Mawazo ya wasomi wetu tanzania

ommy15

JF-Expert Member
Jan 23, 2011
648
814
Habari zenu wanaJF,nimatumaini yangu wengi ambao niwadau wa hili jukwaa ni wanafunzi wa vyuo,wahitimu na watarajiao kuwa wanavyuo. Ila kuna malumbano ambayo mara nyingi nimeyakuta hasa kwenye jukwaa hili la elimu,hii hasa ni juu ya chuo kipi eti ni bora Tanzania yaani udsm vs mzumbe,udsm vs udom,mzumbe vs sua. Mm binafsi sijawahi vutiwa na mjadala huu na kwa watu wasomi wavyuo vikuu kama nyie mnaoanzisha mjadala na kuchangia,narudia sijawahi vutiwa wala kufurahishwa kwani michango na mada zenyewe zinadharaurisha na kushusha hadhi zenu na za vyuo vyenu.Kwani baadhi yenu mnafikia hadi kuwaona wenzenu mbwa koko! Kweli hii ndio kazi ya wasomi,hii ndio kazi ya JAMIIFORUMS(The home of Great thinkers)? Mfano ni thread yenye kichwa "ubora wa digriiza udom na st.joseph". Hapa nlishindwa kuelewa kuanzia aliyeanzisha mjadala hadi wachangiaji(sio wote) kwamba nini hasa wanajifunza huko kwenye chuo bora Tanzania{UDSM} kwani naona jinsi wasivyokuwa na uelewa wa usomi na kazi ya msomi ktk jamii yake.
Kwa upande wangu msomi ni mtu mwenye uwezo wa kutambu,kuchanganua na kutatua au kupendekeza njia za kumaliza matatizo yaliyopo ktk jamii,na hii ndo iliyokuwa sifa kubwa na ya pekee kwa wasomi wa mlimani kipindi cha nyuma(enzi za kina Prof.Issa Shivj,Tundu Lissu)na wengine ambao hadi leo tunaona mchango wao ktk jamii. Wanafunzi wengi wa mlimani wasasa mnadharau sana vyuo vingine sijui hapo mnaifundisha nini jamii yetu.
kweli matatizo yapo sio udom,st,Joseph,muccobs tu hata hapo kwenu pia,pili mkumbuke waliochaguliwa udom au st.joseph mlisoma nao huko mashuleni na wengi wanauwezo kama wenu na hata kuwashinda baadhi yenu ila hilo hamliangalii kwani mnakiburi cha historia ambayo hamjaijenga nyie bali mnafanya juhudi kubwa kuibomoa.Kama kweli nyie niwanafunzi bora na mmegundua kwamba vyuo hivyo havina ubora mbona sijawahi sikia mmetoa mapendekeza kwa waziri anayehusika au serikali nini kifanywe(kama udsm ya miaka ya nyuma). Acheni ushabiki kwani hamjengi elimu yetu mnabomoa hivyo nategemea siku1 mtagoma kushiniza serikali iwapatie udom,st.joseph,sua,muccobs,tumaini n.k walimu bora kama wenu.
Kwakifupi malumbano yenu hayaoneshi kama kweli nyie mnaweza kupambana na changamoto za maisha ambazo zinahitaji wasomi ambao ni waadilifu,hawana majivuno na dharau,pia kusoma kwenye chuo bora africa au duniani bado wewe binafsi unaweza usiwe bora kwani mifano ipo ni wangapi wamemaliza mzumbe,udsm lakini wanafanya madudu jiulizeni wanaoingia mikataba ya kijinga nchini walisoma wapi? Hivyo basi nadhani ifike sehemu jukwa hili liwe sehemu ya kuheshimika na kuheshimiwa lakini kwa jinsi ilivyo sasa tunajidhalilisha kama wasomi na watanzani coz we dont think of solutions to our problems.
Jiulize ww kama msomi wa chuo bora utasaidia vipi kuleta ubora wa elimu nchini nasio malumbano yasiyo na tija,kuna mambo mengi ya kujadiliana humu mfano jinsi gani wanamzumbe,wanasua,wanaudom,wanudsm etc mnaweza nufaika na jumuia ya afrika mashariki.Remember the life that you are livng u didnt choose but that life choosed u.
 

Renegade

JF-Expert Member
Mar 18, 2009
6,680
5,819
Wasomi wa Tanzania wamechoka, ndio maana wanajadili vyeti badala ya quality ya mtu, wengi wao usipokuwa na cheti cha Mlimani kwao hujasoma, Hawataki kuviona vyeti vya vya vyuo vingine, Japo wengi wao wamekalia viti ofisini kwa kupewa na wajumba zao, inapofika wakati wa kuajiri wanajifanya kuangalia vyuo. Wasomi hawafanyi tafiti, wakifanya tafiti matokeo wanafungia kwenye makabati yaliyojaa vumbi, tafiti zao nyingi ni feki kama siyo COPY AND PASTE. Wengi wanataka kutajirika haraka haraka.Wanakimbilia kwenye Siasa, hawana ujasiri wala Vision ya kuiokoa Tanzania kwenye Janga la Usultani wa CCM. Wamebaki wapiga porojo tu, maneno yao yanaenda na upepo. Hakuna jipya Tanzania, nchi inaliwa, haiendi mbele inarudi nyuma. Inachosha sana. HAKUNA JIPYA.
 

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,536
5,642
Tatizo watanzania hatupendi kuambiwa ukweli. Ubora wa hivi vyuo unatofautiana. Mijadala kama hii ni muhmu ili kuongeza chachu. Elimu ya Udom, st.joseph, Kiu n.k unaweza kulinganisha na Mlimani au Sua?
Mijadala ni muhimu ili jamii itambue upupu unaofanywa ktk elimu zetu.
Mimi binafsi naipenda sana hii mijadala.
 

Perry

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
10,019
1,762
Me nadhan huo huwa ni ule utani wa kishule 2,ebu maliza chuo uende mtaani ndo utajua kama kuna cha udsm,sua,iaa,ifm,udom,mzumbe wala saut..cku hzi waajiri wengi wameisha zinduka..wanaangalia nin alicho nacho graduate kichwani na co chuo alicho soma.
 

Engager

JF-Expert Member
Jan 12, 2011
327
65
Tatizo watanzania hatupendi kuambiwa ukweli. Ubora wa hivi vyuo unatofautiana. Mijadala kama hii ni muhmu ili kuongeza chachu. Elimu ya Udom, st.joseph, Kiu n.k unaweza kulinganisha na Mlimani au Sua?<br />
Mijadala ni muhimu ili jamii itambue upupu unaofanywa ktk elimu zetu.<br />
Mimi binafsi naipenda sana hii mijadala.
<br />
<br />
ha ha ha.... Mijadala isiyo na outcome (solution) unaipenda?? Ar u a realy grt thinker dah! Pole mtz komaa kulaum serikali.
 

AshaDii

Platinum Member
Apr 16, 2011
16,219
17,980
Na nukuu: "tuwe tunaandika kwa aya" - JF Member


(narudi Mkuu na proper post... ila by the time being Please work on the above)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom