo ingawa nakosa mapato kwenye hii biashara ya chips kwakuwa nakosa muda wa kusimamia ila nikiwekeza pesa kidogo na muda wa kusimamia napata hela bila shida.
 
Self-made

Member
Oct 14, 2020
7
45
Mimi kwanza ndio bado sina kaziii na wala sina ata mia hapa na jana sijala nimekosa hela kama ulivyokuwa unakosa wee mkuuu emb. Nipe ata mchongo naweza fanya nipate na mm hela. Nina elimuu ya chuo kikuuu tena ud . Emb okoa jahazii mm naweza beba ata zege tuanzie hapa alafu hio milion 15 tutajua tu tutumieje😂😂
 
Mc cane

JF-Expert Member
May 18, 2018
5,231
2,000
Wazo la zaidi ya fedha uliyopata (Tsh. 15,000,000) kumkabidhi mtu akuzalishie ni moja kati ya mawazo mabaya ya kibiashara uliyowahi kuyawaza

Kwa kuwa huna kazi kwa sasa, popote utakapoweka hela yako na wewe uwepo hapo
 
lontor

Senior Member
Apr 5, 2017
183
1,000
Bwana mdogo...mawazo ntakayokupa hapa wenzio hulipia ila sabab malaika wako mkubwa leo wacha nikupe mawazo.

1.achana na kwenda mwanza..kama uko dar..nenda rufij au bagamoyo kuna maeneo nayajua ekar utapata kwa lak4..ila angalizo..ukienda usinunue nunue tuu...kule kuna maeneo fertile na maeneo ambayo sio fertile...chkua ekar zako 4...fanya hyo mambo ya ufugaj
Hyo nyumba ya kujenga jenga vyumba viwil visizid mil5..yaan hapo kiila kitu.

Hela inayobak..mil5..weka bank..ipige fix kabisaa...sasa hyo nyingne inayobak ndo uanze hangaika nayo..na tena usianze biashara ya zaid ya 2m....yaan rud 0 kabisa..kama huna aibu anza kukomaa.hakikisha hyo biashara inakupa hata elf10 kwa siku.

Na hapo ndo kwenye mtihan.umiza sana kichwa kujua ufanye biashara gan...sabab amini nakwambia..ukifata ushaur wa watu wanaokwambia uanze tu biashara na hyo hela..hela yoote hyo itaisha na hutaamin ila utanikumbuka.

Na pia hyo biashara unayoanza usianze tu mwenyew..tafuta mentor yaan mtu ambae tayar anafanya nawew uingie kat hapo.mwombe akuelekeze anafanyaje uende nae sawa..

Nmemaliza.
Mleta mada chukua hii madini
 
danielhipoliti

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
358
500
Nakubaliana kabisa
Wazo la zaidi ya fedha uliyopata (Tsh. 15,000,000) kumkabidhi mtu akuzalishie ni moja kati ya mawazo mabaya ya kibiashara uliyowahi kuyawaza

Kwa kuwa huna kazi kwa sasa, popote utakapoweka hela yako na wewe uwepo hapo
 
Patroman

JF-Expert Member
Nov 12, 2018
636
1,000
Chagua kufanya biashara Kati ya hizi tatu.....duka la vipodozi na urembo.....duka la chakula na nafaka....na duka la miamala ya fedha....baada ya miaka mwaka mmoja leta mrejesho hapa.... biashara njema.
 
Fighter23

Member
Sep 22, 2019
34
125
Tafuta eneo zuri maeneo ya makazi ya watu kisha jenga banda zuri la Biashara ya kuonesha live soccer matches, movies, na betting agency. Hutatumia mtaji mkubwa na rahisi kupata mapato mazuri kwa kipindi kifupi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom